ADC - Kitaweza kuvunja ngome ya Chadema, CUF? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ADC - Kitaweza kuvunja ngome ya Chadema, CUF?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hasan124, Sep 5, 2012.

 1. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Home [​IMG] Makala [​IMG] Siasa [​IMG] ADC: Kitaweza kuvunja nguvu ya Chadema, CUF?


  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]ADC: Kitaweza kuvunja nguvu ya Chadema, CUF?[/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 05 September 2012 13:38[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  •Dira ya mabadiliko, tumaini la Watanzania
  Na Mwandishi Wetu
  HAYAWI hayawi, hatimaye yamekuwa, ni maneno yaliyokuwemo kwenye nyimbo na vipeperushi vya Chama kipya cha siasa cha Alliance for Democratic Change, ADC kilichopata usajili wa kudumu mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Chini ya kiongozi wake wa taifa, Said Miraji ADC kimefanikiwa kupata usajili wa kudumu baada ya kujikusanyia wanachama waliokidhamini katika mikoa kumi ya Tanzania Bara na Visiwani.
  ADC imepata hati ya usajili wa kudumu baada ya kukamilisha masharti waliyopewa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, wakati walipokabidhiwa usajili wa muda mwezi machi mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Chama hicho, Said Miraji anasema ADC itaanza kufanya mikutano ya hadhara kwa lengo kuandikisha wananchama wengi zaidi ili chama hicho kiweze kupata ushindi wa kishindo wa madiwani, wabunge na rais mwaka 2015.
  Je kitaweza kupenya katika ngome za vyama vya CUF na Chadema? Miraji anasema, "Kwanza nieleze wazi tunaingia katika ulingo wa siasa na chama kipya tukiwa umejipanga vilivyo, sisi hatukukurupuka tumefanya utafiti na kuamua kuingia ulingoni kwa makusudi na malengo ya kuleta mabadiliko, na wananchi wataona mabadiliko"
  Anasema ADC inaingia katika ulingo wa siasa ikimtazama mshindani wao mkubwa kuwa ni chama tawala na sio chama chochote cha upinzani iwe CUF wala Chadema na kwamba watatafuta mtaji mahali penye watu.
  Anaongeza kuwa ADC kinalenga kujipatia wafuasi na wanachama kutoka miongoni mwa watanzania zaidi ya milioni 30 wasioridhishwa na mienendo ya vyama vya siasa vilivyo na usajili na ambavyo vinafanya siasa hapa nchini.
  Anasema chama hicho kitaendesha siasa za kistaarabu na kwamba vurugu hazitakuwa na nafasi.
  Anaongeza kuwa katiba ya chama hicho sio ya mtu mmoja wala watu 100 na kwamba imeainisha mambo yote yatakayoondoa udikteta na kutoa haki kwa baadhi ya viongozi huku ikiwasahau wanachama na wananchi wanaokiunga mkono.
  Anasema katiba ya ADC imezingatia ukomo wa madaraka na kuweka kamati maalumu ya usuluhishi ambayo haitawahusisha viongozi wa juu wa chama ili kuepuka kuwafukuza ovyo wanachama wake hasa wanapofanya makosa ambayo yanaweza kurekebishika, au pale wanapohitilafiana na uongozi wa kitaifa.
  "Katiba yetu inamlinda kila mwanachama, sisi sote ni wanachama na viongozi tuliochaguliwa tunaongozwa na katiba. Chama hiki hakina mwenyewe watu wanaruhusiwa kuja kujiunga wasisubiri mpaka wafukuzwe katika vyama vingine ambavyo havijui umuhimu na thamani ya wanachama," anasema Miraji
  Anasema wanasiasa walio kwenye vyama visivyo na msimamo na ambao wanasimama katika msingi wa haki na uadilifu, wanakaribishwa kujiunga na chama hicho ili waweze kutetea haki za wananchi na kutoa mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
  "Tutasimamia kwenye ukweli, tutakuwa tayari kukosolewa pale yatakapojitokeza mapungufu…lengo letu kuu ni kujenga taifa lenye neema," anasema Miraji.
  Miraji anasema ADC ni dira ya mabadiliko itakayoleta tumaini kwa watanzania na kwamba alama ya nyota iliyopo katika chama hicho ni ya kuwamulika na kuwatoa wananchi wa Tanzania kwenye giza.
  Anasema Chama hicho hakitaki mawakala na badala yake kinataka wawakilishi na kitakuwa tofauti na vyama vingine ambavyo viongozi wake wamekuwa wakila kwa niaba ya wananchi na sio kufanya kazi ya kuwakomboa na kuwatetea na ukandamizaji unaofanywa na watawala.
  Miraji anaongeza kuwa msingi wa uongozi katika chama hicho kipya ni kuwa na hofu ya Mungu na kutangaza kuwa Chama chake hakitampokea mwanachama yeyote anayetuhumiwa kwa kufuja mali ya umma.
  "ADC itasimamia misingi ya uadilifu. Tunasema haya kwa dhati kwa kuwa wote tunayo hofu ya Mwenyezi Mungu…hatutaki na hatutampokea mwanachama yeyote ambaye anatajwa katika ufisadi na ulaji rushwa" anasema.
  Watu mbalimbali waliohudhuria mkutano huo mkuu wa kwanza wa chama hicho kipya walitoa nasaha zao akiwemo mshiriki wa karibu wa viongozi wa Chama hicho, na mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed ambaye alitambulishwa kama mlezi wa chama hicho.
  Akawakumbusha viongozi waliochaguliwa katika mkutano huo kutotumia vibaya midomo yao kwa kutoa kauli za kibabe, matusi, vitisho na udhalilishaji kwa kisingizio chochote kile kwani kufanya hivyo watashindwa kulinda na kuendeleza urithi na maadili ya kitaifa.
  Anasema ADC, imeanzishwa katika kipindi cha changamoto hasa kwa vyama vya upinzani kuwa na kazi ya ziada katika kupigania maendeleo ya kidemokrasia huku vikitafuta ridhaa ya wananchi ili kupewa dhamana ya kuongoza.
  "Ukweli vyama vya siasa vinakabiliwa na mazingira mazito na kutoshindana na CCM pekee, bali vinashindana na kundi kubwa la taasisi za umma na binafsi ambazo zimejaa makada wa CCM,
  Anasema moja ya matatizo yanayoathiri upinzani ni kukosa ajenda ya pamoja ya kudumu ambapo anasema baadhi ya vyama vya siasa vimejikuta vikiingia katika ushindani baina yao, badala ya kuwa na makakati wa pamoja wa kuiondoa CCM madarakani.
  Akitoa salamu zake katika mkutano huo Hamad Rashid alivunja ukimya na kutamka kuwa yupo tayari kujiunga na Chama hicho endapo kitapinga ubinafsi kwa ajili ya maslahi ya taifa.
  "Nami nipo tayari kujunga na ADC, wakati wowote huko mbele ikiwa mtaongoza kwa kuepuka migogoro na kauli za kibabe za sasa bwana mkubwa amesema, na badala yake kusimamia misingi ya kuwa kioo cha jamii, na kuwasemea wananchi wanyonge bila kujali itikadi, imani zao au maeneo wanayotoka" anaongeza.
  Hamad, anawaonya viongozi wa ADC kuepuka na kuwakataa viongozi walevi wa madaraka ambao anasema viongozi wa namna hiyo hutumia muda mwingi kutatua migogoro ya ndani, kuliko kuwasaidia Watanzania kuondoa matatizo yanayowakabili.
  "Ulevi wa madaraka ni tofauti na ule wa pombe. Hakuna dalili ya kuumwa kichwa wakati wowote unapokuwa madarakani, hautoki mwilini mpaka ufe au ufukuzwe. Na humfanya mtu awe haoni wala hasikii na hafahamu isipokuwa yale anayoyataka yafanyike kwa kutumia nguvu za maamuzi, muwaepuke viongozi wa aina hii" anaonya.
  Anasema katika kipindi cha miaka 20 ya mfumo wa vyama vingi nchini, watanzania wamekata tamaa na kuachwa njia panda na wanasiasa waliowaamini na kuwasikiliza wakati wote na kwamba ili kurejesha tumaini lililopotea kwa wananchi, viongozi wa ADC wanapaswa kuwa tofauti na aina hiyo ya viongozi.
  Hamad anaongeza kuwa chanzo kikuu cha kukosekana kwa demokrasia ndani ya vyama vingi vya siasa inatokana na tabia za viongozi walevi wa madaraka ambao hutumia muda mwingi kutatua migogoro ya ndani kuliko kuwasaidia Watanzania kuondokana na lindi la umaskini, ujinga na maradhi.
  Anasema ni hatari kubwa kuona watanzania wengi wanashindwa kumudu gharama za maisha ikiwa ni pamoja na kukosa uwezo wa kumudu kupata mlo na baadhi yao kufa kwa njaa, pamoja na maradhi yanayotibika na wanashindwa kuingia kwa wingi katika ushindani wa ajira ulimwenguni na wa kibiashara huku wakiwa na viongozi .
  "ADC inatakiwa itimize lengo lake na kuleta mabadiliko na kuwa tumaini kwa Mtanzania, viongozi muwe na dhamira ya kuijenga taasisi kwa faida ya taifa na si kwa faida yenu" anasema.
  Hamad anaongeza kuwa ni lazima kwa taasisi inayojijenga kama ADC iwe na itikadi ambayo inaunganisha nafsi na viwiliwili vya wafuasi wake ili walitimize lengo la kuwapo kwake.

  Source: MWANANCHI Newspaper.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Karibuni ila kama hamuwezi siasa za fujo na mapambano basi hamfai hata kuitwa chama cha siasa ,hivi mtakuwaje cjhama cha siasa kama hamjajiandaa kupambana ,waTanzania wa leo wameshachoka na vyama vya siasa za kistaarabu.

  Tunajua chama kimoja tu ambacho kina siasa za jino kwa jino ,wanangangari CUF ambao hivi sasa wapo machimboni wakikusanya zana nzito.Kidogo wametulia na kuipisha CDM kuona nguvu zake zitaishia wapi,CDM wakipigwa mkwala tu basi ujue ,wanangangari hawana sumile tena ,ni ngangari mpaka kieleweke ,na safari hii kwa taarifa tu mambo mpaka kwenye viwanja vya ikulu.
   
 3. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa nini tufikirie kitavidondosha CDM na/au CUF wakati bado hakijaweza wa TLP na UDP??? CDM na CUF bado ni level zingine kwa vyama vya upinzani...!!
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,213
  Likes Received: 10,555
  Trophy Points: 280
  Ndoto za Alinacha.
   
 5. d

  davidie JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna chama cha upinzani na chama cha ushindani sasa mimi naona adc ni chama cha ushindani na vyama vya upinzani sio chama cha mlengo madhubuti wa kisiasa.
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwani lengo la ADC ni kuidondosha CDM au CCM ili kuchukua dola? Kama lengo lake ni kuidondosha CDM basi hakifai na kimekufa kabla ya kuzaliwa. Kinachotakiwa na watanzania kwa sasa ni chama au vyama vitakavyoweza kuwaongoza kuondokana na joka kuu CCM ambalo limevuruga maisha na mastakabali wao. Hivyo, kama ADC kimeundwa kuidondosha CDM kitadondoka hata kabla ya kuingia vitani. Laiti kingedhamiria kukosoa makosa ya CUF ambayo ndilo chimbuko la chama hiki. Kama kitakamia kuiangusha CDM basi kitakuwa pandikizi na nyemelezi la CCM. Heri wahusika watambue hili haraka na kuachana na mipango uchwara ya kuangusha wengine.
   
 7. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huna lolote, unaleta viswahili tu hapo!! Kitu gani ambacho hujaelewa hapo
   
 8. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwanini usiseme ADC inaweza vunja ngome ya CCM? kwani hao CDM na CUF ndiyo wanaotawala nchi hii?
  Ama kweli chama cha upinzani hapa Bongo kipo kimoja tu' nacho ni CDM. Utaki unaacha
   
 9. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,465
  Trophy Points: 280
  Kumbe ADC malengo yake ni kuvunja nguvu ya chadema na cuf na sio kushika dola dhidi ya ccm.!
   
 10. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  CCM ni watu hatari sana! yaani wameipa ADC usajili wa kudumu tena kwa fasta fasta ili chama hicho kije kupambana na vyama vya CDM na CUF. So ADC=CCM C
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  AKIMA hamad rashid wana akili za kijinga hawawezi kunishawishi nijiunge ADC

  HIVI LENGO LAO NI KIVIONDOSHA CDM na CUF??
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  ADC ni CUF na hao CUF wameolewa na CCM kwa ndoa ya MUAFAKA.

  ADC hawana sera ni cha Kizanzibara na wale jamaa wa UAMSHO
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Je CDM ni chama cha wakatoriki?
   
 14. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Kumbe ndio maana wakaweka rangi kama za cdm ili wakati wa kupiga kura watuchanganye
   
 15. M

  MTK JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Poor Said Miraji, things are easier said than done! kwa umri wa chama chake ni rahisi sana kwake kuahidi chochote, kuwa rahimu na mwadilifu sana katika kauli zake; but he has to stand the test of time; say in a years time tuone atakuwa anaongea nini; overtime atagundua kwamba maono, mitazamo, mikakati na mbinu za wanachama wake za kufikia malengo yao ya kisiasa zinaanza kutofautiana na hapo ndipo atakapojikuta analazimika kubadili mbinu za uongozi kukidhi mahitaji ya nyakati;

  Miraji asifikirie kina seif sharif hamad na huyo mdhamini wao hamad rashid Mohamed ni mashetani sana kufika hapo walipofikia kutotaka hata kuonana usoni!! life is dynamic and he has to strive to cope with the evolving dynamics in his ADC; lest he has failed hata kabla hajaanza.

  Yetu ni macho na masikio, Best wishes Miraji.
   
 16. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  :bange:vyama vingine bwana....eti mlezi wao yuko ccm B alafu chama kinajiendesha na wavuta bange kadhaa kwa mda.......njaaa mbaya aiseee!!wamegombea ruzuku ccmB wameona waanzishe ADM ili watoto wao wapishane vyooni.....chezeya njaaa....maalimu seif hala yeye peke yake yahe....
   
 17. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mbona CCJ kilinyimwa usajiri wa kudumu?au walifanya ivyo kumkomoa nape na wenzake?
   
 18. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  fraud ppo!...upuuz m2bu!...
   
 19. s

  sad JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  chama hiki waasisi wake ni jumua ya uamsho zanzibar. sasa mbona cuf ina nguvu zanzibar ADC wanapoteza muda kwani sasa kumbe wanataka kugombana na cuf na chadema. mtadondokea pua na kupotea katika siasa za tanzania. hawana jipya. vyama hapa tanzania ni C.C.M, CHADEMA. CUF , NCCR MAGEUZI, TLP na vyama njaa ambavyo havina hata mbunge wala diwani. ADC kwakuwa mumetoka CUF mtakuwa na siasa za CUF tu
   
 20. s

  sad JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ADC c.c.m ina hamu sana kuwatumia kisha musambaratike.c.c.m hata cuf hawaipendi sana ila wanaheshimu ile ndoa tu zanzibar
   
Loading...