ACT-Tanzania yalibomoa gazeti la Mbowe, Tanzania Daima

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
KAMA ni Majanga basi ndio yanayolikuta gazeti la Tanzania Daima ambalo linamilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Freeman Mbowe,baada ya hivi sasa kukimbia na lundo la wahariri na waandishi wake wa Habari, ambapo sasa mwandishi wake muhimu Abdallah Khamis amehama rasmi gazeti hilo linalotoka kila siku. Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Taarifa za kuamika ambazo mtandao huu umezipata zinasema kwa sasa ni wazi gazeti hilo limekuwa likipungukiwa waandishi wake baada ya Mwandishi muhimu Abdalla Khamis kulitema gazeti hilo na kwenda kwenye chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania na kuukwaa nafasi ya Afisa Habari wa chama hicho.

Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko ndani ya Gazeti la Tanzania Daima anasema kwa sasa gazeti limekuwa likipitia katika kipindi kigumu, ambapo anadai kuondoka kwa Abdallah Khamis ni wazi sasa gazeti hilo linaingia kwenye kipindi kigumu.

Pichani ni Abdallah Khamis



IMG-20150313-WA0001.jpg


"Yule bwana Khamis ni mwandishi mmoja ni mzuri sana tena mimi kama mwandishi mwenzake nasikitika sana kwa uongozi kumwacha mwandishi huyo aondoke kirahisi hivyo,maana ukizungumzia Abdalla unazungumia kiungo muhimu sana na sijui hatma ya gazeti baada ya kuhama yeye" ametupasha mtoa huyo taarifa.

Mtandao huu umenasa barua ambayo imethibitisha ni wazi amekuwa Afisa Habari wa ACT-Tanzania, kwa mujibu wa Barua hiyo ambayo yeye Abdallah alikwa akiwataarifu waandishi mbalimbali wa vyombo vya Habari kwamba chama cha ACT-Tanzania kitakuwa na Mkutano mkuu ambao unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Ambapo barua hiyo inasomeka hivi "Chama cha ACT-Tanzania kitafanya Mkutano wa Halmashauri Kuu, Kamati kuu na Uzinduzi wa Chama kuanzia machi 27-29/2015 Kutokana na umuhimu wa chombo chako katika kuupatia umma wa Tanzania habari sahihi, tunakaribisha uwakilishi kutoka kwako katika shughuli hiyo. Tunaomba mtupatie majina ya waandishi na wapiga picha watakaohudhuria matukio hayo kwa siku hizo tatu. Asante kwa ushirikiano wako Abdallah Khamis Afisa Habari".

Nafasi hiyo ya Afisa habari wa chama hicho ilikuwa ikishikiliwa hapo awali na Karama Kaira,ambaye haijasemekana mara moja amepewa nafasi gani ndani ya chama hicho kichanga cha siasa nchini.

Kuhama huko kwa Mwandishi huyo kunazidi kuliacha gazeti la Tanzania Daima katika wakati mgumu ambapo wiki chache zilizopita Gazeti hilo liliondokewa na Mhariri wake muhimu Edson Kamukara ambaye ametimkia gazeti la Mawio, Mbali na Kamukara wahariri wengine waliolikacha Gazeti hilo ni Amana Nyembo ambaye nae ametimkia Gazeti la Mwananchi na kuwa sub editor.

Mhariri mwingine aliondoka Gazeti hilo aliyekuwa Mhariri Mtendaji Ansbert Ngurumo ambayo naye ametangaza kuachana na gazeti hilo ambapo inasemekana anajiaadaa kugombania Ubunge hapo kwenye uchaguzi mkuu hapo baadae kwenye mikoa ya kanda ya ziwa na Nafasi yake kujazwa na kwenye Gazeti hilo ikajazwa na Neville Meena,ambaye alikuwa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Waandishi waliohama.

Achia mbali Wahariri,kuna waandishi mbalimbali waliohama hivi karibu ni Shaban Matutu ambaye amehamia Gazeti la Mtanzania na Lucy ngowi aliyehama hivi karibuni. Wengine waliohama ni Bwana Maziku aliyehamia kwenye Kampuni inayohusika na kusimamia magari ya Uda na kuwa afisa habari.

Source: Tanzaniaclassic.blogspot.com
 
Ushabiki kweli haufai, sasa ww unavyoonge utafikiri huyu mwandishi ndio alilianzisha hili Gazeti, na hata alilianzisha lakini si kuna kufa? Angekufa ungesemaje? Nikuulize swali, je mgunduzi wa Meli bado anaishi? Na kama kafa je Meli hazitengezwi tena?
 
ACT inapoteza mwelekeo wa vita yake. Kama kweli mnatafuta kukubalika nchini yapasa kwanza mjue adui yenu ni nani na mapambano yenu yaelekezwe huko. Kupambana na mtu mmoja mmoja tena kiongozi wa chama cha upinzani kama chenu hamueleweki. Hata hivyo mtu hakai kwenye ajira kwa vile inampa heshima bali kwa kangalia maslahi. What if mhariri huyo kahama kwa kuona maslahi anayopata ni kidogo?
 
Kwahiyo Act ni Gazeti? sio chama cha siasa. kinavuna waandishi toka media mbalimbali

Hii ndiyo inayoitwa "loosing the battle before the battle"! ACT wameshashindwa vita kabla ya vita. Huwezi kuanza vita bila kujua unapigana na nani?
 
ACT Tanzania haiwezi kukibomoa chama cha siasa kwa kumuajiri mfanyakazi mmoja tu.

Kwa taarifa yako tu ni kwamba "waandishi" wa habari ni wengi sana nchi hii na mtu yoyote anaweza kuwa replaced
 
Ushabiki kweli haufai, sasa ww unavyoonge utafikiri huyu mwandishi ndio alilianzisha hili Gazeti, na hata alilianzisha lakini si kuna kufa? Angekufa ungesemaje? Nikuulize swali, je mgunduzi wa Meli bado anaishi? Na kama kafa je Meli hazitengezwi tena?
Mbona unatoa mapovu sana mkuu, mimi nimewahabarisha tu kama ambavyo tunahabarishwa mambo kadha wa kadha humu chumbani, sasa kama limekukera vumilia tu.
 
TataMadiba, hilo "lundo la wahariri na waandishi" waliokimbia Tanzania daima ni wangapi jumla? Na wote wamekimbilia ACT?
Umeshtushwa mpaka kusoma mada yote huwezi, kuwa na moyo mgumu soma yote ujue kwa nini nimesema ACT imelibomoa hilo gazeti.
 
Hii ndiyo inayoitwa "loosing the battle before the battle"! ACT wameshashindwa vita kabla ya vita. Huwezi kuanza vita bila kujua unapigana na nani?
Hahahaa, acheni kutapatapa. Abdallah Kahamis amekwenda kuwa kama alivyo Tumaini Makene pale CHADEMA, patamu hapo.
 
Hahahaa, acheni kutapatapa. Abdallah Kahamis amekwenda kuwa kama alivyo Tumaini Makene pale CHADEMA, patamu hapo.
Kwahiyo sasa tunakwenda kuona watoto wote wa nyumba ndogo wanavyopasuana mchana kweupe kazi kweli.
 
Kesho tutasikia kuwa Nyumbani kwa Mbowe hali ni mbaya kwani House girl wake amehamia ACT hivyo hakuna mtu wa kuosha vyombo na kupiga deki.
Teh! teh! teh! theeeeee!!!!!!!! Wacha ni cheke miye kijukuu cha Sambai maana siasa imevamiwa.
 
ACT inapoteza mwelekeo wa vita yake. Kama kweli mnatafuta kukubalika nchini yapasa kwanza mjue adui yenu ni nani na mapambano yenu yaelekezwe huko. Kupambana na mtu mmoja mmoja tena kiongozi wa chama cha upinzani kama chenu hamueleweki. Hata hivyo mtu hakai kwenye ajira kwa vile inampa heshima bali kwa kangalia maslahi. What if mhariri huyo kahama kwa kuona maslahi anayopata ni kidogo?
Inferiority complex. Umefikia hatua hii ya kujishuku? Pole sana.
 
Yes,Ni uamuzi mzuri,huwezi kufanya kazi kwa MCHAGGA Ukatoka.Ni UBEPARI(UBWANYENYE) VS UTUMWA.Gooood !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom