mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,410
- 4,988
Chama cha ACT Wazalendo kimemwandikia rasmi Msajili wa Vyama vya Siasa malalamiko dhidi ya Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amosi Makalla kutokana na matamshi yake ya madai kuwa CHADEMA kinaendesha harambee ya kununua virusi vya M-pox na Ebola kwa lengo la kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Katika barua rasmi ya tarehe 24 Machi 2025 iliyotumwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo Jambo TV tumepata kuiona, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, ameeleza kuwa kauli ya Makalla ni "ya kizembe, isiyo na msingi na inayoweza kuzua taharuki kwa jamii."
"Kauli hii haitakiwi kutafsiriwa kuwa ni hujuma dhidi ya CHADEMA pekee, bali ni kauli inayohujumu nchi kitaswira na kiuchumi," amesema Ado Shaibu katika barua hiyo.
Kwa mujibu wa ACT Wazalendo, kauli kama hiyo inaweza kuwa na athari kubwa kwa sekta ya utalii na uwekezaji nchini kwa kuwa inajenga hofu kuhusu usalama wa kiafya wa Tanzania kimataifa.
Katika maombi yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, ACT Wazalendo wanapendekeza Makalla ajieleze kuhusu kauli hiyo, kufuta kauli hiyo hadharani, kuomba radhi kwa umma na hatua nyingine za ziada zinazoweza kuchukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Pia soma

- Msajili wa vyama vya siasa, kama unaweza kum summon Mnyika kuhusu No reoforms No election, basi Amos utamsummon kwa m-pox na ebola saga
- CHADEMA wakiongozwa na John Mnyika waitikia wito wa kufika kwenye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
- Makalla: CHADEMA wanataka kuingiza Ebola Tanzania ili wazuie uchaguzi!