MILKYWAY GALAXY
JF-Expert Member
- Dec 12, 2008
- 204
- 89
Swali lako ni zuri, likijibiwa hilo tutapata mwanga
Kwa mtazamo wangu sidhani kama hili swala la karo elekezi linawezekana......kwani tution fee itakuwa ndogo.....ila ukiangalia gharama za maradhi na chakula sidhani kama hapo kunaweza kuwa na mjadala!!!!
Katika shule zilizo bora....mtoto anakula milo minne!! Anapata matunda,maziwa nk.....
Maradhi mtoto analala chumba kimoja watoto wawili.....bafu zuri na choo cha maji safi.......kwa mazingira kama haya ni bora kumuambia mwenye shule afunge shule afanye biashara nyingine........kinyume na hapo naamini haitawezekana.
Eti MAJARIBIO....
Majaribiooooo.... 😨😨😨💀👊👌
Watoe Amri tu, hakuna majaribio...!!
Priveta schools fees... eg
Ada kwa day... Max. 500,000
Boarding, Max... 1,500,000
Hakuna zaidi ya hapo... hakuna michango yoyote... shule itakayo changisha kufungiwa haraka sana
..
Serikali inafanya majaribio kwani ni ADA NI DAWA..? 😨😨
Hamna kitu hapo, kwanini iwe majaribio na kwanini iwe kwa baadhi ya shule?
.....nilichokiona kuna shule zina sauti kuliko serikali....
Hamna kitu hapo, kwanini iwe majaribio na kwanini iwe kwa baadhi ya shule?
.....nilichokiona kuna shule zina sauti kuliko serikali....
Watoto wanalishwa wali maharage daily,vitafunio andazi za mia mia na chai ya strungi halafu ada milioni 10
Hizi shule ni chache sana zinazo hudumia wanafunzi kwa gharama halisi za ada wanazotoza nasema hivyo kutokana kuwa nina wadogo zangu mmoja yupo shule moja arusha mwingine Dar lakini nikiwauliza wanachokula hakiendani na ada yenyewe unakuta ada 2,998,000 lakini wanakula hadi makande, hawa jamaa wanapata faida kubwa kupitia migongo ya Wazazi wenye uchu wa kuwapa watoto wao elimu bora, mapendekezo kungekuwapo wakaguzi pamoja na kukagua taaluma wakague na swala la wanafunzi kupewa lishe inayolingana na pesa za chakula wanazotoa.
Mkuu, mwanangu yupo st Joseph millennium pale goba juzi kati kanilalamikia sana kuwa anataka kuhama sbb msosi ni ndondo kwenda mbele yaani balaa. Nimekomaa kibaba baba tu kwamba nooo! Lknni kaja kugundua kuwa ile fees wazazi tukilipa haiendi straight shuleni kumbe akaunti ni ya dayosisi ya dsm so mpaka kamati ikae ndo hela iende shule. Ada ni mil 3.2 kwa mwaka. Hii haki kweli?
Hii 2.5 unapendekeza kwa ajili ya vyuo gani? Alafu ni kwa diploma, bachelor na kundelea au?Hakuna cha feza wala nani,wale wanaotoza zaid ya mil 3 warud 2.5,wakiona ngumu waende nchi nyngne,msimamo uwe hvo tuone