Kumbuka wimbo wa Wagosi wa Kaya - Nyeti
Kuna beti moja jamaa waliimba hivi
"
...
Kuna kitu kinaniuma saaaaana san sana sana sana
Usipende kunyanyasa mwenzio mkiwa ofisini
Siku ya siku na wewe unapigwa chini, haupo tena kazini
Na una shida halafu unaranda randa mtaani, eeh
Yule mwenzio uliyemtilia chonjo kazini, mnakutana mtaani
Utaanza vipi kwanza kumwangalia usoni
Mwenzio tartiibu anakatiza na baloon
..."
Hapa vijana tunapata fundisho kwamba mwajiri ni mwajiri tu, imagine hawa vijana wanavyolalamikiwa kwa matumizi mabaya ya lugha dhidi ya watangazaji na redio zingine, dhidi ya wasanii waliokuwa nje ya mfumo wa unyonyaji wa bosi wao etc.
Ninaamini watasimama na kusonga mbele zaidi, lakini ni fundisho.