PostGE2025 ACT Wazalendo: Mahakama kuu imetoa kibali kesi ya kupinga uteuzi wabunge Viti Maalum uliofanywa na INEC

PostGE2025 ACT Wazalendo: Mahakama kuu imetoa kibali kesi ya kupinga uteuzi wabunge Viti Maalum uliofanywa na INEC

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Leo tarehe 30 Disemba, 2025 Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu Dodoma ikiketi chini ya Jaji Ephery Kisanya imetoa uamuzi wa muhimu katika kesi dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuhusu Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalumu iliyofunguliwa na ACT Wazalendo. Katika uamuzi huo mdogo, Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi la Serikali na kuagiza kesi iendelee katika hatua ya kesi ya msingi.

Hatua hiyo imekuja kufuatia maombi ya kimahakama (Application for Leave) yaliyowasilishwa na ACT Wazalendo tarehe 19 Novemba, 2025 kupitia shauri la Mahakama Kuu namba 28632 la mwaka 2025 kuomba kibali cha Mahakama Kuu kufungua kesi ya msingi ya kupinga Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalumu uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 7 Novemba, 2025 uteuzi ambao ulionekana kukiuka Katiba na kukosa misingi ya haki.

Awali, katika hatua ya shauri la Maombi ya Kibali cha kufungua kesi ya msingi, Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu iliweka mapingamizi ikidai kuwa Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi inayoombwa kufunguliwa na ACT Wazalendo. Mahakama katika uamuzi wake uliotolewa leo imeona kuwa mapingamizi hayo hayana msingi na imeyatupilia mbali na imetoa ruhusa kwa kesi ya msingi kufunguliwa na kusikilizwa.

Katika madai yetu, ACT Wazalendo tunapinga utaratibu uliotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalumu kwani kwa maoni yetu tunaona kuwa Tume imevunja vifungu vya Katiba na Sheria ya Uchaguzi. Vilevile, tunataka Tume ya Uchaguzi ikaeleze Mahakama ilitumia utaratibu gani kupata idadi ya Viti Maalumu vya Ubunge ilivyovitoa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliopata viti 113 na CHAUMMA waliopata viti 2 ilhali fomula ya idadi ya viti kwa kila chama kinachostahiki inayopatikana chini ya sharti la Ibara ya 78(1) ni viti visivyopungua 6.

Aidha, tunakusudia kuomba Mahakama iitake Tume kueleza ni matokeo yapi ya Uchaguzi wa Ubunge waliyotumia kukokotoa idadi ya Viti vilivyostahiki kwa kila chama kilichoshiriki Uchaguzi kwani kwa mujibu wa Matokeo tuliyokusanya, ACT Wazalendo tuna kura 2,222,162 ambazo ni sawa na 6.77% ya kura za Ubunge.

Baada ya uamuzi huu wa Mahakama, sasa kesi ya msingi kwa ajili ya kuhoji masuala hayo na mengineyo iko wazi kufunguliwa. Tayari Mawakili wa Chama wamekamilisha hatua zote za kufunguliwa kwa kesi hiyo.

Pia Soma: Sakata la wabunge wa viti maalumu, ACT Wazalendo yatinga mahakamani
1767096892963.png
 
Hamna kitu hapo, kugungua is a simple thing. Sasa kazi ni hapo kuwaengua! Kufuta kuteuliwa kwao!
Sawa na ioe ya kuoinga upuuzi wa ile Tume, wamekubaki kufungau kesi lkn eti tume inaendelea na kazi yake! Rubbish!
 
Hii ni nafasi ya kuongeza wabunge kutoka vyama vya upinzani ili bunge lipate uhalali. Act wakipata 6 pamoja na wale wa Pemba watakuwa chama kikuu cha upinzani na Chaumma wakipewa viti vingine vinne, kambi ya upinzani itakuwa angalau angalau.

Amandla...
 
Itasaidia nini?
 
Uhalili wa bunge hauaji kutokana na idadi ya wabunge kutoka chama fulani bali ridhaa ya raia wengi na kuzingatiwa kwa mchakato wa kikatiba unaoutumika kuwapata hao wabunge wenyewe.
 
Uhalili wa bunge hauaji kutokana na idadi ya wabunge kutoka chama fulani bali ridhaa ya raia wengi na kuzingatiwa kwa mchakato wa kikatiba unaoutumika kuwapata hao wabunge wenyewe.
Hilo unalijua wewe. Uhalali wa Bunge lililopita ulitokana na Covid 19. Wakipatikana wabunge kama 25 kutoka upinzani utawapa uwezo wa kudai bunge lililopo linawakilisha raia wakazi wa Tanzania.

Halitakuwa linawakailisha Tanzania kwa sababu ushindi wa CCM ni 98% sasa hilo bunge lenye wabunge 25 litapatikana wapi kama sio la kuchonga
 
Halitakuwa linawakailisha Tanzania kwa sababu ushindi wa CCM ni 98% sasa hilo bunge lenye wabunge 25 litapatikana wapi kama sio la kuchonga
Hilo unajua wewe. Mbona hata wakati wa Mwendazake hali ilikuwa hivi hivi. Sasa hivi kuna wabunge wa saba wa upinzani wa kuchaguliwa. ACT-WAZALENDO sita na Chaumma mmoja. Chaumma wakapewa wawili wa kuchaguliwa na hivyo kuwapa wabunge watatu. Ikiwa kutokana na kesi ya ACT-WAZALENDO, ACT Wazalendo watapewa wabunge 6 wa viti maalum na Chaumma wataongezewa wanne ili watimie sita basi jumla ya wabunge wa upinzani watakuwa 19, ambayo haitoshi kuwa na kambi rasmi ya upinzani.

Amandla...
 
Hii ni nafasi ya kuongeza wabunge kutoka vyama vya upinzani ili bunge lipate uhalali. Act wakipata 6 pamoja na wale wa Pemba watakuwa chama kikuu cha upinzani na Chaumma wakipewa viti vingine vinne, kambi ya upinzani itakuwa angalau angalau.

Amandla...
ACT wanataka viti vya CHAUMMA sio kwamba viti maalum vitaongezwa!! Kama cut off ni 5% Je Chaumma wamefikishaje ilihali hawajapata 5% ya kura za ubunge?

Nadhani Tanzania tunatumia bado D'hondt method of proportion kugawa nafasi za viti maalum, mfano CCM ina zaidi ya 98% ya kura za ubunge meaning inatoa 98% ya viti vya viti maalum. Sasa hivyo viti 6 sijui vya chaumma au ACT vinatoka wapi na tayari kisheria CCM ana above 98%?
 
ACT Wazalendo watapewa wabunge 6 wa viti maalum na Chaumma wataongezewa wanne ili watimie sita basi jumla ya wabunge wa upinzani watakuwa 19, ambayo haitoshi kuwa na kambi rasmi ya upinzani.
Viti 6 vinatoka wapi? Kwani ACT imefikisha 5% ya kura za wabunge? Hivi unajua kura zote za wabunge wa ACT Zanzibar ni sawa na za mgombea wa CCM jimbo la Kawe?

Unaleta speculations wakati kesi haijakaa hivyo. CCM haina aibu kuwa wenyewe, hata CUF walisusia uchaguzi mkuu 2016 na CCM ikachukua bunge zima!! sembuse sasa?
 
Back
Top Bottom