Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,619
Kwenye sakata la TPA vs DP World, Zitto Kabwe amechagua kuwa Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ambaye hakupenda asilani mapinduzi matukufu.
Huenda Prof. Lipumba naye kwa kimya chake anatafakari kuungana naye.
Aliisaliti nchi kwenye Tume ya Madini, alinuka rushwa kwenye PAC akiwa M'kiti wake akitisha/akishinikiza Bodi na Menejimenti za Mashirika ya Umma kumpa bahasha, ameisaliti Tanganyika (Tz Bara) kwenye sakata la TPA na DP World kwa kutounganisha nguvu na wenzie.
Huenda naye tunapata mashaka alienda Burji Khalifa kwa wakati wake kuchukuwa chake.
Ila nguvu ya uuma wenye uzalendo (umma ulioweka kando tofauti zao na kuamua kuungana pamoja kuokoa hatima na mustakabali wao) umemthibitishia kuwa mlungula aliopokea Burji Khalifa kumbe ni kitanzi chake tu na kwamba kuchagua kwake kuwa kinyume na umma huo kunamporomosha kisiasa na kutamfungia milango ya fursa za kisiasa Tanganyika.
Safari hii tutachagua chama kulingana na msimamo kilichochukuwa kwenye sakata la bandari na rasilimali za Tanganyika (Tz Bara).
Wapinzani wa kweli safari hii acheni kugombea urais (muiachie CCM urais) tafuteni kwa udi, uvumba na manemane kuingia Bungeni kuiokoa nchi.
Wapinzani hamuwezi kuishinda CCM kwenye nafasi ya urais hata mkiungana wote kwa sababu nafasi ya urais haitegemei kura za kwenye masanduku, rais haingizwi ikulu na kura anaingizwa na dola.
Kumshinda rais kwenye uchaguzi ni ndoto ila ni rahisi kumuondoa kupitia Bunge. Mwacheni ashindaye ashinde ila kamsubirini Bungeni.
Zitto, 2024 na 2025 zinabisha hodi. Jitathmini mapema kama wewe ni Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe au Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (Zaim).
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app