Ada ya leseni ya kumiliki silaha ya moto iangaliwe

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,558
2,854
Silaha sio chombo cha Starehe/kuburudisha kinasaidia kufanya kazi ya Ulinzi na hivyo kupunguza majukumu ya Askari wetu.

Kwaajili ya kutafuta Mapato Serikali ya awamu ya tano ilipandisha ada hii toka elfu 10,000 kwa mwaka mpaka elfu 75,000. Naamini hilo ongezeko halikuzingatia mawazo ya wadau.

Kuna Mwaka jirani yangu alivamiwa, tuliweza okoa mali zake kwa kusaidiana naye kwakuwa tulikuwa na silaha. Wale vibaka walikimbia. Silaha zinasaidia kwa kuwadhibiti vibaka wadogo.

Naomba Serikali kwakuwa inatatua kero za watu,wapitie hapa warekebishe, wote tunajenga nchi yetu.

Ahsante

Pia soma > Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania
 
Pia Watu waliovuka miaka 70 wasichukuliwe SIRAHA zao! Umri urekebishwe, labda kama mtu ni Mgonjwa wa Akili.Nimeshuhudia mtu anaenda kulipia kufika polisi, SIRAHA inachukuliwa kwakuwa ana miaka 70. Sheria mbaya.Oneni Rais wetu mstaafu ana miaka zaidi ya 90 ana nguvu na akili. Bado anaweza kumiliki SIRAHA katika umri ule
 
Mchakato ni Urasimu Mkubwa kwakuwa tunasaidia kazi ya Ulinzi waliangalie,ila isiwe kama Marekani, unanunua kama njugu.Kiwango cha Leseni kinakatisha tamaa kulipa,baada ya miaka kadhaa inakuwa kama unanunua SIRAHA upya kwa gharama za Leseni utakazokuwa umelipa
 
Wajinga kama kina 7ya ukisia yupo nje unaziwasha kwenye roof kama tatu.
 
  • Kicheko
Reactions: rr3
Hayo mambo ya SIRAHA achana nayo.huenda wewe labda unbiashara kubwa ambazo unaona kuna umuhimu wa kumiliki siraha.LKN marekani sasa hivi inaumiza kichwa jinsi ya kudhibiti umilikaji wa siraha.kama kodi ilipanda ilikuwa kwa nia nzuri tu kwa maana ya udhibiti.

Angalia marekani na nchi nyingine jinsi siraha zinavyotumika bila kuzingatia masharti waliopewa hao wamiliki.ss tz silaha za nn wakati tunalindwa vzr tu na askari wetu.tuongelee maswala mapana yenye mustakabali wa nchi yetu.
 
Hayo mambo ya SIRAHA achana nayo.huenda wewe labda unbiashara kubwa ambazo unaona kuna umuhimu wa kumiliki siraha.LKN marekani sasa hivi inaumiza kichwa jinsi ya kudhibiti umilikaji wa siraha.kama kodi ilipanda ilikuwa kwa nia nzuri tu kwa maana ya udhibiti.angalia marekani na nchi nyingine jinsi siraha zinavyotumika bila kuzingatia masharti waliopewa hao wamiliki.ss tz silaha za nn wakati tunalindwa vzr tu na askari wetu.tuongelee maswala mapana yenye mustakabali wa nchi yetu.
Mkuu usiangalie kwa hicho la namba hiyo. Hata hivyo kwa RAIA mmoja mmoja kulipia 75,000 kwa ajili ya silaha sio shida sana kwakua mara nyingi watu hao wanakua na uwezo

Ila fikiria kwa watu wa fursa kwenye kampuni binafsi za ulinzi. Ukiwa na gobore 10 tu manaake unapaswa kulipa 750,000 wizara ya mambo mengine. Bado vibali vingine,gharama za uendeshaji. Matokeo yake utalipa walinzi mshahara wa laki na nusu wanabakia kuwa omba omba huko kwa wateja na kufanya kazi za kuosha magari
 
Una hoja ya msingi lakini umeongeza chumvi.

Ada ya leseni ya pistol ilipanda toka 35000 hadi 70000 na siyo kutoka 10000 hadi 75000 hivyo hakuna Silaha inayolipiwa 75000 na Mtanzania.

Silaha rifle na shotgun zilipanda toka 15000 hadi 35000.

Endelea na maelezo yako sasa.
 
Mkuu usiangalie kwa hicho la namba hiyo. Hata hivyo kwa RAIA mmoja mmoja kulipia 75,000 kwa ajili ya silaha sio shida sana kwakua mara nyingi watu hao wanakua na uwezo...
kwa tahmini yangu kwa nchi hii hizo kampuni za ulinzi ndizo zinazoongoza kwa kuwanyonya watumishi wao.Kampuni inalipa laki tatu na nusu kwa kampuni au zaidi lkn walinzi wanalipwa laki moja na nusu na cjui wameambizana karibu kila mkoa ukienda malipo yanafanana, haya mambo ndo hatuyataki.

Ili kodi na ushuru vipungue basi hayo makampuni nayo basi yawe considerate kwa walinzi wao.
 
Pia Watu waliovuka miaka 70 wasichukuliwe SIRAHA zao! Umri urekebishwe, labda kama mtu ni Mgonjwa wa Akili.Nimeshuhudia mtu anaenda kulipia kufika polisi, SIRAHA inachukuliwa kwakuwa ana miaka 70. Sheria mbaya.Oneni Rais wetu mstaafu ana miaka zaidi ya 90 ana nguvu na akili. Bado anaweza kumiliki SIRAHA katika umri ule
Hilo la age limit ni uhuni wa Polisi, sheria haisemi hivyo na haina limit ya umri.
 
kila mtu akimiliki si yatakuwa majanga , nadhani ile kamati inayokaa kuchambua maombi ya mwombaji iongeze umakini
 
kwa tahmini yangu kwa nchi hii hizo kampuni za ulinzi ndizo zinazoongoza kwa kuwanyonya watumishi wao.Kampuni inalipa laki tatu na nusu kwa kampuni au zaidi lkn walinzi wanalipwa laki moja na nusu na cjui wameambizana karibu kila mkoa ukienda malipo yanafanana,haya mambo ndo hatuyataki.Ili kodi na ushuru vipungue basi hayo makampuni nayo basi yawe considerate kwa walinzi wao.
Ndio kuna gharama za uendeshaji sasa ndugu yangu. Sisemi inapaswa walipwe laki na nusu ila kuna gharama nyingi me mmiliki anazoingia ndo maana inakua hivyo
 
Unatumia silaha ya moto kudhibiti kibaka? Acha utani mkuu. Mbona hiyo force unayotumia ni kubwa sana angalia itaweza kuku-cost siku moja.

Silaha ya moto ni kuzibiti majambazi sio vibaka
 
Ilo Ni kweli

Ilo pia serikali iondoe urasimu kwny mchakato mzima wa kupata silaha.

Unajikuta unazungumzia korido kibao na makabrasha,

Hali inayochochea vitendo vya rushwa.
Bora waendelee na ukiritimba manake wengine tuna hasira za karibu
 
Hayo mambo ya SIRAHA achana nayo.huenda wewe labda unbiashara kubwa ambazo unaona kuna umuhimu wa kumiliki siraha.LKN marekani sasa hivi inaumiza kichwa jinsi ya kudhibiti umilikaji wa siraha.kama kodi ilipanda ilikuwa kwa nia nzuri tu kwa maana ya udhibiti.

Angalia marekani na nchi nyingine jinsi siraha zinavyotumika bila kuzingatia masharti waliopewa hao wamiliki.ss tz silaha za nn wakati tunalindwa vzr tu na askari wetu.tuongelee maswala mapana yenye mustakabali wa nchi yetu.
 
Nimeshangaau uliposema silaha inasaidia kuwadhibiti vibaka wadogo wakati silaha matumizi yake ni mapana kuliko kuwadhibiti vibaka wadogo.Japo hilo la kuwadhibiti vibaka wadogo ni moja ya jukumu la silaha.siamini kama unaweza kumiliki Silaha ukashindwa kutoa75,000
 
Unatumia silaha ya moto kudhibiti kibaka? Acha utani mkuu. Mbona hiyo force unayotumia ni kubwa sana angalia itaweza kuku-cost siku moja.

Silaha ya moto ni kuzibiti majambazi sio vibaka
Kibaka nae ni mhalifu kama wahalifu wengine. Mind that moja ya sababu mtu huomba kibali cha kumiliki silaha ni kujilinda dhidi ya uhalifu wowote (vibaka, majambazi, wezi n.k).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom