Magufuli alikuwa muislam?kujificha kwenye kivuli cha udini badala ya kujibu hoja ni udhaifu
Wakristo Siku ZOTE wamekua wakipinga na Kupigia Kelele udhaifu Wa Viongozi.
Nyerere Alitaka mpaka kupinduliwa . Hapakua na sababu za kidini Bali maisha magumu na ukosefu Wa ajira .
Mkapa alipingwa sana na Lisu ,Mtikila , Mrema n.k bila kujali Dini yake .
Magufuli alipingwa zaidí na Wakristo hasa Maaskofu na Wanaharakati Japo alikua anakubalika kutokana na kuwashughulikia majipu na majizi Kwa haraka na Kufunga Akaunti Zao. Na pia kuzuia mikataba ya kinyonyaji . Lakini pia JPM alikua na Uzalendo Kwa nchi yake na watu wake kuliko kuwa Kibaraka Wa Wazungu na Waarabu .JPM alikataa kuruhusu watanzania kuhujumiwa na wahuni waliotaka kuleta mambo ya ushoga ,wizi kupitia mikataba ,rushwa ya kuficha fedha Dubai na Uswis na Afrika kusini.
Wananchi wanyonge waliona Uzalendo Wa JPM kwenye kupigania Mali za Watanzania.
Lakini alipingwa kwenye Suala la Demokrasia na utawala Wa Sheria Japo wavunja Sheria wakati mwingine wanatumia mwanya huo huo KUFANYA uhalifu.
Tofauti na Utawala Wa Awamu hii ni kufumbia macho mawaziri ,wakurugenzi na makatibu wanaotumia vibaya fedha za umma kujinufaisha na kukwamisha miradi ya Serikali huku Wananchi WAKIWA wanakamuliwa Kwa Kodi na Tozo wao wanastarehe na kujilimbikizia Mali kupitia ofisi za umma .
JPM alipingwa sana .Hata walioshangilia sana kifo chake WENGI ni wale Wa Dini yake yaani wakristo.
Kwa hiyo ni upuuzi mkubwa kusema kuwa Rais Samia anakosolewa na Kupingwa Kwa sababu ni muislam.
Kwa Maana nyingine tuseme kwamba uwekezaji Sasa unaletwa Kwa misingi ya kidini ndio Maana wanaingia mikataba ya kihuni .
Sasa tumeshagundua mapema na tumeamua kukataa uhuni huo.
Kwanza wazungu hawana Tena mambo ya Ukristo Wala Dini zaidi ya teknolojia na uchumi . Hivyo kusema kuwa Wazungu wanapowekeza wanawekeza Kwa sababu ya Dini ni upuuzi.
Hata Dubai ya miaka hii haipo Kwa sababu ya kupigania Dini . Pale Dubai ni mabilionea wanaangalia namna ya kushika uchumi Wa Dunia SIO Dini.
Watanganyika tuamke tuachane na propaganda za Wana CCM uchwara wanaoona kuwa 2025 ni mwisho Wa Wezi na familia zao kukalia ofisi za umma.