ACT presha ya nini!

ACT presha ya nini!

hivi hiki chama kipo nchi gani maana sijawahi kisikia zaidi ya hapa jf ama fb basi ,huku mitaani ni cdm na ccm ttu
 
Hiki ni chama kipya cha siasa inchini katika kujitambulisha sehemu mbalimbali ,ACT kinajipambanua kama wapigania democrasia wa kweli na wao ni wawazi na kimekuwa kikiwananga wapinzani wenzake hasa CHADEMA eti huko hakuna democrasia wala hakuna uwazi hii imenishangaza kwelikweli,kinajaribu kuwa ambia watu wajiungenacho kwa kuwa hakuna demokrasia ya kweli wala uwazi huko Chadema hapa ndipo ninapo washangaa zaidi,

Nilicho kitegemea mimi viongozi wa chama hichi wangetuuzia sera,itikadi ,dira,mipango,malengo na ilani zoa nilitegemea kuona sera za mazingira,afya,maji,kilimo,uwekezaji ,elimu,uchumi,usawa ,haki na nyingine nyingi kutoka ACT ambazo hazilingani na vyama vingine hasa CHADEMA, lakini mambo ni tofauti wanatuambia tujiungenacho tu kwa kuwa CHADEMA hakuna demokrasia! wala UWAZI haya ni maajabu .Kwa kuwakumbusha tu Chadema kimekuwa sauti ya wasio kuwa na sauti inchini hasa bungeni kimekuwa wasemaji wa watanzania maskini wasio na pa kusemea wamekuwa wawakilishi wa watanzania .

Napenda niwakumbushe ACT kuwa hutukuanza kuipenda CHADEMA hivihivi ila walitenda tukawaona,ACT acheni maneno bila vitendo kwani hizo ni taarabu tu,Napenda kuwa ambia ACT waTZ kwa wingi wao ni maskini wa kutupwa wengi wa walio maliza chuo kikuu wapo mtaani wakirandaranda hakuna ajira, wakulima wengi wanalima kwa jembe la mkono AFYA mbovu elimu inazorota ,barabara mbovu,maji hakuna na mabadiliko hakuna nilitegemea ACT watazungumzia sera hizi na si mapambano walio yaanza,ninapenda kuwaambia ACT hakuna democrasia duniani isiyo na mipaka hakuna.Na napenda kuwa kumbusha wa Tanzania waikumbuke CHADEMA wakati mwingine watakapo piga kura.

Mkubwa

Hao ACT wanatafuta kick kwa Chadema,

Waache wapime wenyewe ili wajue kama Chadema ni saizi yao ama lah. Ukiwajadili wao ndio wanafurahi, ndio kitu roho yao inapenda.

Kwa sasa tuwape muda wajijenge, lakini kick wanayoitafuta kupitia chadema haitowasaidia kiviiiiiiile, maana umri wa Chadema unatosha kabisa kuwa kama sio baba basi mama wa ACT. Sasa baba au mama akipagana na mtoto, si kila mmoja atamshangaa huyo mzazi? Chadema kupambana na CCM ni sawa bin sawia, maana hali ya siasa, uchumi na jamii ingekuwaje nchi hii leo hii bila chama cha imara cha upinzani kama Chadema bara ama CUF pale Zanzibar?
 
naona mzee mtei umeamua kuja kuitetea saccos yako na mkwe wako mbowe. mzee naomba uelewe kwamba saccos yako imeshafilisika, watanzania sio wajinga wa kuburuzwa na saccos yako ya wachaga..hii dhambi ya ubaguzi wa kikanda inaendelea kuwatafuna... mzee mtei . hivi mnavyosema act ni chama cha kiislam na cha waha mnamaanisha nini?
Na sisi tukisema chadema ni chama cha kikristo na cha wachaga mtabisha?
mzee wangu waambie vijana wako waache ubaguzi.
ACT DAIMA. TAIFA KWANZA. CHAMA BAADAE..

si ujiunge huko,mayowe ya nini???
wewe ulishaona wapi chama cha upinzani kinashabikiwa na maccm????? eti wanachama wa ccm ndo hao hao wa act!!!!!!!!! hii ni zaidi ya usanii !
 
Tangu niliposikia maelezo ya ACT siku ya press conference yao, nikawapuuza.
 
chama makini cha ACT ndicho kitakachotuletea maendeleo
 
Back
Top Bottom