ACT; Hii ni Siri msiyoijua, Wenzenu wanaijua ila wamewaficha.

Chama cha wala rushwa na watoa rushwa hiko,kinatumia pesa za walipa kodi kununua madiwani na kujifanya kinaungwa mkono.bora nibaki niwe sina chama kama nilivyo,lkn sio kwenda chama cha kijani
Lakini Mkuu usipokuwa na chama na usipokuwa kiongozi, unaacha gap kwa hao unaodhani hawafai kuwa viongozi wako.

Any way, nakushauri tuungane kutoe elimu na hamasa itakayotusaidia kujenga vyama bora na kuandaa viongozi bora
 
Hongera sana mleta mada, hongera sana.
Asante ndugu yangu, naomba tuungane kutoa elimu na hamasa inayoweza kutusaidia kujenga vyama bora na viongozi bora. Hii ni moja ya njia kubwa inayoweza kutusaidia kuwa na Tanzania tuitakayo. Tanzania tuitakayo haziwezi kuja kwa bahati Nasibu tu kama wengi wanavyoamini.
 
Mkuu, mimi ni mmoja wa watu wanaojitahidi sana kutoa elimu ya uraia ikiwemo humu jukwaani. Nipigie makofi kwanza kwa hilo. Ama si stahili!? Joking!

Mbona sijawahi kuambiwa mchochezi wala kugombana na mtu?

Ujue kuna watu wanaodhani kuwa upinzani maana yake kugombana na watu, kugombana na serikali, kuumia n.k Ifike mahali ieleweke kuwa hizo ni kama ajali na sio lengo la msingi, kwa hiyo inapofaa kuepuka ni vizuri kuepuka. Yapo mambo mengi yanaweza kufanywa na vyama vya upinzani na yakawa na manufaa makubwa kwa vyama vyenyewe na Taifa kwa ujumla tena bila kugombana na mtu. Ukitaka kuyajua ni yapi, pitia nyuzi zangu za nyuma na kama utakuwa na swali utauliza. Napenda uelewe ukawaeleweshe na wengine ndugu yangu.
Utapataje wanachama ki-eletronic! Ili kupata wanachama unahitaji mkutano uweze kujibu hoja za wananchi! Mikutano ya ndani imezuiliwa sasa unafanyaje siasa!!!
 
Lakini Mkuu usipokuwa na chama na usipokuwa kiongozi, unaacha gap kwa hao unaodhani hawafai kuwa viongozi wako.

Any way, nakushauri tuungane kutoe elimu na hamasa itakayotusaidia kujenga vyama bora na kuandaa viongozi bora
Ni kweli sina chama lkn ni mpiga kura mzuri tu,na nitakuwa hivyo maisha yangu yote,kwa sababu wanasiasa sio watu wa kuwaamini kabisa,ona huyu jamaa alivyoaminiwa na akapewa ridhaa kwa anayoyafanya sasa.mwanzoni alianza vizuri lakini sasa ni vituko vitupu.
 
Ni
Mkuu, kuna tatizo kubwa sana la "Misconception" miongoni mwa vyama vya siasa vya upinzani Tanzania. Yaani wanaamini siasa za upinzani maana yake maandamano, mikutano majukwaani na kusikiliza Rais Kasema nini nao waseme kinyume chake na nje ya hapo hamna cha kufanya. Hii si sawa. Wanakuwa wamejifungia kwenye kaduara kadogo sana kifikra ama kwa kutokujua ama kwa kutokutaka kufikiri nje ya box.

Inafaa vyama vya upinzani viweze kusoma mazingira na nyakati na kuweza kuendeana nayo badala ya kulazimisha kwenda vile walivyozoea. Mazingira yanabadilika, watu wanabadilika, utawala unabadilika n.k. Ni lazima wapinzani nao wajifunze kubadilika kwa kweli. Unajaribu kupita njia ambayo kila ukijaribu unakwama ila unang'ang'ana tu eti kwa hoja kuwa jana ulipita hapo? kweli?

Ni kupe mfano mmoja rahisi sana kueleweka, hivi ni watu wangapi wanahudhuria mkutano wa hadhara wa kawaida na ni watanzania wangapi unaweza kuwafikishia ujumbe huo huo ambao ungefikisha kwenye mkutano, lakini ukaufikisha kwa njia za elektroniki na kila mmoja akauona akiwa nyumbani kwake? Tatizo Content unayo?
Ninge comment lakini basi
 
Utapataje wanachama ki-eletronic! Ili kupata wanachama unahitaji mkutano uweze kujibu hoja za wananchi! Mikutano ya ndani imezuiliwa sasa unafanyaje siasa!!!
Acha ubishi ndugu, . Usipende kufikiria kushindwa hata kea vitu simple vinavyowezekana.

Hapa wewe unataka ubishe tu ili baadae u conclude kuwa haiwezekani. Usipoweza wewe wenzako wataweza na kukuongoza nawe utabakia kulalamika tu kuwa canal kandamiza. Ni vyema wale wanaoamini wana mawazo mazuri wakaamka sasa, vinginevyo wakiendelea kusema haiwezekani, wenye mawazo mabaya watasambaza na kusimamia mawazo yako na wenye mawazo mazuri watakoma kwa kutokuwajibika
 
Ni kweli sina chama lkn ni mpiga kura mzuri tu,na nitakuwa hivyo maisha yangu yote,kwa sababu wanasiasa sio watu wa kuwaamini kabisa,ona huyu jamaa alivyoaminiwa na akapewa ridhaa kwa anayoyafanya sasa.mwanzoni alianza vizuri lakini sasa ni vituko vitupu.
Ukiishia kuwa mpiga kura tu basi, unaweza ukajikuta una machaguo mawili na yote hayafai ila lazima uchague moja. Ndio maana nafikiri kuna haja ya kufanya kitu zaidi ya kupiga kura, na kitu hicho ni pamoja na kuandaa hao wapigiwa kura ambao ni potential.
 
Ni

Ninge comment lakini basi
Hicho kinachokufanya udhani una mawazo sahihi lakini hata kuyasema unaogopa lakini wale wenye mawazo yasiyosahihi hawaogopi; huyo ndio adui yako, wala adui yako sio serikali kama unavyofikiri.
 
Kiongoz nimekufwatilia vizur sana,na naweza sema umeandika vizuri ila mawazo yako yalipaswa yachukuliwe na vyama vyote vya siasa ikiwepo na chama tawala.mana ata chama tawala hakina jambo jipya kwa wananchi na nchi kwa ujumla zaidi ya porojo zasiasa za toka uhuru ndo maana kama nchi tumeshindwa kupiga hatua kubwa za maendeleo ukilinganisha na muda na rasilimali zilizopo.chama kilichopo madarakan leo kipo sio kwasababu kina sera nzuri bali ni mnufaika wa mfumo toka uhuru kwasababu wao ndio waliokuwepo toka mwanzo.sasa na vyama vyaupinzani vilivyokuja kuibuka badae navyo vikawa havina jambo jipya tofaut na chama tawala linaloenda moja kwa moja kwa wananchi ndo maana vimekua na agenda chache kati ya nyingi zinazoweza kulisaidia taifa japo naweza sema vimejitahid sana kwasababu ya changamoto wanazokutana nazo.Kwaiyo mawazo yako ni mazuri ila ili hivi vyama kufanya hayo lazima kwanza kuwe na haki na Usawa wa shughuli zakisiasa,kwa maana ya vyama vyote kua na usawa wakufikia wananchi nakufanya hayo uliyoyasema bila kuingiliwa au kuingiliana vyenyewe kwa vyenyewe ili kudhoofishana.vinginevyo aya mambo yatabak kwenye makaratasi nakuendelea na siasa zetu hiz hizi za sasa.
 
Ni ushauri makini, lakini kilicho muhim sana kwa sasa ni kudai uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima na katiba mpya.
 
Ni ushauri makini, lakini kilicho muhim sana kwa sasa ni kudai uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa nchi nzima na katiba mpya.
Shida ni kwamba unapotegemea third party kama msingi wa mafanikio yako, unachotaka third party afanye anaweza asikifanye milele. Kwa hiyo isitegemee third part iwe ndio cause agent.

Kwa mfano unayetaka akupe hiyo katiba unayotaka kwanza ndio ufanye mambo ya maana asipokupa utafanyaje?

Mimi naona kuna vitu vingi tu tunaweza kulifanyia kwenye mazingira haya haya na tukafanya vizuri. Mfano angalia tu hapa ukileta Uzi wa maana wachangiaji hamna ila leta ujinga tu uone watu watakavyojaa, unadhani tatizo katiba?
 
mkuu bethlehem safi sana kwa ushauri mujarabu kabisa kwa ndugu zetu hawa wa act........kazi kwao sasa kufuata au kjifanya viburi kama jamaa zetu walee ambao sasa wanatapatapa!!
 
Hivyo vita ndio vimeanza leo au vimeanza tangu vyama vingi vilipoanzishwa? Vyama vya upinzani vina matatizo yale yale tangu mfumoo wa vyama vingi ulipoanzishwa na ndio maana hadi leo hawajaweza kufanikiwa. Hiyo chadema yenyewe unayoizungumzia haijawahi kufikia malengo hata mara moja na ikiendelea inavyokwenda itakuwa inarudi nyuma kila siku na mwishowe itapotea. Sasa ukiwa unalalamika tu, Vyama vya upinzani vimeanza kulalamika toka kipindi hicho hadi leo tu vinalalamika, kulalamika sawa, ila haiwezi kuwasaidia. Hakuna anayesikiliza malalamiko yao. Ni lazima kuangalia ni nini cha kufanya na si kufanya tu ili iwe wamefanya, kufanya ili wafanikiwe. Sijui tunaelewana sasa?
cdm kufa ilisha tabiliwa kufa toka mnaanzidha ACT ukweli yamekushinda ACT sasa umekaa mbali umewaachia mfupa wenzako unajifanya mshauri

wewe huwezi kamatwa na tena hutakuja kamatwa kama utaendelea kuongea vitu rahisi kama hivyo, watawala hawatakuja kaa watishwe na huo ushauri mwepesi

wenzako wako kwenye battle ndio maana wanapigwa risasi wanafungwa kila siku kwa sababu wanaongea vitu vigimu mbele ya watawala
 
Mkuu,
Ni aibu Mwanaume kujinasibisha na mwanamke,
Ni aibu kucoment issue za msingi bila kusoma na
Ni aibu kwenye vitu serious kutoa ushauri bila bases.

Vineno viwili vimekuchoma mwanamke wewe ha ha haaaaaaa
 
cdm kufa ilisha tabiliwa kufa toka mnaanzidha ACT ukweli yamekushinda ACT sasa umekaa mbali umewaachia mfupa wenzako unajifanya mshauri

wewe huwezi kamatwa na tena hutakuja kamatwa kama utaendelea kuongea vitu rahisi kama hivyo, watawala hawatakuja kaa watishwe na huo ushauri mwepesi

wenzako wako kwenye battle ndio maana wanapigwa risasi wanafungwa kila siku kwa sababu wanaongea vitu vigimu mbele ya watawala
Kukamatwa sio sifa wala sio sehemu ya mafanikio Bali hiyo ni kama ajali. Sijambo la kutegemewa kuona eti MTU anajisifu kuwa kiashiria chake cha mafanikio ni yeye kukamatwa Mara kwa Mara, huo ni ujinga.
 
Kukamatwa sio sifa wala sio sehemu ya mafanikio Bali hiyo ni kama ajali. Sijambo la kutegemewa kuona eti MTU anajisifu kuwa kiashiria chake cha mafanikio ni yeye kukamatwa Mara kwa Mara, huo ni ujinga.
endelea kuamini hivyo kinadharia zaidi kuliko hali halisi iliyopo kwenye ground tena ukiwa nyuma ya keyboard na id fake ni rahisi sana, watawala hawatishwi hata siku moja na hizo nadharia na tena wangependa iwe hivyo

ila ukweli ni kwamba hiyo kamata kamata unayoiita wewe ni ujinga ndio inayotisha watawala na imewafanya wanasiasa wengi wafanikiwe hadi kuingia ikulu

labda ungeniambia kwa mfano ni mwanasiasa gani africa amefanikiwa kwa siasa hizo za nadharia bila kuteswa na kuswekwa ndani na watawala

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Betlehem, hizo stats umezitoa wapi? Nini source ya kuzijustify? Au ni mawazo yako tu!
 
Back
Top Bottom