ACT-Wazalendo tangazeni sera za Chama chenu sio mtu

ACT-Wazalendo tangazeni sera za Chama chenu sio mtu

Mjadala dhidi ya Zitto umeshafungwa. Mlimfukuza wenyewe sasa mmebaki kulialia hapa JF.
 
Niamini ninachosema, ACT ipo kwa kazi maalum chini ya uongozi wa Kiongozi Mkuu mwenye mamlaka yote - itakufa baada ya uchaguzi mkuu baada ya kumaliza kazi yake ya kuzigawa kura za wapinzani.
 
Mjadala dhidi ya Zitto umeshafungwa. Mlimfukuza wenyewe sasa mmebaki kulialia hapa JF.

Lazima ajadiliwe kama wewe unavyomjadili slaa

Shetani lazima ajadiliwe na wafuasi wa Mungu

Huyu binadamu mlimtumia kukivunja chama chetu akiwa ndani...tukamshtukia...tukamtimua

Sasa mnamtumia ku confuse wananchi akiwa nje....na hapa pia hatutamuacha awachanganye wananchi
 
Niamini ninachosema, ACT ipo kwa kazi maalum chini ya uongozi wa Kiongozi Mkuu mwenye mamlaka yote - itakufa baada ya uchaguzi mkuu baada ya kumaliza kazi yake ya kuzigawa kura za wapinzani.

Huo ndio ukweli mkuu.

Jiulize Kitila ni nani? Amekuwa mkuu wa kitivo cha elimu chuo kikuu Dar tawi la chang'ombe kwa muda wote akiwa anafanya active politics na hajawahi kutimuliwa au kupewa onyo kazini...wakati sheria ya utumishi wa Umma hairuhusu....Jiulize yeye ni nani?

Jiulize hadi CHADEMA wanachukua maamuzi ya kuachana nae sio wamekurupuka...wanamfahamu vizuri sana...kumbuka wao ndio wamemfanya awe hivi alivyo......

Ukiangalia hata humu JF hakuna mfuasi wa CDM aliyegeuka na kumfuata...ni wale wa CCM ndio wanamshabikia pamoja na ID mpya zilifofunguliwa na watu wake.

Na kuna wengine ambao ni wafuasi wa watu kama Mkandara kiasi kwamba leo zito akifa na yeye ataomba azikwe naye kaburi moja
 
Last edited by a moderator:
Anachofanya Zitto leo kilifanywa miaka zaidi ya 10 iliyopita na chadema sasa huwezi kupimana ubavu na mtu anayejitangaza kwa kushindana na mtu ambaye hata mimi nikiandaa mkutano wenye jina la chadema mkutano unajaa kitu ambacho hata ccm hawakiwezi hata Nape Nnauye hawezi kuandaa mkutano ukahudhuriwa na watu timamu
 
Last edited by a moderator:
Niamini ninachosema, ACT ipo kwa kazi maalum chini ya uongozi wa Kiongozi Mkuu mwenye mamlaka yote - itakufa baada ya uchaguzi mkuu baada ya kumaliza kazi yake ya kuzigawa kura za wapinzani.
Kwani wapinzani kura zao ni ngapi mpaka zigawanywe na ACT??? Msimezeshwe kila kitu vingine sumu, unatakwimu za waliopiga kura 2010?? Unafahamu ni idadi gani ya watu hawana mihemuko na vyama vya siasa iwe UKIWA au sisiemu. ??? Hao ndio shabaha ya wazalendo.
 
Ukiwa mtu makini utagundua Zito ameacha siasa za kuleta Ukombozi unaoambatana na Mabadiliko ya kweli yenye kuleta mrejesho na matokeo halisi kwa WANANCHI.

Badala yake tuonaona Zito amebakia kuendesha siasa za:-

-Kujijenga na zenye kumpa UMAARUFU yeye mwenyewe.

-Hana kusudio la kukibomboa au kukiathiri chama tawala (CCM) ila amedhamiria kwa dhati kabisa Kuubomoa Upinzani shabaha yake kuu hasa ni CHADEMA.

Inatia aibu,SHUJAA kugeuka kuwa KIBARAKA,kilichobakia ni kumhurumia tu Zito maana safari yake ya kisiasa inamtatanisha,alikofikia hajui ATOKAKO,ALIKO wala AENDAKO.

NAMHURUMIA ZITO KABWE maana Mwisho wa yoote atavuna fedheha.
Hata YESU alikuwa analiliwa hivyo, lakini akawaambia watu, msinililie mimi, jililieni ninyi wenye dhambi. Kijana ZITTO haupaswi kumhurumia, jihurumie wewe ambaye umefanywa zezeta na akina MBOWE.
 
Kwani wapinzani kura zao ni ngapi mpaka zigawanywe na ACT??? Msimezeshwe kila kitu vingine sumu, unatakwimu za waliopiga kura 2010?? Unafahamu ni idadi gani ya watu hawana mihemuko na vyama vya siasa iwe UKIWA au sisiemu. ??? Hao ndio shabaha ya wazalendo.
wewe jifanye hamnazo, lakini ukweli ndiyo huo.
 
Mjadala dhidi ya Zitto umeshafungwa. Mlimfukuza wenyewe sasa mmebaki kulialia hapa JF.
Simmesha muoa nyinyi CCM, mwali wenu bado mbichi, endeleeni kujipigia tu. Ila kumbukeni hamtaweza kuzuia mafuriko kwa mikono!
 
Kuna kosa moja la kimkakati na kiuelewa wanalifanya hawa watu mbali ya kutomjua adui yao na kupambana na CHADEMA nalo ni kufanya siasa za mtu badala ya sera za Chama.

Kutwa nzima wamejaa humu kumpromote na kumtetea Zitto badala ya kutangaza Sera za chama.

Ni hatari sana kwa chama kuwekeza kwa mtu kwasababu hamna Mkataba na Mungu.Hivi ikitokea Mungu akamchukua Zitto ndiyo mwisho wa ACT-Wazalendo?
chama kinachojengwa na mtu mmoja hicho nacho ni chama kweli - mikakati afanye yeye, hela atafute yeye, mikutano aandae yeye na kuhutubia yeye; anachofikiri kuhusu chama ndiyo hicho hicho kinafanyika, sasa siku akipata malaria akashindwa kupanda jukwaani na chama kinaugua pamoja naye!!
 
Mwenyenazo twende kazi......here we gooo, shusha takwimu na sio kuhemukwa
tuanze na hili la kwanza. Je ni kina nani wafadhili wenu, wapi mmepata mapesa mengi hivyo -mmeshatumia zaidi ya billion moja - mmezipata wapi?

Chama cha Kizalendo haya tangazieni umma source ya pesa zenu.
 
Sina kadi ya chama chochote, navutiwa na siasa za kizalendo kama nilivowahi kuvutiwa na siasa za vyama vingine vya upinzani. Muulize Mbowe, mzee mtei na dr slaa wakati chama kinaanza kujengwa walitoa wapi pesa?? Inasemekana walipokuwa wanatoa ndio wazalendo wanatoa hukohuko.
 
Back
Top Bottom