Adam Mchomvu hakui?

Adam Mchomvu ni moja kati ya majina makubwa na yenye athari chanya katika muziki wa Tanzania hususani Bongo Fleva!

Amewapa mashavu wana kibao na wanakiri kuwa uwepo wa Adam ulirahisha safari zao za mafanikio katika kiwanda Cha muziki! Zaidi ya asilimia 70 ya wasanii walioibuka kabla ya mapinduzi ya internet wanajua athari za Adam Mchomvu!

Ni miongo kadhaa Sasa tokea nianze kumsikia jamaa. Mshkaji ni mkongwe kweli kweli. First time namsikia alikuwa anamtambulisha Young Dee ni kati ya 2008 au 2007 sikumbuki vizuri.

Baada ya miaka kadhaa nikamsikia anamtambulisha Dogo janja, nikamsikia anamtambulisha Asley.... Marioo..... Young Lunya.... Jamaa hakunji Wala nini yupo cool!

Enzi hizo za Nako 2 Nako jamaa alikuwa wa moto Sana. Hapa Dj Fetty Fetilicious pale Ruben Ndege a.k.a ncha kali halafu Kuna Mr Born 2 shine... Jamaa waliteka vipindi vyote vya mchana wakawa wanatamba wao tu!

Zilikuwa siku njema Sana! Walikuwa vijana halafu wajanja wanaset trend halafu wadau tunaishi nazo!

Huku na huku Ncha kali akasepa akaenda kujitafuta kwanza. Mdogo mdogo Fetty akakaa pembeni ajipange upya!

Hatujakaa sawa Bdozen akahama media! XXL zikaja sura mpya kabisa akina Mumybaby na genge lake kutoka East Africa radio! Mchomvu Yuko pale pale!

Siku zikapita Ruben Ndege akarudi ila this time sio mtangazaji ni boss kabisa yaani sijui kitengo Cha ubunifu sijui maudhui sielewi ila boss! Bdozen akarudi ila kapoa flani sio chekibob kama zamani kwanza brand yake ya born2shine ishakuwa kubwa Sana kimsingi yeye ni boss! Mara Fetty na yeye karudi ila this time kaenda vipindi vya akili nyingi anahoji waheshimiwa yaani yupo kwenye vipindi vinavyohusu taifa! Vipindi vinavyotoa dira ya taifa! Mchomvu Yuko pale pale! Bado chekbob vile vile, muhuni muhuni vile vile! Watu wake akina Young Lunya!

Anapiga watu ngwala kuanzia stejini Hadi studio! Anakaa kihuni huni anavaa milegezo kama yupo kwenye balehe! Ni mtangazaji tu tangu mwaka 2008 Hadi Leo! Hana nafasi nyingine mjengo zaidi ya ukongwe!

Ina maana huyu jamaa amestuck hapo au! HAKUI, atatangaza bongofleva XXL Hadi uzeeni! Haoni haja ya kukua kitaaluma, kinafasi na hata kimtazamo?

Au Mimi ndio sielewi?

"Tatizo Adam Mibangi" - Emmanuel Mbasha.
 
Kabla hata hajaja clouds fm Adamu Mchomvu amevuruga sana back in 2000's pale Mbeya fm/ Bomba fm huko mbeya.... Jamaal ni mkongwe haswa. Enzi hizo anajiita Tall wa ajabu.
 
Fetty juzi amekula kitengo, boss. Ncha kali kala kitengo, boss. When it comes to Fiesta, Bdozen ana kitengo chake pia ana brand yake, so ni boss. Mumybaby ana project yake, dadahood, kimsingi ana jambo lake Kuna movement inaonekana! Kennedy the remedy personality yake inaonekana ana focus ametulia sio kihuni kama baba la baba Adam Mchomvu! Adam usela mavi mwingi, Hadi Leo anavalia suruali kwenye makalio nani ampe kitengo, Hadi Leo anaongea kihuni huni utafikiri yupo kwenye balehe! Ila kwa kuwa ni life lake, fresh asiingie tu kwenye mihadarati!
 
Tujue elimu yake kwanza maana inaweza changia kutokukuwa maan an mwenzake fetty ameshapanda cheo sasa hivi ni mtayarishaji wa maudhui hapo kwao soon anaondoka kwa kipaza
 
Mkuu kwa hiyo ulitaka akatangaze taarifa za habari Ili uone kakua?Ukuaji wa mtu upo akilini mwake Nashangaa Kuna watu wananiambia skuizi nimekua niache bangi nawashangaa iliandikwa wapi ndumu wavute watoto?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom