Ada za shule hizi...

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,357
2,000
Salaam wakuu,

Ninaomba msaada kwa wanaofahamu juu ya ada za shule hizi kwa elimu ya msingi (mtoto wa kuanza darasa la kwanza).

- Hazina International

- Feza Schools

- Ali Hassan Mwinyi Elite

- Sunray Primary.Nimejaribu kupitia kwenye tovuti zao sijapata chochote zaidi ya links ambazo hazina chochote. Nimesikitika lakini ni hivyo hivyo kwenye karibu kila sekta nchini kwetu, uwazi wa mambo ni kama dhambi.

Anyway, nisilalamike sana naamini hapa nitapata wadau watakaoweza kunisaidia hilo na lolote la ziada juu ya shule hizo au mojawapo ya shule hizo.

Natanguliza shukrani.
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,357
2,000
nayo jua ni feza boys 4.5milion kwa nursery school
mjomba wako keshapita hiyo level..sasa mwakani nataka aanze la kwanza...

hebu nifanyie mpoango dada yangu.

Kwenye website zao wameweka mawasiliano yao (namba za simu) ila kwa sasa nipo mbali na simu na wifi yako ana mchecheto kweli wa kufanya maamuzi soon!
 
miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,899
2,000
mjomba wako keshapita hiyo level..sasa mwakani nataka aanze la kwanza...

hebu nifanyie mpoango dada yangu.

Kwenye website zao wameweka mawasiliano yao (namba za simu) ila kwa sasa nipo mbali na simu na wifi yako ana mchecheto kweli wa kufanya maamuzi soon!
labda nikupe namba ya mwalimu mmoja wa nursery umpe wifi yangu afanye mchakato sipo kwenye position ya kufuatilia kaka yangu
 
scooman

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
2,725
2,000
Salaam wakuu,

Ninaomba msaada kwa wanaofahamu juu ya ada za shule hizi kwa elimu ya msingi (mtoto wa kuanza darasa la kwanza).

- Hazina International

- Feza Schools

- Ali Hassan Mwinyi Elite

- Sunray Primary.Nimejaribu kupitia kwenye tovuti zao sijapata chochote zaidi ya links ambazo hazina chochote. Nimesikitika lakini ni hivyo hivyo kwenye karibu kila sekta nchini kwetu, uwazi wa mambo ni kama dhambi.

Anyway, nisilalamike sana naamini hapa nitapata wadau watakaoweza kunisaidia hilo na lolote la ziada juu ya shule hizo au mojawapo ya shule hizo.

Natanguliza shukrani.
Rule ya biashara do not let competitors know your costs and prices sababu kwa kufanya hivo competitor anaweza kupunguza bei za huduma/bidhaa zake ili wateja waje kwake.Hiyo ndio reason ya kutoweka gharama zao wazi ukitaka hizo information nenda sehemu husika
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,357
2,000
Rule ya biashara do not let competitors know your costs and prices sababu kwa kufanya hivo competitor anaweza kupunguza bei za huduma/bidhaa zake ili wateja waje kwake.Hiyo ndio reason ya kutoweka gharama zao wazi ukitaka hizo information nenda sehemu husika
Kwa dunia ya sasa sidhani kama hii rule ina apply au hata kama hii rule ni ipo kwenye biashara/uchumi in general.

Tutumie mfano wa bidhaa nyingine kama sabuni. Umeshawahi kusikia mtu anasema, "nunua sabuni yetu kwa kuwa ni bei rahisi kuliko ile nyingine?"

Pamoja na kwamba bei ya bidhaa inaweza kuchangia kununuliwa kwake lakini sio factor kubwa katika kununuliwa kwake. Hii haiwezi kuwa kisingizio cha kutokuweka wazi ada na gharama za shule. Ninachohisi mimi ni kwa kuwa ada na gharama hizi hazina market value reality (extortion in the name of education) ndiyo maana haziwekwi public.

Lakini sababu nyingine kubwa zaidi naamini ni kuiga mfano wa serikali. Ingia kwenye tovuti za wizara na idara mbalimbali za serikali uone ni mambo gani wameyaweka huko. Suala la uwazi kwa nchi yetu ni tupo nyuma sana kwa kweli tusitumia huo ushindani kama kisingizio.
 
Heaven Sent

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
20,968
2,000
Shukrani mkuu...niitie tu wote wadau wa elimu. Kukuza kazi kweli kweli jamani sasa mama mtoto anasema mtoto hawezi kupelekwa Bunge primary eti..dah!

espy, Heaven Sent, Heaven on Earth gfsonwin mkuje mnisaidie tafadhali...
Eeh bora wifi kaamua kuwekeza kwenye elimu kuliko kwenye kitchen party lol.

Ikishindikana kupata hizo costs humu, itabidi tu mtumie mawasiliano yao
 
Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
16,520
2,000
Holla, sina taarifa zozote kuhusu hizo shule ulizotaja kwa ombi unalotaka. Ila kwa shule ya Hazina nafahamu kuna watoto wa ndugu na jamaa wamemaliza pale. Ada kwa mwaka kwa shule ya msingi inafikia milioni 3 (darasa la kwanza) na inaongezeka kila mtoto anapopanda darasa.

Wao wanazingatia zaidi masomo na ufahamu wa mtoto akimaliza darasa la saba hapo ataweza kufanya interview shule yoyote na atapita bila wasiwasi. Ndivyo ilivyotokea kwa watoto wa hao jamaa zangu. Sasa hivi wako sekondari Feza Sec.

Ila hawa hazina naona hawajatilia mkazo sana kwenye watoto kuzungumza kiingereza kwa uhuru kama shule hizo nyingine.

Ila pia kuna shule inaitwa Kwanza unit iko mikocheni. Ada yao ni makadirio ya Tsh. Milioni 3 na mtoto anakuwa vyema kwenye kuzungumza lugha ya kiingereza kiufasaha anajiamini kuliko mwanasiasa yeyote ila kiswahili atapata tabu sana kukisoma kukizungumza hata kufanya mtihani wa kiswahili hadi umtafsirie kwa kiingereza ndo ataweza kuelewa.

Kila la kheri.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom