Ada ya kutumia WhatsApp yaondolewa

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Wamiliki wa app ya mawasiliano ya WhatsApp wamefuta ada ambayo watumizi wake wamekuwa wakitakiwa kulipa kila baada ya mwaka mmoja.

Wamiliki wa huduma hiyo wamekuwa wakiwatoza watu $0.99 kila mwaka baada ya kuitumia kwa mwaka mmoja.

Ada hiyo ilianza kutozwa miaka michache iliyopita lakini kampuni hiyo inasema haijakuwa na manufaa sana.

Taarifa kutoka kwa wamiliki wa WhatsApp inasema: “Watu wengi wanaotumia WhatsApp hawana kadi za benki na wengine huwa na wasiwasi kwamba baada ya mwaka mmoja watazuiwa kuungana tena na marafiki na jamaa.”

“Kwa hivyo, wiki chache zijazo, tutaondoa ada zote tunazotoza wa wanaotumia aina mbalimbali za app yetu na hutatozwa tena pesa ili kutumia WhatsApp.”

Kwa sasa, WhatsApp, ambayo humilikiwa na Facebook, hutumiwa na watu bilioni moja na kampuni hiyo inatumai kuondolewa kwa ada kutavutia watu wengi zaidi.

Lakini bado wamesisitiza kwamba hawatakuwa wakiweka matangazo na badala yake watatafuta njia nyingine za kujipatia mapato.

Chanzo: Ada ya kutumia WhatsApp yaondolewa - BBC Swahili
 
Mh! Hz ofa nyingine ni hz....ngoja tuojionee
 
Whatsapp ilishachukuliwa na CIA kwa ajili ya Kazi Maalumu....hivyo wameona iwe Free tu kila mtu ajianike tu...ndio maana sasa hivi Whatsapp sio salama sana hasa kwenye Magroup kuna namba ukiiunga kwenye magroup inajibu maswali inajiita WIKI...
 
CIA wana matumizi pia na Facebook ndio maana Osama Bin Laden alikuwa hataki ujinga huo akaweza kukaa salama miaka yote hiyo bila kukamatwa na Marekani.
 
Back
Top Bottom