PreGE2025 ACT-Wazalendo: Hatukubaliani na CHADEMA katika ajenda ya ‘No Reform, No Election’

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mfumo wa vyama vingi wa mwaka 92' umewekwa ili kuwafanya Ccm iendelee kuwa madarakani.
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ambaye ni Mtia nia nafasi ya Urais katika Uchaguzi wa Oktoba mwaka huu Dorothy Semu anasema kuwa wao hawakubaliani na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika ajenda ya ‘No Reform, No Election’.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sawa. Lakini wao wana mbinu gani mbadala. Kama wataingia kwenye uchaguxi kwa hali hii wategemee yale yale ya 2019, 2020 na 2024.
 
Huyo mwakani ni mkuu wa mkoa kama mama mgwira na queen sendiga..
Sasa no reform, no election ataielewa vipi?!
 
..ukitaka kujua msimamo wa ACT msikilize Othman Masoud achana na Dorothy Semu.
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ambaye ni Mtia nia nafasi ya Urais katika Uchaguzi wa Oktoba mwaka huu Dorothy Semu anasema kuwa wao hawakubaliani na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika ajenda ya ‘No Reform, No Election’.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ila anachokiongea hakina tofauti sana na Chadema. Chadema na ACT wakubaliane kitu kimoja.
 
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ambaye ni Mtia nia nafasi ya Urais katika Uchaguzi wa Oktoba mwaka huu Dorothy Semu anasema kuwa wao hawakubaliani na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika ajenda ya ‘No Reform, No Election’.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Basi mkubaliane na ccm no katiba mpya
 
Kama upinzani wenyewe hawaeleweki ww unadhani nn kifanyike?
Kweli asee. Ila ni hivo tu wadau kutaka maslahi binafsi.. kingetengenezwa chama kimoja tu Cha opposition alafu tuone Kama Hawa mbuzi wataonja Tena mema ya nchi.
 
..ukisikiliza maelezo yake utaona kwamba wanaunga mkono Chadema.

..kwa mfano, anasema mabadiliko yaliyofanyika ni hadaa, wanataka mabadiliko ya kweli.
Hilo hata NCCR Mageuzi wanasema. Pamoja na ukweli huo ( wanaujua zaidi kwa sababu wamekuwa wakishiriki chaguzi zote baada ya 2020. Nadhani walipata ushindi mmoja tu Zanzibar kwa mbinde). Wanakataa strategy ya No Reform No Elections.

Amandla..
 
Ndio maana ya kuwa na vyama vingi kila chama kinakuwa na mawazo yake na mwekekeo wake

Haiwezekani wote wakawaza kama Chadema

Vinginevyo kusingekuwa na kuwa na vyama vingi

Ns Chadema sio head prefect wa kuwaamulia vyama vingine wawaze vipi

After all ukienda kuangalia kiundani ACT WAZALENDO ni chama kikubwa kuliko Chadema sababu kimetoa makamu wa Raisi wa Zanzibar

Chadema ilitakiwa wawasikilize ACT wazalendo kujua nini siri yao ya mafanikio sio ACT Wazalendo iwasikilize Chadema

Huyo mama yuko sahihi.Kama Act wazalendo imefanikiwa kutoa makamu wa Raisi ina maana nyota yao kubwa na inang'ara kuliko maruhuni wa Chadema
 
Hilo hata NCCR Mageuzi wanasema. Pamoja na ukweli huo ( wanaujua zaidi kwa sababu wamekuwa wakishiriki chaguzi zote baada ya 2020. Nadhani walipata ushindi mmoja tu Zanzibar kwa mbinde). Wanakataa strategy ya No Reform No Elections.

Amandla..

..Act wana "operation linda demokrasia."

..Chadema wana "No Reforms No election."

..wote wanasema watashawishi vyama vyenzao, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, na nchi marafiki.

..naamini wote wana MALENGO yanayofanana.
 
Kwangu mimi shida ya " No Reforms No Elections" ni ambiguity yake. Kwangu mimi hawajajieleza vizuri ina maana gani. Kwa kifupi ni kuwa wengi wangependa kujua kama Chadema watashiriki kwenye uchaguzi kama hapatakuwa na reforms. ACT-Wazalendo wansema watashiriki lakini watalinda demokrasia. Chadema wanatakiwa wa clarify hili maana watu wanahitaji kujitayarisha kugombea kama watashiriki. Kama hawatashiriki watachukua hatua gani kuhakikisha kuwa haufanyiki ( kama ndio nia yao). Muda uliobaki ni mfupi na wanatakiwa ku simplify hoja yao. Hiyo na pamoja ya kuweka wazi cut off date ni lini. Kuwa ikifika tarehe fulani ndio tutafanya uamuzi.

Amandla...
 
..ACT wamesema watashiriki baada ya kutathmini reform zitakazofanyika.

..suala la ACT kushiriki limeachiwa Kamati ya Chama ya viongozi.

..Ni kwamba watu hawafuatilii wanachozungumza ACT, lakini kuna misimamo mikali inatoka haswa upande wa Zanzibar.

..Pia watu hawafuatilii mjadala na mabishano kati ya ACT na serikali kuhusu " kura ya mapema. "

..Zanzibar wana utaratibu wa kupiga kura kwa siku mbili. Siku ya kwanza ni kwa ajili ya wasimamizi na vyombo vya dola. Siku ya pili ni kwa ajili ya wananchi wa kawaida. ACT wanapinga utaratibu huo wakiamini kura siku ya kwanza ni kwa ajili ya kushindilia makura ya CCM.
 
Bottom line ni constituency tofauti zinazogombewa. ACT Wazalendo sio tishio kwenye kiti cha urais hata kama Zanzibar yote itawapa wao kura. CDM wao nguvu yao ni bara na hivyo ndio tishio kwenye suala la urais na uongozi wa Bunge.

Unfortunately mapambano ya ACT Wazalendo Zanzibar hayatiliwi maanani na vyama vya bara maana kwa kiasi fulani wanawaona kama sehemu ya utawala. Hilo la kupiga kura siku mbili wataachiwa wapambane wenyewe. Na wao kwa kiasi fulani wamejitoa katika mpambano una endelea Bara.

Amandla...
 
Back
Top Bottom