Achomwa kisu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Achomwa kisu

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Mar 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Amani [​IMG]
  [​IMG]
  Na Mwandishi Wetu
  Mkazi mmoja wa Manzese Argetina, jijini Dar es Salaam, aliyetambuliwa kwa jina la Richard Epro (28), amechomwa kisu mbavuni na kijana mwenzake aliyejulikana kwa jina la Calvin Henry baada ya kukataa kumuuzia kipisi cha bangi... Akiongea na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kwamba, Richard ambaye ni muosha magari katika Kituo cha Mabibo Mwisho, anadaiwa kuwa anafanya biashara ya bangi akishirikiana na wenzake.

  [​IMG]
  “Calvin alifika hapa Mabibo majira ya mchana na kumkuta Richard akiwa bize na kazi yake ya kuosha gari, akamtaka amuuzie bangi, lakini kijana huyo alimkatalia akidai kuwa anayefanya biashara hiyo hakuwepo na kwamba yeye si muhusika. Jamaa alipoambiwa hivyo akasema hataki kusikia maneno hayo hivyo kumlazimisha amuuziwe,” alisema shuhuda wetu.

  Aliongeza kuwa, Richard alipoona anazidi kusumbuliwa huku akiwa kazini, aliamua kumsukuma akijua labda litakuwa ndiyo suluhisho la Calvin kuondoka lakini badala yake, aliangukia kwenye mtaro wa maji machafu na ndipo balaa lilipoanza.

  “Baada ya kuona kasukumwa na kuangukia kwenye mtaro wa maji machafu, Calvin alinyanyuka na kutoa kisu kisha kumchoma nacho Richard mbavuni na kumsababishia kutokwa na damu nyingi na alipoona hali hiyo alianza kutimua mbio lakini majeruhi alijitahidi kupiga yowe za mwizi, ndipo watu wakajitokeza na kumsaidia kumkamata mtuhumiwa,” alisema shuhuda huyo.

  [​IMG]
  Alisema mtuhumiwa aliponyoka na akakimbilia katika ghorofa B la Urafiki ambapo alipanda juu lakini wananchi walimfuata huko na kufanikiwa kumkamata na kumteremsha chini kisha wakamfikisha Kituo cha Polisi Urafiki na kuwekwa rumande.

  Habari zinasema, baadaye polisi walifika eneo la tukio wakamchukua majeruhi wakampeleka kutibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

  “Mganga mkuu wa hospitali hiyo alishauri apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na jeraha lake alilolipata kuwa kubwa,” alisema mtoa habari huyo.

  Hadi tunakwenda mtamboni, polisi walithibitisha kuwa mtuhumiwa alikuwa bado anashikiliwa katika Kituo Cha Polisi Urafiki akisubiri kufikishwa mahakamani.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  uwazi [​IMG] [​IMG]Katika tukio moja askari mmoja wa Kampuni ya Ulinzi ya Flamingo Security iliyopo Kimara jijini Dar es Salaam ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, aliuawa kikatili na watu wasiojulikana akiwa katika lindo lake, Upanga nyumba iliyopo Plot namba 191 mtaa wa Mazengo wilayani Ilala.

  Watu waliokuwa katika eneo la tukio waliliambia gazeti hili kuwa askari huyo aliuawa na kikundi hicho cha watu kisha mwili wake kutupwa katika chumba cha choo huku akiwa amefungwa kamba miguuni, mikononi pia walimjaza vitambaa mdomoni.

  Taarifa zaidi zilidai kuwa dalili za maiti hiyo zilionyesha kuwa wauaji hao walimnyonga askari huyo kutokana na alama zilizokuwepo shingoni.

  Mwili wa marehemu uligunduliwa na watu waliokwenda katika eneo hilo kisha kutoa taarifa polisi ambapo walifika na kuupeleka katika Hospitali ya Amana.

  Wakati huo huo, mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Moshi anayedaiwa kuwa ni jambazi, alipigwa vibaya na wananchi wenye hasira pale alipokutwa katika jaribio la kuiba gari ya Afisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

  Inadaiwa kuwa, jambazi huyo akiwa na wenzake ambao walitimua mbio, walitaka kuiba gari hilo majira ya saa 2.00 asubuhi katika Mtaa wa Samora.

  Mmiliki wa gari hilo, inadaiwa kuwa aliingia ofisini ambapo aliwahi kutoka na kuwaona
  majambazi hao wakifungua gari ndipo alipiga mayowe yaliyosababisha wasamaria wema kutokea.

  Habari zinasema kuwa kufuatia mayowe hayo, walijitokeza wananchi wenye hasira ambao walimponda kichwa na sehemu zingine za mwili hadi kupoteza fahamu.

  Imeelezwa kuwa jambazi huyo akiwa hajitambui, polisi waliokuwa doria walifika katika eneo la tukio ambapo walimchukua na kumpeleka katika Hospitali ya Amana kwa matibabu.

  Aidha, katika maeneo ya stesheni jijini Dar es Salaam, kijana mmoja anayedaiwa kuwa ni kibaka aliokolewa na askari polisi wakati wananchi wenye hasira walipotaka kumuua kwa kuhisi alitaka kuwaibia abiria waliokuwa wakisafiri kwa treni ya kwenda bara.

  Habari zilizopatikana eneo la tukio zilidai kuwa, kijana huyo alikamatwa wakati akitaka kumuibia abiria mmoja fedha mfukoni ndipo alipewa mkong’oto uliokwenda sambamba na kuchaniwa suruali na nguo zake za ndani hivyo kufikishwa Kituo cha Polisi Kati (Central Police) akiwa mtupu.

  Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Bw. Masindoki Masindoki
  hakupatikana kuelezea matukio hayo.

  Naye mwandishi wetu Issa Mnally anaripoti kuwa kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana, mwishoni mwa wiki iliyopita alipata kipigo kikali kilichosababisha kupoteza fahamu baada ya kuvunja mlango wa gari na kumwibia mzungu mmoja raia wa Canada begi lenye nyaraka mbalimbali.

  Tukio hilo lilitokea Kijitonyama nje ya Hoteli ya Mallenium Tower Makumbusho jijini Dar es Salaam baada ya mzungu huyo kuegesha gari yake aina ya Tata.

  Habari zinasema baada ya mzungu huyo kuteremka na kuingia katika jengo hilo ndipo kijana huyo alipovunja mlango wa gari hilo na kuiba bengi lakini mzungu alirudi ghafla na kumfuma akifanya uhalifu huo.

  Walinzi wa maeneo hayo na wajenzi wa barabara ya Ally Hassan Mwinyi, walimkimbiza na walipomkamata walimpa kichapo kilichosababisha apoteze fahamu.

  http://www.globalpublisherstz.com/2008/01/22/dar_kama_kenya.html
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  <table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="100%"><tbody><tr><td align="left"><table bgcolor="#dddddd" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" height="23" width="100%"><tbody><tr><td width="606">

  </td> <td align="right" width="139">photos</td> <td align="right" width="12">
  </td> </tr> </tbody></table></td> </tr> <tr> <td bgcolor="#999999">[​IMG]</td> </tr> <tr> <td class="shortnews" align="left" bgcolor="#ffffff" valign="top">
  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Rais Jakaya Kikwete akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo rasm&#305; kat&#305;ka ikulu ya Ankara nch&#305;n&#305; Uturuk&#305;.Pemben&#305; ak&#305;ms&#305;k&#305;l&#305;za n&#305; Rais wa nch&#305; hiyo Abdullah Gul.Ra&#305;s K&#305;kwete yupo kat&#305;ka z&#305;ara ya kikazi nchini Uturuki

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  JK na mwenyeji wake Ra&#305;s wa Uturuki Abdukkah Gul wak&#305;kagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya Rais K&#305;kwete kuwasili katika ikulu ya nch&#305; h&#305;yo iliyopo jijini Ankara

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Rais wa Uturuki Abdullah Gul na mkewe wakiwakaribisha ikulu ya j&#305;j&#305;n&#305; Ankara JK Mama Salma.

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akimkaribisha JK ofisini kwake jijini Ankara, Uturuki.

  <!--ThumbBegin-->[​IMG]<!--ThumbEnd-->
  JK akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kitaifa (State Baquet) iliyofanyika katika ikulu ya nchi hiyo jijini Ankara, wa tatu kulia ni mwenyeji wake Rais wa Uturuki Abdullah Gul na kushoto mke wa Rais wa Uturuki Hyrunisa Gul.Kulia ni Mama Salma Kikwete.​

  </td></tr></tbody></table>
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Bodi ya Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Dunia (WB), imeidhinisha mkopo wenye thamani ya Dola milioni 40 za Marekani kwa ajili ya kufanikisha mradi wa kufadhili ujenzi wa makazi hapa nchini.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na WB, fedha hizo zilitolewa kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa (IDA).
  Malengo ya mradi huo ni kuanzisha mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, itakayotolewa kwa masharti ya kulipwa katika muda mfupi na mrefu.
  Tatizo hilo linaongezeka kila mwaka, ikiwa ni matokeo ya ukosefu wa mikopo ya ujenzi wa makazi, sekta rasmi ya ujenzi wa nyumba za kuishi, kasi ya ukuaji wa idadi ya watu, kuanzishwa na kukua kwa miji.
  "Kwa kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa makazi, fedha hizi zitasaidia kuibua ukuaji bora wa uchumi, ambao matunda yake ni kuwepo ajira na kupunguza umasikini," alisema Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, John Murray McIntire. Kuibuliwa kwa mradi huo kumechochewa na maboresho ya hivi karibuni kuhusu mazingira ya mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
  Kupitishwa kwa sheria namba 17 ya mwaka 2008 inayohusu nafasi ya mikopo katika kufanikisha ujenzi wa nyumba, imechochea kasi ya serikali kuwa na mfuko wa fedha za ujenzi wa nyumba na kusababisha matarajio makubwa.
  Pia, mpango mahususi wa Benki Kuu ya Tanzania (Bot) kwa ajili ya asasi ndogo za fedha, unaziwezesha (asasi) kuwa imara katika sekta ya fedha, kuinufaisha jamii kwa kutumia mgawanyo mdogo wa fedha, hivyo kuwa miongoni mwa mazingira yaliyofanikisha mradi huo.
  Kiongozi wa kikosi kazi cha utekelezaji wa mradi wa WB nchini, Michel Noel, alisema soko la mikopo linawatenga watu wengi katika kuboresha makazi yao.
  Alisema hali hiyo inaibua haja ya kuwepo mpango bora wa fedha utakaowafikia wasionufaika na mikopo michache inayotolewa sasa, ili wakamilishe ujenzi.
  Hii ni mara ya tatu kwa IDA kuidhinisha fedha kwa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2009/2010, hivyo kufanya kiasi cha jumla yaka kufikia Dola milioni 250.  CHANZO: NIPASHE
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amekanusha vikali kwamba serikali imelegeza msimamo wake wa kukataa kununua mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Dowans Tanzania Limited na sasa iko katika mchakato wa kuinunua.
  Hivi karibuni uliibuka uvumi kuwa serikali imeamua kuinunua mitambo hiyo licha ya kusitisha mipango hiyo baada ya shinikizo la Bunge mwaka jana.
  Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Waziri Ngeleja alisema kuwa taarifa hizo si za kweli kwani msimamo wa serikali ni kutoinunua mitambo hiyo yenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 100.
  “Unajua hayo ni maneno tu ya mitaani labda ndio wanadhani kuwa serikali itanunua mitambo ya Dowans, ila napenda kuwahakikishia wananchi kuwa serikali haipo kwenye mchakato huo kama wanavyofikiria,” alisema Waziri Ngeleja.
  Moja ya maazimio ya Bunge katika mkutano wake wa Februari mwaka 2008 ni kuitaka serikali kuvunja mkataba na Dowans, ambayo ilirithi mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kutoka kwa kampuni tata ya Richmond Development (LLC) ambayo ilibainika kupata zabuni hiyo kinyume cha sheria na taratibu.
  Vile vile uchunguzi uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, kuichunguza Richmond nje na ndani ya Tanzania ulibainisha kuwa ilikuwa kampuni ya kitapeli.
  Baada ya kubainika kuwa serikali iliipa zabuni hiyo kwa njia za upendeleo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili walioiongoza Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi walilazimika kujiuzulu. Kabla serikali haijatangaza nia yake ya kutoinunua mitambo hiyo, ulizuka mjadala mkubwa uliowahusisha wabunge, maofisa wa serikali, wanasiasa na makundi mbalimbali ya jamii huku kundi moja likitaka inunuliwe na lingine likipinga.
  Hoja kwamba serikali imebadili nia kuhusu mitambo ya Dowans ilitiwa nguvu na habari zilizozagaa mitaani hivi karibuni na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba zabuni ya ununuzi wa majereta ya kuzalisha umeme wa magewati 160 imesitishwa kwa kuwa sasa mchakato ni kununua Dowans.
  Serikali ilisimamisha mchakato wa zabuni uliokuwa umefikiwa na Tanesco, na kutoa siku 90 kwa ajili ya kupitiwa kwa taratibu zite za zabuni kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma.
  Serikali ilichukua uamuzi huo baada ya kugundua kulikuwa na ukiukaji wa taratibu kama zilivyoanishwa kwenye sheria ya manunuzi ya umma. Kwa hili hiyo, Waziri Ngeleja alisema zabuni hiyo sasa itafunguliwa Machi 19, mwaka huu (Ijumaa ya wiki ijayo).
  Wakati huo huo, Waziri Ngeleja jana alisaini mkataba wa makubaliano baina ya wizara yake na Kamati Tekelezi Tasnia ya Uziduaji (EITI).
  Alisema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuendeleza na kudumisha uwajibikaji na uwazi wa utoaji wa taarifa kuhusu mapato yanayotokana na uvunaji wa rasilimali za madini. Aidha, alisema EITI ni taasisi itakayosimamia utekelezaji wa programu na taratibu zinazotambulika kimataifa katika kuweka uwazi wa mapato ya uvunaji wa rasilimali za madini, gesi asilia na mafuta kwa umma.
  Alisema suala hilo litasaidia kuwawezesha wananchi kufahamu mchango wa rasilimali hizo katika maendeleo ya nchi.
  “Suala ni kwamba wananchi watapatiwa taarifa sahihi za mchango wa uwekezaji katika rasilimali za nchi na hivyo kujenga imani kwa serikali katika kuwaletea maendeleo endelevu kupitia taasisi hiyo,” alisema Ngeleja. Kwa mujibu wa Ngeleja, serikali ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha makundi ya kijamii pamoja na makampuni yanahusika katika kuunda kamati tekelezi ya EITI yenye wajumbe 15 watakaosimamia suala hilo.
  Ngeleja alisema utekelezaji wa shughuli hizo unahitaji ushirikishwaji wa jamii, makampuni na ngazi mbalimbali katika serikali ili kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana kupitia rasilimali hizo.
  Aliongeza kuwa serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa sheria itakayosimamia shughuli za Tasnia ya Uziduaji na kwamba hivyo inakusudia kuanzisha mchakato wa utungaji wa sheria hiyo.
  Aidha alisema taasisi hiyo tayari imeshaanza kazi, ila kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuandaa muswaada ili upelekwe bungeni katika mkutano ujao.
  Alisema asilimia 45 ya mapato ya nchi hutokana na madini, hivyo taasisi hiyo itasaidia kuongeza uwazi wa upatikanaji wa matumizi hayo katika rasilimali ya nchi.
  Mwenyekiti wa Tasnia ya Uziduaji, Jaji Mstaafu Mark Bomani, aliahidi kuwa taasisi hiyo itafanya kazi kwa uwazi na uadilifu ili rasilimali za nchi zinufaishe taifa pamoja na wawekezaji.  CHANZO: NIPASHE
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Tume ya Ushindani (FCC), imesema tatizo la kuingia kwa bidhaa bandia nchini linachangiwa na baadhi ya maofisa wa serikali wasio waaminifu ambao hula njama na wafanyabiashara wanaoziingiza.
  Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa tume hiyo, Gregory Ndanu, wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kukabiliana na bidhaa bandia na hatimiliki.
  Mkutano huo uliandaliwa na Ubalozi wa Marekani.
  Alisema kuna maofisa wasio waaminifu hivyo kuna umuhimu wa kuimarisha taasisi zote zinazohusika katika mkakati wa kupambana na bidhaa bandia. "Taasisi zote zikiimarishwa na uaminifu ukawepo, tunaweza kupunguza tatizo hili kwa kiasi kikubwa sana," alisema.
  Alisema wauzaji bidhaa bandia wamekuwa wakijali maslahi yao binafsi bila kujali afya za watumiaji wa bidhaa zao.
  Aidha, alisema hata kesi ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mahakamani huchelewa hivyo kuwa moja ya vikwazo vya kupambana na bidhaa hizo.
  Alisema FCC imekuwa ikitaifisha bidhaa bandia kila zinapokamatwa na wahusika wamekuwa wakitozwa faini kati ya Shilingi milioni moja hadi tano.
  Alisema hadi sasa FCC imeshateketeza bidhaa bandia zenye thamani ya Shilingi bilioni mbili.
  "Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa bandia wameanza kuwa waoga, FCC wakati mwingine tukiamua kuwapeleka mahakamani adhabu inakuwa hadi Sh. milioni 50," alisema.
  Naye Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, alisema bidhaa bandia bado ni tatizo hata Marekani, Afrika Mashariki na karibu duniani kote.
  Alisema kumekuwa na bidhaa bandia za dawa za binadamu, vipodozi na vinywaji hali inayotishia afya za wananchi.
  Alisema Marekani imeona njia bora ya kupambana na bidhaa hizo na wizi wa kazi za wasanii ni kuimarisha taasisi zinazohusika na udhibiti wa bidhaa na mwaka 2000 walianzisha bodi ya kusimamia hakimiliki katika mji wa Virginia.  CHANZO: NIPASHE
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ghorofa Dar hatarini kuanguka, lipo Kariakoo [​IMG] Wananchi wakilitazama jengo la ghorofa 8 liliopo katika makutano ya Mtaa wa Mafia na Swahili ambalo limezuiwa kuendelea na ujenzi jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Wiliam Lukuvi, kutokana na ujenzi hafifu uliosababisha kuweka nyufa sehemu ya chini ya jengo hilo.
  Vicky Kombe na Emerentiana Masondole
  WAKAZI na watu wanaofanya shughuli zao maeneo ya Kariakoo jana walipata kitu kingine cha kushangaa lakini kinachotishia usalama wao; jengo la ghorofa nane lililo na ufa na ambalo wakati wowote linaweza kuanguka eneo hilo la kibiashara lenye watu wengi.

  Watu wengi walikuwa wamesimama chini ya jengo hilo lililo kwenye makutano ya Mtaa wa Swahili na Mafia baada ya kupata habari kuwa liko hatarini kuanguka kiasi cha serikali ya mkoa kusimamisha ujenzi wake ikiwa ni miaka michache tangu iundwe kamati iliyopewa jukumu la kuchunguza majengo yaliyojengwa chini ya viwango, lakini ripoti yake ikatiwa kapuni.

  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa serikari imesimamisha ujenzi wa jengo hilo kwa sababu linaweza kusababisha maafa makubwa baada ya kupata ufa mkubwa katika ghorofa ya kwanza.

  "Linaweza kusababisha maafa makubwa kwa wakazi wanaoishi karibu na eneo hilo pamoja na watu waliokuwa wakiendesha shughuli zao katika ghorofa hilo," alisema Lukuvi akizungumzia jengo hilo linalomilikiwa na Salmin Mohamed.

  Lukuvi pia alisema kuwa kutokana na hatari inayoweza kusababishwa na kuanguka kwa jengo hilo, serikali imeamua kufunga barabara ya Mtaa wa Mafia kuanzia makutano ya Mtaa wa Nyamwezi mpaka makutano ya Mtaa wa Sukuma.

  Lukuvi alisema Mtaa wa Swahili pia utafungwa kuanzia makutano ya Mtaa wa Mkunguni na Swahili mpaka makutano ya Mtaa wa Kariakoo na Swahili.

  Lukuvi alisema kuwa waliojadili na kuandaa usalama wa jengo hilo walipendekeza kwamba mabasi ambayo yalikuwa yakitumia barabara ya Mtaa wa Swahili na Mtaa wa Mkunguni kuingia eneo la soko la Karikaoo, sasa yatatakiwa barabara ya Mtaa wa Sikukuu.

  Hatari ya jengo hilo kuanguka imekuja katika kipindi ambacho usalama wa majengo mengi jijini Dar es salaam na hasa eneo hilo la katikati ya jiji ukionekana kuwa mdogo. Mwaka 2006 jengo la hoteli ya Chang`ombe Village lilianguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

  Mwaka 2008, jengo la ghorofa kumi la kampuni ya McSon lililokuwa Mtaa wa Kisutu lilianguka na watu kadhaa waliliripotiwa kufa.

  Baada ya jengo la Changombe Villa kuanguka, waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliunda tume kukagua majengo ambayo yalijengwa kwa kukiuka taratibu na kwa mujibu wa Waziri Mkuu Mizengo PInda aliyekariri ripoti hiyo ya tume hiyo bungeni, zaidi ya mejngo 100 yalikiuka taratibu za ujenzi.

  Pinda aliliambia Bunge kuwa ripoti hiyo ilibaini pia kuwa maghorofa 81 yalibainika kukiuka masharti ya ujenzi, wakati wamiliki wa maghorofa 22 yaliyojengwa bila kufuata sheria za ujenzi hawakupatikana.

  Wakati huohuo, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi, Tanzania Boniphace Muhegi alisema kuwa kutokea kwa ubovu wa majengo na kutokuwa na ubora kunasababishwa na vifaa duni vinavyotumika katika kazi za ujenzi.

  "Ubovu wa majengo kutokidhi ubora kwa kiwango kinachohitajika unatokana na elimu duni na vifaa hafifu vinavyotumika katika kujengea pamoja na uzembe wa msimamizi wa kutotembelea eneo la ujenzi,"alisema Muhegi.

  Aliwataka wasimamizi wa majengo kuwa makini wakati yanapojengwa ili watoe taarifa kwa sehemu husika endapo wataona dalili za jengo kutokidhi ubora.

  Jengo lilo linamilikiwa na Salimin Mohamed ambapo walipangisha wafanya biashara na makazi ya watu.


  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18470
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  photos [​IMG] Mwalimu wa Shule ya Msingi Muongozo iliyopo mtaa wa Mafere, Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina moja la Kuboja, leo mchana ametupiwa vyombo nje kutoka kwenye nyumba ya shule aliyokuwa anaishi, amri ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa Wilaya.

  Imeelezwa kuwa mwalimu huyo alishapewa barua ya uhamisho kutoka shule hiyo kwenda Shule ya Msingi Mikumi iliyopo Magomeni, agizo ambalo alilikaidi licha ya kupewa notisi ya miaka mitatu ili ahame.

  Inadaiwa kuwa baada ya kukaidi amri hiyo, serikali iliwatuma watu mara kadhaa ili kwenda kumhamisha lakini alikuwa akiwatolea panga na kuwafukuza hivyo walishindwa kumtoa hadi leo ambapo wameenda na kumkosa, hali iliyowalazimu kumtolea vitu vyake vyote.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Shuma, alikataa kuongelea kabisa suala hilo na kudai kuwa ni amri kutoka kwa Mkurugenzi hivyo yeye hana lolote la kuongea.
  Pamoja na hayo yote, Mwalimu Kuboja amefundisha katika shule hiyo kwa muda wa miaka 11 kabla ya kuhamishwa.

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
  Baadhi ya vitu vya mwalimu Kuboja vikiwa vimetolewa nje na wagambao wa jiji

  [​IMG]
  Picha hii inaonyesha ndani ambapo alikuwa akiishi mwalimu huyo
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  NATESEKA

  ijumaa [​IMG]
  [​IMG]

  Na Mwandishi Wetu

  Ikiwa ni miezi kadhaa imekatika toka akumbwe na skendo ya kupiga picha za ngono, mnenguaji mkongwe wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ aliye pia ‘mnyapala’ wa safu ya wacheza shoo, Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’, anadaiwa kuibuka kutoka mafichoni akielezea mateso aliyoyapata kufuatia kuandikwa kwa skendo hiyo...
  Akiteta na Ijumaa juzi jijini Dar es Salaam kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, mmoja miongoni mwa watu wa karibu wa mnenguaji huyo alisema kuwa, tangu kuandikwa kwa habari hiyo, shoga yake huyo amekuwa hana raha, huku akiona soni kama siyo aibu hata kutembea mitaani.

  Aliongeza kuwa, Aisha amekuwa akimweleza jinsi anavyoteseka kwa skendo hiyo lakini akaona uamuzi sahihi ni ‘kujificha’ kwanza kuacha hali itengemae kabla ya kujitokeza na kuwataka radhi mashabiki wake kwa kile kilichotokea.

  “Nimekuwa nikiongea naye mara kwa mara na kunieleza kuwa, anateseka kwa skendo hiyo lakini nikawa namtuliza kwa kumwambia kwamba, achukulie ni sehemu ya kujikwaa katika maisha, awe mvumilivu kwani hilo nalo litapita,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

  “Mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa mwishoni mwa mwezi uliopita na akaniambia kuwa, haoni sababu ya kuikacha fani yake ya unenguaji iliyompatia heshima kwa muda mrefu eti kwa sababu ya skendo, akanihakikishia kwamba, ipo siku atajitokeza na kuwaomba radhi watu wake.”

  Hata hivyo, mwanzoni mwa wiki hii gazeti hili lilitonywa kuwa, Bendi ya Twanga itakuwa ikifanya mazoezi katika Ukumbi mmoja uliopo Ofisi za ASET Vijana, Kinondoni na kwamba, Aisha Madinda atakuwepo pia.

  Mwandishi wetu alitinga eneo hilo majira ya saa 8:00 mchana na kufanikiwa kumtia machoni mnenguaji huyo lakini katika hali ya kusikitisha alionekana kudhoofika kiafya hali iliyoashiria kuwa, maombi ya mashabiki wake ndiyo yanayoweza kumrejesha katika hali yake ya zamani.

  Katika hali ya kushangaza, Mwandishi Wetu alipomsogelea kwa lengo la kutaka kufanya mahojiano naye mnenguaji huyo aligoma katakata huku akieleza kuwa, hawezi kusema chochote isipokuwa Mkurugenzi wake, Asha Baraka ndiye mwenye mamlaka hayo kwa sasa.

  “Mimi siwezi kuongea chochote, wewe kama unataka kupiga picha piga tani yako lakini usiniulize lolote kuhusu mimi, ongea na Mkurugenzi wangu,”alisema Aisha huku akiweka mapozi ya kila aina.

  Katika kupata kinachoendelea kuhusu mnenguaji huyo, Ijumaa lilimsogelea Asha Baraka ‘Iron Lady’ na kufanya naye ‘fesi tu fesi intavyu’ ambapo kwa maelezo yake alisema kuwa, wanakubali kuwa, Aisha aliteleza lakini wanaamini bado kuna kila sababu ya kumsamehe na kumwacha aendelee na maisha yake.

  Alisema kuwa, uongozi wa ASET hauwezi kumtenga mnenguaji huyo kwakuwa amefanya kazi na Bendi hiyo kwa muda mrefu na kuiletea mafanikio makubwa hivyo wana kila sababu ya kumpokea na kumwongoza katika misingi inayotakiwa.

  “Mimi kwa Aisha ni kama mama au dada yake, na ninavyojua, mtoto anapojisaidia kiganjani mzazi huwezi kuukata mkono bali utausafisha kisha kuyaacha mambo yaendelee. Vivyo hivyo kwa Aisha, kafanya kosa lakini hakuna kosa lisilostahili msamaha, kwahiyo asamehewe,” alisema kiongozi huyo na kuongeza:

  “Atakachokifanya Aisha ni kuwaomba radhi mashabiki wake na katika kila sehemu ambayo tutafanya shoo atafanya hivyo kabla ya kuanza kutumbuiza”.

  Aisha alikumbwa na skendo ya kupiga picha chafu na mchumba wake aliyefahamika kwa jina la Khumalo akiwa nchini Afrika Kusini kisha picha hizo kusambaa jijini Dar es Salaam.

  Hata hivyo, baada ya tukio hilo kuripotiwa, mnenguaji huyo aliingia mafichoni kabla ya juzi kuibuka na kuelezwa kuwa, ataendelea na kazi yake ya unenguaji katika bendi yake kama kawaida.

  Watanzania tusahau yaliyopita, tumsamehe Aisha na tumuombee kwa Mungu amuepushie mitihani katika maisha yake-Mhariri.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akionekana mwenye furaha baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Shree Hindu Mandal, jijini Dar es Salaam jana alikokuwa amelazwa tangu Ijumaa iliyopita kwa matibabu.  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Hindu Mandal, jijini Dar es Salaam, alikolazwa kwa siku sita, baada ya daktari aliyekuwa akimtibu, Dk. Ramaiya Kaosheki, kuridhishwa na maendeleo ya afya yake. Maalim Seif, ambaye alilazwa kutokana na matatizo ya shinikizo la damu na kifua, alitoka saa 4:00 asubuhi.
  Naibu Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Ashura Mustafa, alisema jana kuwa baada ya kutoka hospitali, Maalim Seif anatarajiwa kuendelea na shughuli zake za kawaida muda mchache ujao.
  Maalim Seif, aliugua ghafla wakati akijiandaa kupanda ndege kwenda Mascut, Oman, Ijumaa wiki iliyopita.
  Afya yake ilianza kuzorota ghafla muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndega wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Zanzibar.
  Maalim Seif alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya afya yake kubadilika ghafla.  CHANZO: NIPASHE
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Dk. Mwinyi Haji Makame.  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imependekeza sheria mpya ambayo itafuta uwezo wa mahakama kukamata mali za Serikali na kupigwa mnada pale Serikali inaposhindwa kutekeleza hukumu za mahakama katika muda mwafaka.
  Naibu Msaidizi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Saleh Said Mubarak, amesema muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyi Haji Makame.
  Alisema muswada huo utaweka utaratibu wa namna ya kuishtaki Serikali na mahakama za Zanzibar kutokuwa na nafasi za kukamata mali za Serikali pale inaposhtakiwa na kushindwa kutekeleza hukumu kwa muda muafaka.
  “Mahakama hazitokuwa na uwezo tena wa kukamata mali za Serikali pale Idara yoyote ya Serikali inaposhtakiwa na kushindwa kesi na badala yake madai yote yatalipwa kupitia Mfuko wa Hazina wa Serikali,” alisema. Alisema tayari muswada huo umeshapitishwa na Baraza la Mapinduzi na unatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachotarajia kuanza Machi 24 mwaka huu.
  Chini ya sheria hiyo, ni marufuku mali za SMZ au vitu vinavyotoa huduma kwa umma au viongozi wa Serikali kukamtwa na kupigwa mnada kwa amri ya mahakama.  CHANZO: NIPASHE
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).  Magari 746 zikiwemo daladala 594 za jijini Dar es Salaam na mabasi 152 ya mikoani yapo hatarini kufutiwa leseni za usafirishaji kutokana na kukaidi kulipa faini ya makosa ya usalama barabarani.
  Magari hayo yalikaidi kulipa faini hiyo wakati wa zoezi la kuyakagua lililokuwa likiendeshwa na kampuni ya Majembe Auction Mart.
  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imewatahadharisha wamiliki wa magari hayo kulipa faini wanazodaiwa ndani ya siku saba zijazo na kwamba baada ya muda huo kumalizika, yatafutiwa leseni na hayatapewa leseni kokote Tanzania Bara hadi hapo watakapolipa faini hizo.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Meneja na Usalama wa Sumatra, Aaron Kisaka, alisema kazi ya usimamizi wa usafiri mkoani Dar es Salaam na mabasi ya masafa marefu ambayo ilianza kufanywa na kampuni ya Majembe Desemba mwaka jana, ilibaini baadhi ya madereva kukiuka masharti ya leseni zao na kusababisha kutozwa faini.
  Alisema kwa Januari pekee, kampuni ya Majembe ilikamata daladala 494 ambapo 176 kati ya hizo hazijalipa faini hadi sasa.
  Alisema Februari daladala 691 zilikamatwa na kwamba 418 kati ya hizo zimekaidi kulipa faini, wakati mabasi ya mikoani ambayo yalikamatwa kwa kipindi hicho ni 174, kati yake 152 hayajalipa faini.
  Alisema mabasi hayo yalibainika kufanya makosa mbalimbali na madereva wa magari hayo walikubali makosa yao kwa kusaini fomu za adhabu kulingana na kosa husika.
  “Baada ya ufuatiliaji wa mabasi yaliyofanya makosa hayo, mamlaka imebaini kuwa kuna baadhi ya wamiliki wamekuwa wakikaidi kulipa faini walizoandikiwa kwa mujibu wa fomu ya adhabu walizosaini na kukubali makosa waliyofanya,” alisema Kisaka na kuongeza kuwa:
  “Kutokana na hali hiyo, mamlaka inawaagiza wamiliki wote wa mabasi walioandikiwa adhabu kulipa faini hizo ndani ya siku saba kuanzia Machi 12, mwaka huu (leo) watakaokiuka watafutiwa leseni zao.”
  Aliwaonya wamiliki ambao wametorosha magari yao baada ya madereva wao kukataa kutoa ushirikiano kwa kampuni ya Majembe kuwa hawatapewa leseni ya usafirishaji mkoa wowote nchini.
  “Nitoe tu angalizo kwa wanaokusudia kununua gari la abiria ambalo limekuwa likitoa huduma ya usafiri nchini, nawashauri kuwasiliana na mamlaka ili kuhakiki iwapo gari hilo halijafungiwa kutoa huduma ya usafirishaji kwa kushindwa kulipa faini kwa sababu watakaonunua mabasi yaliyofungiwa watalazimika kulipa kwanza faini hizo kabla ya kupewa leseni,” alisema.
  Hata hivyo, Kisaka hakutaja kiasi cha faini ambacho kinadaiwa kwa magari hayo na badala yake alisema faini zilikuwa kuanzia Sh. 100,000 hadi 250,000 kulingana na aina ya kosa.
  Hata hivyo, inakadiriwa kuwa magari hayo yanadaiwa zaidi ya Sh. milioni 130.
  Desemba mwaka jana, Sumatra iliiteua Kampuni ya Majembe Auction Mart kufanya kazi ya kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa utekelezaji wa masharti ya leseni za usafirishaji kwa mabasi ya abiria jijini Dar es Salaam na yale ya mikoani kazi ambayo itafanywa kwa mwaka mmoja kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani.  CHANZO: NIPASHE
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  Na Mwandishi Wetu
  Ni skandali nyingine yenye uzani mkubwa kuzunguka Kanisa hususan kwa waumini wenye mlengo wa kilokole, baada ya kuibuka kwa tuhuma kwamba baadhi ya watumishi wa kiroho wanazitumia nafasi zao kupata pumziko la ngono kutoka kwa waumini wao...
  Gazeti ‘5 Star’ kwa habari za mastaa, Risasi Jumamosi lina ‘data’ za kiuchunguzi, malalamiko kutoka kwa waathirika pamoja na nukuu za wachungaji wanaothibitisha kuwepo kwa ‘kamchezo hako’ na kuwanyooshea vidole baadhi ya watumishi wenzao kwamba wanahusika.

  Kwa mujibu wa uchunguzi wetu pamoja na kauli za waathirika, baadhi ya watumishi wa kiroho wakiwemo Maaskofu, Wachungaji na Mitume wamekuwa wakiwageuza katuni waumini wao wa kike na kufanya nao mapenzi bila ridhaa yao kwa kuwafanyia ibada maalumu ya kupokea a.k.a Deliverance.

  Uchunguzi unabainisha kwamba, watumishi hao huku wakitambua dhima waliyonayo katika kulipa afya neno la Mungu, huingia katika mtego wa dhambi kwa kuwarubuni waumini wao wanaofika mbele yao, madhabahuni wakitaka huduma.
  Mmoja wa waumini ambao wamewahi kukumbwa na balaa la Deliverance (delivarensi) aliyejitambulisha kwa jina moja la Sophia, aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa, alifika kwenye moja ya makanisa yenye mlengo wa kilokole, yaliyopo Wilayani Kinondoni, Dar na kujikuta mikononi mwa mtumishi mmoja maarufu.

  Muumini huyo alisema kuwa, alikwenda kanisani hapo kwa lengo la kufanya sala ya toba lakini mchungaji huyo alipokuwa akimfanyia usaili, aliingiwa udenda juu yake, hivyo akamchomekea kuhusu huduma ya delivarensi.
  “Aliniambia nina dhambi nyingi, kwahiyo roho wa bwana amemwambia nahitaji sala ya kupokea, yaani delivarensi. Nikamwambia mchungaji mimi nipo tayari, akanijibu kama ndivyo basi huduma hiyo lazima ifanyike usiku katika mazingira ambayo sijayazoea.

  “Nilifikiri angeniambia kanisani lakini haikuwa hivyo, aliniambia nikapange chumba hoteli, halafu nimtaarifu. Nikamjibu sina pesa za kupanga chumba, yeye akaniambia mtumishi wa Mungu yupo, akatoa shilingi 100,000 akanipa,” alisema muumini huyo.

  Aliendelea kusema: “Nilipanga chumba hoteli (jina tunaliminya) kisha nikamtaarifu, akaniambia nioge vizuri ili niwe safi kwa ajili ya kupokea. Akanisisitiza kuwa baada ya kuwa safi nisivae nguo yoyote zaidi ya kanga moja mpya. Nami nikatii.

  “Saa nne usiku mchungaji alifika hotelini hapo, mwanzoni akawa anaongea kwa kukemea mapepo yaniondoke, baadaye sauti ikawa inashuka, akawa ananisugua mgongo kama ananifanyia ‘masaji’, nilipohoji akaniambia hiyo ni sehemu ya ibada ya delivarensi.

  “Aliendelea kunisugua, akaniondoa kanga nikabaki bila nguo, akanisukumia kitandani. Nilipomuuliza akasema na yeye ni binadamu kama mimi, kwahiyo anaweza kuanguka dhambini lakini atatubu, akaning’ang’ania mpaka akatimiza haja zake.”

  Hata hivyo, jina la mtumishi huyo wa kiroho mwenye ‘taito’ kubwa na waumini ‘wa kumwaga’, linabaki kwenye kuta za Risasi Jumamosi kwa sababu maalum.

  Mbali na muumini huyo, gazeti hili lina maelezo ya kondoo mwingine ambaye lawama zake anazielekeza kwa mchungaji huyo huyo kuwa naye alimfanyia ‘spesho delivarensi’ kwenye gesti moja iliyopo Kinondoni.

  Muumini huyo aliliambia gazeti hili kuwa, alikwenda kwenye kanisa la mchungaji huyo akiwa na mchumba wake kwa lengo la kutaka baraka za kiroho kabla ya kuamua kufunga ndoa.

  “Tulipofika pale Mchungaji … (anamtaja jina) akaniambia mimi nilikuwa na tatizo la ndani ambalo lingesababisha ndoa yangu isidumu. Tukamuuliza cha kufanya akasema ni lazima nipokee sala ya delivarensi.

  “Akaniambia nipange chumba hoteli, niwe peke yangu halafu yeye atashirikiana na mimi kufanya delivarensi. Sikuwa na pesa yeye akanipa lakini usiku nikiwa chumbani alikuja, akanizuga mpaka tukafanya mapenzi, hiyo ilinikera sana.

  Gazeti hili, pia lina ‘eksheni’ ya mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili (jina tunalo) ambaye naye aliingizwa ‘mkenge’ na kufanyiwa delivarensi kwenye gesti moja iliyopo Kwaremi Sinza, jijini Dar es Salaam.

  Habari zinasema kuwa, mwanamuziki huyo akiwa anasindikizwa na msaanii mwingine wa nyimbo za Mungu mwenye jina kubwa pia, alikwenda kanisani kwa mchungaji mmoja (naye anahifadhiwa) kwa ajili ya kufanya sala ya toba.

  Chanzo chetu kinasema kuwa, baada ya mwanamuziki huyo kuzungumza na mchungaji, walikubaliana kwenda kufanya ibada ya delivarensi kwenye gesti hiyo.

  “Wakati mchungaji na … (anataja jina la mwanamuziki) wapo chumbani gesti, huyo mwanamuziki mwenzake alikuwa anamsubiria kwa nje,” alisema mtoa habari wetu.

  Katika moja ya mahubiri yake, Askofu Mkuu wa Full Gospel & Bible Fellowship, Zakaria Kakobe aliwahi kukemea tabia ya baadhi ya watumishi wa Mungu kwenda kuwafanyia maombi waumini kwenye vyumba vya peke yao.

  Alisema kuwa, mtindo huo unaondoa utakatifu na kubakiza maswali yenye utata kujibika, akisisitiza kuwa, usafi daima ndiyo unaolinda ukristo.

  Aidha, Kakobe aliwahi kusema ifike mahali makanisa ya kilokole yafe na kubaki makanisa yanayohubiri wokovu.
  Mchungaji Daniel Rashid Gingo, alisema kuwa, wakristo wengi wamesahau kusoma Biblia na kuwaamini manabii ambao wengi wao ni wa uongo tofauti na mafundisho ya Yesu Kristo.

  “Wakristo wengi wamesahau Biblia, ndiyo maana wanakumbwa na udanganyifu wa delivarensi na baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu, wengine wanafikia kuuziwa kipande cha sabuni shilingi 10,000 kwa kuambiwa kina upako wakati kipande hicho dukani ni shilingi mia moja,” alisema Gingo.

  Gingo ambaye pia ni mwandishi wa kitabu cha Wakristo Msidanganyike, aliendelea kusema: “Ninachoomba Wakristo wenzangu tukae chini na kusoma Biblia, mimi naamini wewe mwenyewe ukifunga na kuomba kwa Mungu wako basi utapona ili mradi uwe umemkubali Muumba wako, tuachane na utapeli wa manabii waongo.”

  Wakati Mchungaji huyo akisema hayo, Askofu wa Huduma ya Neno la Upatanisho lililopo Kitunda Bustani ya Edeni (Matembele ya Kwanza Kivule), Nicolaus Suguye naye alikiri kuwa, baadhi ya watumishi wa Mungu wamekuwa wakifanya mambo yasiyompendeza Muumba wao.

  Suguye alisema kuwa, leo hii baadhi ya watumishi wamekuwa wakitoa unabii wa uongo kwa kutumia msemo wa ‘Roho wa Bwana amesema’ na kulaghai waumini wao na kujikuta wanaanguka katika dhambi ya uzinzi.

  Mpakwa mafuta huyo wa Mungu aliwaomba watumishi wa kweli kusimama imara na kuwaombea watumishi wanaofanya mambo hayo maeneo ambayo si mazingira ya uwazi la sivyo Tanzania itaingia kwenye janga baya ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii.
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, kimemwomba Rais Jakaya Kikwete kuifuta Bodi ya Pamba nchini kwa kile kilichoelezwa kuwa haiwasaidii wakulima wa zao la pamba.
  Ombi hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, katika kikao cha viongozi wa serikali na CCM wa mkoa huo, kuhimiza mpango wa kilimo kwanza katika wilaya ya Maswa.
  Alisema Bodi ya Pamba nchini imekuwa haisimamii uendelezaji wa zao hilo, hivyo kumfanya mkulima wa zao hilo kuendelea kulima kienyeji hali ambayo imekuwa haimkwamui kiuchumi.
  Alidai kuwa Bodi ya Pamba imeacha wajibu wake kama ilivyokuwa zamani wa kusimamia uzalishaji na usambaji wa mbegu na pembejeo kwa wakulima wa zao hilo kwa wakati, jambo ambalo hivi sasa halifanyiki.
  “Tunamwomba Rais afute bodi hii ama iboreshwe zaidi, maana hakuna kazi wanayoifanya kwa wakulima wetu, zamani ilikuwa ndiyo inasimamia uandaaji wa mbegu zinazostahili kupandwa kwa kanda fulani, lakini sasa hivi wameweka mawakala ambao ni wanunuzi wa pamba kutoka kanda zote na kuzichambua bila kuzitenganisha” alisema.
  Alieleza kuwa sasa mashamba mengi ya zao la pamba mimea yake imekuwa ikishambuliwa na wadudu hali ambayo inafanya uzalishaji wake kuwa mdogo, hivyo kusababisha pato la mkulima kuwa la chini na kuendelea kuwa masikini.
  Aliwataka maafisa ugani wawe karibu na wakulima kwa ajili ya kuwapatia ushauri unaotakiwa kwa wakati, kuanzia kipindi cha kuandaa mashamba hadi kupanda sambamba na kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati.
  “Ni vizuri maafisa ugani wetu hasa walioko maeneo ya vijijini ambako ndiko wakulima wengi wanapatikana wakawa karibu nao kwa ajili ya kuwapatia ushauri unaotakiwa kuanzia wakati wa kuandaa mashamba hadi kipindi cha upandaji, jambo hilo liwe sambamba na kuwafikishia pembejeo kwa wakati” alisisitiza.
  Zao la pamba limekuwa likishuka kwa ubora kila mwaka jambo ambalo linaelezwa limesababishwa na kutosimamiwa na Bodi ya Pamba, hali ambayo inawafanya baadhi ya wakulima kutolima na kutafuta zao mbadala la kibiashara mkoani Shinyanga.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Mtera (CCM), John Malecela.  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepanga kuelekeza mashambulizi yake ya operesheni Sangara mkoani Dodoma, na safari hii kimeahidi kumg’oa Mbunge wa Mtera (CCM), John Malecela.
  Kamanda atakayeongoza operesheni hiyo, John Mrema, alisema jana kuwa kama kawaida chama hicho kitakuwa kikipasua anga kwa usafiri wake wa kawaida (helikopta).
  Alisema Mkoa wa Dodoma haujawahi kuwa na mbunge kutoka vyama vya upinzani na kwamba wanatarajia wa kwanza atatoa jimbo la Mtera.
  Malecela mwenyewe bado hajaweka wazi msimamo wake iwapo atagombea tena au atapumzika.
  Mrema alisema operesheni hiyo itadumu kwa siku 10 na kwamba wanatarajia kuvuna idadi kubwa ya wanachama kama ambavyo walivuna katika operesheni za Mkoa wa Kagera na Tanga.
  “Mzee Malecela ajue tunaenda Dodoma na jimboni kwake tutafanya kazi kubwa kata zote kuhakikisha mgombea wetu katika uchaguzi wa mwaka huu ananyakua jimbo,” alisema Mrema.
  Mrema alisema operesheni hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Slaa.
  Alisema Dodoma ni mkoa muhimu lakini chama hicho hakikuwahi kufanya kazi kubwa ya kukijenga lakini safari hii wamemua kufanya kweli.
  Alisema mkoa huo ukipata viongozi wazuri ni rahisi kusonga mbele kwani mazingira yake ni mazuri na unarasilimali za kutosha.
  Alisema wanatarajia kufanya mkutano wa uzinduzi Jumatatu mjini Dodoma na kesho yake wataanza rasmi operesheni sangara maeneo ya mjini. Alisema wanatarajia kufanya operesheni hiyo katika majimbo yote tisa ya mkoa huo na kwamba wanatarajia kusimamisha wagombea wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
  “Tunaomba wananchi wa Dodoma watupokee na watusikilize kwa makini maana tunawapelekea sera nzuri na tunataka kuijenga Dodoma mpya na yenye neema,” alisema.  CHANZO: NIPASHE
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Wagombea wahaha kutafuta uungwaji mkono Mikusanyiko ya misiba, kidini, sherehe vyawa lulu Viti maalum nako hapatoshi...ni mchakamchaka
  Sasa hakulaliki, majimboni kunawaka moto. Hivi ndivyo unavyoweza kusema katika kipindi hiki cha lala salama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
  Hali ya wasiwasi kwa baadhi ya wabunge kurudi tena bungeni inazidi kuwa juu, huku wagombea wapya wakionekana kuwa na kiherehere cha kutaka nafasi hiyo ya uwakilishi.
  Mikusanyiko mbalimbali kama vile misiba, kidini, sherehe na ya kijamii, sasa imekuwa fursa adhimu kwa wagombea kujinadi na kutafuta ushawishi wa kuungwa mkono.
  Nguvu kubwa za kifedha na mikakati ya kisiasa, nayo imekuwa karata nyingine inayotumiwa kutafuta ushawishi kuungwa mkono.
  Ushindani mkubwa hauonekani tu katika nafasi za majimbo, bali kwa upande wa ubunge wa viti maalum nako kumekucha.
  Wanawake wa Chama cha Mapunduzi (CCM) wanaotaka kuwania ubunge, wanadaiwa 'kukabana' koo kutafuta ushawishi kwa wajumbe watakao wapigia kura, huku wale wa vyama vya upinzani hasa vyama vya Chadema na CUF nao wakitoana jasho kutafuta kupenya kwenye nafasi hizo.
  Uchunguzi uliofanywa na Nipashe Jumapili, umebaini kwamba kwenye majimbo harakati za wabunge wanaotaka kutetea nafasi zao na wale wanaotaka kuwaondoa kwenye nafasi hizo zinazidi kuongezeka kiasi kwamba hisia za uadui na kutazamana kwa jicho la husuda zimeenza kujichomoza mapema.
  Uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa mawaziri na manaibu mawaziri, wengi wao wapo roho juu, kutokana na kuhofia kukosa ubunge ambao ndiyo tiketi kubwa ya kukwaa uwaziri.
  Hii inatokana na kujitokeza kwa sura nyingi mpya kwenye majimbo yao, ambao wanaonekana kuwa na mvuto.
  Mawaziri wengi wanajikuta katika wakati mgumu kipindi hiki cha karibu na uchaguzi, kutokana na nyadhifa za kiserikali wanazoshikilia kuwaweka ‘bize’ kiasi cha kukosa muda wa kutosha kuwa karibu na majimbo yao, lakini sasa wanalazimika kurudi kwa wananchi kuomba kuchaguliwa tena.
  Lakini kazi kubwa ipo kwa mawaziri na manaibu ambao walizipata nafasi hizo kutokana na ubunge wa viti maalum. Hawa huenda baadhi yao wasirudi bungeni kutokana na nafasi za ubunge wa kuteuliwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi safari hii.
  Lakini baadhi yao wamesoma alama za nyakati, wameamua kujitosa kwenye majimbo kujaribu bahati yao baada ya kujiaminisha na kujiridhisha kuwa wanaweza kuhimili ushindani kwenye nafasi hizo za kuchaguliwa.
  Hali hiyo inaelezwa italeta ushindani wa aina yake kwenye majimbo na dalili zimeshanza kujionesha kuwa kutakuwa na ushindani utakaoleta mvuto wa aina yake kwenye uchaguzi wa safari hii.
  Jijini Dar es Salaam nako mambo si swari. Homa ya uchaguzi hasa kwenye nafasi ya ubunge inazidi kupanda kwa kiwango cha juu siku hadi siku.
  Homa hiyo imezidi kupanda hivi karibuni, baada ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, kutangaza uwezekano wa kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni huku Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akitarajiwa kugombea Jimbo la Kawe.
  Mbali na jimbo hilo Zitto amesema pia wananchi wa majimbo ya Geita, Kahama, Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini wote wanamhitaji ili awawakilishe.
  Hata hivyo, Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hadi sasa bado hajafanya uamuzi rasmi wa jimbo gani kati ya hayo atakwenda kugombea.
  Habari za Zitto kugombea Kinondoni ambako Iddi Azan wa CCM ndiye mbunge zimesababisha mshtuko kwa CCM wilayani humo na katika kuthibitisha hilo, hivi karibuni Umoja wa Vijana wa chama hicho wilayani humo, ulimuonya mbunge huyo kutojaribu kufanya hivyo kwani ataambulia patupu.
  Naye Mbatia alisema uamuzi wa kugombea katika Jimbo la Kawe unatokana na msingi wa kikatiba na haki ya kila Mtanzania ya kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi zozote.
  Kwa sasa Jimbo la Kawe linashikiliwa na mbunge wa CCM, Rita Mlaki. Hata hivyo, mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Halima Mdee naye alikwisha tangaza kwamba katika uchaguzi wa mwaka huu anawania jimbo hilo.
  Wakati hayo yakiendele, habari zinasema baadhi ya watu maarufu na wenye ushawishi wakiwemo baadhi ya mawaziri nao wanayamezea mate majimbo ya Dar es Salaam na wanachosubiri kwa sasa ni muda tu kuweka dhamira zao hadharani.
  Kwa upande mwingine, mivutano ya makundi ndani ya CCM inatarajia kuleta ushindani mkubwa miongoni mwa wagombea wa chama hicho.
  Uchunguzi wetu unabainisha kuwa karibu katika kila mikoa na hata katika majimbo mengi ya uchaguzi Tanzania Bara, CCM imegawanyika katika makundi.
  Inadaiwa kuwa katika baadhi ya majimbo wabunge wa sasa wa CCM wameandaliwa wapinzani kutoka katika makundi pinzani ndani ya chama hicho. Majimbo hayo yanatajwa kuwa ni Nzega mkoani Tabora, ambalo Mbunge wake ni Lucas Selelii na Lupa mkoani Mbeya, ambalo mbunge wake ni Victor Mwambalaswa.
  Mengine ni Kishapu ambako mbunge wake wa sasa ni Alfred Mpendazoe, Bumbuli mbunge wake wa sasa, William Shelukindo, Vunjo ambako mbunge wa sasa ni Aloyce Kimaro, Kyela ambako mbunge wake ni Dk. Harrison Mwakyembe na Urambo linaloshikiliwa na Samuel Sitta, ambaye ni Spika wa Bunge.
  Kindumbwendumbwe kingine kipo katika Jimbo la Ubungo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Charles Keenja, ambapo watu kadhaa tayari wameshatangaza kutaka kuwania nafasi hiyo akiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na Mkurugenzi wa Vijana wa Chadema, John Mnyika.
  Wengine walioonyesha nia ya kuwania jimbo hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Makete, Hawa Ng’umbi na Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kinondoni, Abdulkarim Atik.
  Pia kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutangaza kuwania ubunge wa Jimbo la Hai kunaelezwa kumuweka katika hali ngumu mbunge wa sasa, Fuya Kimbita, kutokana na kiongozi huyo wa Chadema kuonekana kuungwa mkono na wananchi wengi wa jimbo hilo.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...