ACT Tanzania: Taarifa kwa umma

ACT Tanzania: Taarifa kwa umma

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Posts
4,768
Reaction score
5,102
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY
ACT- TANZANIA.
MAKAO MAKUU OFSI YA UENEZI NA MAHUSIANO YA JAMII

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Tanzania, Kadawi Lucas Limbu, kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya ACT-Tanzania, ametengeua uteuzi wa Thomas Matatizo, kuwa mwanasheria wa chama kuanzia leo, tarehe 1 Januari 2015.

Mwenyekiti wa ACT-Taifa, amefuta uteuzi huo kwa kutumia ibara ya 37(w) (vi) ya Katiba ya ACT-Tanzania.

Bw.Thomas Matatizo ametenguliwa uteuzi wake kutokana na kujipa mamlaka ya kufanya kazi asizotumwa na chama, kushirikiana na wanaokidhoofisha chama na kudhihaki maamuzi halali ya kikao yaliyofanyika jana tarehe 31 Desemba 2015 lakini atabaki kuwa mwanachama na mjumbe wa kamati.

Katika kikao hicho, Kamati ya watu 11 iliyopewa mamlaka ya kuongoza chama kwa mujibu wa sheria Na. 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, iliamua kumvua uwanachama, aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT, Samson Mwigamba, Mshauri wa chama Prof. Kitila Mkumbo na wanachama wengine kutenguliwa nafasi walizokabidhiwa kwa nia ya kukieneza chama lakini badala yake wanatumia nafasi hizo vibaya kukigawa na kukihujumu chama

Kwa taarifa hii, tunawaomba umma wa Watanzania kokote waliko, kutosikiliza kauli na vijineno vitakavyotolewa na Bw. Matatizo au Mwigamba. Kauli halali na thabiti ya chama itatolewa na mwenyekiti au yule ambaye amempa mamlaka.

Aidha chama chetu hakijampa mamlaka ya kuthibitisha wala kubatilisha maamuzi ya vikao mtu yeyote, bali sheria mama ya chama yaani katiba ndiyo inaelekeza mamlaka yenye uwezo wa kufanya hivyo.

Grayson Nyakarungu,
Katibu Mwenezi - ACT, Tanzania.
0755 023 503
 
Kwa nini tusimsikilize " Matatizo"?

Huwa kuna pande mbili za taarifa.
Huna mamlaka juu yetu yanani tusimsikilize
Na nani tumsikilze..

Sisi tutachuja baada ya. Kupata. Taarifa za pande zote ....
 
Tz Politics. Hata hivyo, Kitila unapaswa kujitazama mara mbili maana hadhi yako inazidi kuporomoka kiasi kwamba badae utaonekana kuwa katika kundi la WASOMI WASAKA TONGE.
 
Hawa wanapingana juu ya nani awe mwenyekit kati ya zitto na huyu wa sasa .Ila ukiisoma hiyo barua utapata taarifa kuwa ACT hakina maisha hapo mwenyekit angalikuwa mchaga ndio ungesikia lakini nafikiri si mchaga
 
Jana Nimesikia ACT wamepigwa Mtwara kwa kuvamia mkutano wa CUF wakati hawajaalikwa.

Eti kwa kua Zitto alialikwa na wao wakajialika wakiamini Zitto atawabeba.
 
Kitila Mkumbo na mwigamba jifanyieni tathmini kama approach yenu katika siasa za upinzani bado zinakubalika. Kufutwa kwenye position mara mbili na vyama tofauti kwa tuhuma zilezile ni ishara kuwa chama chochote mtakacho kwenda mtarajie hayo hayo. Jitazameni upya inawezekana kabisa appoach zenu zinaweza kuwa sahihi katika nchi nyingine lakini si kwa mazingira ya siasa za Tanzania. Rudisheni akili katika mazingira ya Tanzania la sivyo heshima inazidi kushuka kila uchao.
 
Siasa za bongo ni commend tosha ila prof mkumbo jitafakari tena ni msomi wewe siasa isikufanye ukadharaulika kiasi huko japo upande wenu na mwigamba hatujasikia tutajadili vizuri tukiwasikia kwa act kama muda mfupi tu mmefikia japo mjue kabisaa safari yenu si ndefu kuweni lakini sana uongozi plus tamaa hatarii
 
Tz Politics. Hata hivyo, Kitila unapaswa kujitazama mara mbili maana hadhi yako inazidi kuporomoka kiasi kwamba badae utaonekana kuwa katika kundi la WASOMI WASAKA TONGE.
Wasomi wanapaswa kusimamia ukweli na uhalisia. Na kamwe sio upepo ukoje, KITU AMBACHO KITILYA KIMEMSHINDA. HUYO HAONGOZWI NA TAALUMA YAKE BALI NA NJAA.
Heshima na credibility yake imeshashuka kitambo sana.
 
Namkumbuka sana huya bwana Matatizo, ni mtu mwenye uwezo wa kipekee, kiukweli aliweza kusimamia Chadema Mzumbe ktk mazingra magumu sana na mpaka akafaniksha graduatn ya Chaso kufanyika ktk upngamizi wa hali ya juu. Kiukweli huyu kjana kajichanganya kwenda ACT.
 
Hata hivyo, ACT ni chama cha wasaliti. Hata siku moja wasaliti hawawezi kuacha tabia za kusaliti. Nasubiria wengine pia wasaliti na kupigwa chini. Nyakarungu Upo???
 
Total tragedy to Prof Kitila. Tragedy of political miscalculations.
 
Jana Nimesikia ACT wamepigwa Mtwara kwa kuvamia mkutano wa CUF wakati hawajaalikwa.

Eti kwa kua Zitto alialikwa na wao wakajialika wakiamini Zitto atawabeba.

hii taarifa sio ya kweli ACT walikuwepo na walikuja kumpa kampani zzk hata hivyo ilikua ni vigumu sana kuwajua kwa sababu hawakua na utambulisho wowote i mean hawakuwa na bendera wala tshirt,mara baada ya mkutano kumaliIka nilipata kuongea na kiongozi wa msafara wa ACT, na waliondoka kwa usalama kabisa uwanjani hapo.
 
Tz Politics. Hata hivyo, Kitila unapaswa kujitazama mara mbili maana hadhi yako inazidi kuporomoka kiasi kwamba badae utaonekana kuwa katika kundi la WASOMI WASAKA TONGE.

Mapema sana niliwahi kusema huyu msomi ni msaka tonge. Nadhani sasa kimeeleweka vizuri.
 
duh mnaanza mwaka na gear kali sana....fukuza, simamisha, onyo kal...... wanachama mtapata lini sasa....--
 
Back
Top Bottom