Ada za shule hizi...

Ada za shule hizi...

mjomba wako keshapita hiyo level..sasa mwakani nataka aanze la kwanza...

hebu nifanyie mpoango dada yangu.

Kwenye website zao wameweka mawasiliano yao (namba za simu) ila kwa sasa nipo mbali na simu na wifi yako ana mchecheto kweli wa kufanya maamuzi soon!
 
Salaam wakuu,

Ninaomba msaada kwa wanaofahamu juu ya ada za shule hizi kwa elimu ya msingi (mtoto wa kuanza darasa la kwanza).

- Hazina International

- Feza Schools

- Ali Hassan Mwinyi Elite

- Sunray Primary.



Nimejaribu kupitia kwenye tovuti zao sijapata chochote zaidi ya links ambazo hazina chochote. Nimesikitika lakini ni hivyo hivyo kwenye karibu kila sekta nchini kwetu, uwazi wa mambo ni kama dhambi.

Anyway, nisilalamike sana naamini hapa nitapata wadau watakaoweza kunisaidia hilo na lolote la ziada juu ya shule hizo au mojawapo ya shule hizo.

Natanguliza shukrani.
Feza schools ada milioni 7
 
Rule ya biashara do not let competitors know your costs and prices sababu kwa kufanya hivo competitor anaweza kupunguza bei za huduma/bidhaa zake ili wateja waje kwake.Hiyo ndio reason ya kutoweka gharama zao wazi ukitaka hizo information nenda sehemu husika
International school of Tanganyika, ISM, Heaven of piece ....shule ambazo ni kweli international websites zao wanaweka bei....hizi international zetu local za kulazimisha zinaogopa nini kuweka bei
 
Write your reply...shule bora si elimu bora kwa mwanafunzi bali ni mwanafunzi bora kwa shule bora uwezo wake mtazame usije jutia my bro!
 
Holla, sina taarifa zozote kuhusu hizo shule ulizotaja kwa ombi unalotaka. Ila kwa shule ya Hazina nafahamu kuna watoto wa ndugu na jamaa wamemaliza pale. Ada kwa mwaka kwa shule ya msingi inafikia milioni 3 (darasa la kwanza) na inaongezeka kila mtoto anapopanda darasa.

Wao wanazingatia zaidi masomo na ufahamu wa mtoto akimaliza darasa la saba hapo ataweza kufanya interview shule yoyote na atapita bila wasiwasi. Ndivyo ilivyotokea kwa watoto wa hao jamaa zangu. Sasa hivi wako sekondari Feza Sec.

Ila hawa hazina naona hawajatilia mkazo sana kwenye watoto kuzungumza kiingereza kwa uhuru kama shule hizo nyingine.

Ila pia kuna shule inaitwa Kwanza unit iko mikocheni. Ada yao ni makadirio ya Tsh. Milioni 3 na mtoto anakuwa vyema kwenye kuzungumza lugha ya kiingereza kiufasaha anajiamini kuliko mwanasiasa yeyote ila kiswahili atapata tabu sana kukisoma kukizungumza hata kufanya mtihani wa kiswahili hadi umtafsirie kwa kiingereza ndo ataweza kuelewa.

Kila la kheri.
Hahaha....Eti anajiamini kuliko akina nani?
 
Back
Top Bottom