Achilia mbali ruzuku na michango, CHADEMA ina vyanzo gani vya mapato?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Binafsi naamini kuwa chama cha siasa ni taasisi. Naamini hivyo pamoja na kutowahi maishani mwangu kujiunga na chama chochote cha siasa hapa Tanzania na kwingineko. Kama taasisi, chama hujiendesha kwa gharama.

Kuna kuwalipa waajiriwa wa chama, kugharimia shughuli za kila siku za chama,kugharimia ziara na operesheni za kichama na kadhalika. Taasisi hujiendesha katika hali ghali. Chama, ili kupambana na changamoto za kiuendeshaji na kisiasa, kinapaswa kuwa na vyanzo vya mapato

Kwa uelewa wangu, chama kama CCM kinamiliki mali mbalimbali kama majengo na viwanja vya mpira. Hizo pekee, ingawa kuna mengine, ni vyanzo vya mapato ya chama. Vipi kuhusu CHADEMA, kama chama kikuu cha upinzani nchini na taasisi muhimu kidemokrasia?

Achilia mbali ruzuku kwa vyama vya siasa na michango ya wanachama, wafuasi, wapenzi, wakereketwa, wafurukutwa na wafia chama, CHADEMA ina vyanzo gani vingine vya mapato? Ina mipango gani ya kujiimarisha kiuchumi?

Michango ya wanachama, hasa Wabunge wa CHADEMA, wakati mwingine ni mzigo na inakera. Ifike mahali CHADEMA iwe na vyanzo vyake vya mapato kama taasisi ili kujiimarisha na kuaminika. Ni kazi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA kusugua bongo

Aione: Tumaini Makene ,Mmawia na wengineo
 
Ili ugombee urais kupitia chadema lazima ununue nafasi hiyo. Mwenye kununua pesa nyingi ndiye anaruhusiwa kugombea nafasi hiyo. Nadhani mfano halisi unao.

Hivyo hicho ni 1wapo wa vyanzo vya mapato
 
Nina mashaka kama CCM inamiliki kihalali chochote kati ya hivyo vilivyotajwa kama vitegauchumi vya Chama . Ni sahihi kusema CCM ilijimilikisha mali zilizokuwa za watanzania wote na kuzifanya kuwa mali za chama. CCM kama chama, hakijawahi kujenga kiwanja chochote hata cha mpira wa pete...Tuacheni mambo ya political correctness tunapoamua kusema ukweli.
 
Kwani vibaya mtu kuhoji. Tusiwe wanafiki chama chochote cha siasa lazima kibuni mbinu za kujiendesha, sio kutegemea ruzuku na michango ya wanachama tu. Na ndio vyama vingi vinakufa taratibu kama UDP, TLP na sasa NCCR kwa sababu kutegemea ruzuku.
 
Petro E. Mselewa ,

..nadhani si busara kuruhusu vyama vya siasa kuwa na miradi ya kibiashara na vitega uchumi.

..tukiruhusu hilo kunaweza kutokea conflict of interest ambapo wabunge au viongozi wa vyama hivyo wakatunga sheria au kuweka mazingira ya kupendelea biashara ua vitega uchumi vyao.

..kwa maoni yangu itungwe sheria ya kudhibiti na kuhakiki mapato ya vyama vya siasa. Vyama vya siasa viendeshwe kwa RUZUKU na MICHANGO YA WANACHAMA. Hata michango nayo iwekewe limit ya kiasi ambacho mwanachama au taasisi inaweza kuchangia.

Nguruvi3
 
Mkuu si busara kabisa. CCM walijaribu katika kuwekeza na michango ya wafanyabiashara leo bado wanalipa gharama.
Chama kilipoteza umiliki, wakawepo wanaoweza kudhamini na ndio wenye sauti. Hili ni funzo la kwanza lililo hai

Huko nyuma akina Dosa Azizi na Mshume kwa mujibu wa Mohamed Said walichangia sana TANU
Nadhani dhamira ya wazee ilikuwa njema sana, kwabahati mbaya michango hiyo tunaona inavyotumiwa katika maandiko vibaya hadi kudhalilisha wanachama wengine. Nyerere hakuwa na mboga n.k.

Nadhani kujitolea, michango ya kawaida na jitihada nyingine binafsi ziwe msingi wa vyama vya siasa

Ninachoweza kukubaliana na Mselewa ni kujitangaza.
Miaka 20 hao Chadema hawana hata FM ya masaa machache!
 
Chanzo kingine ni kila wakifanya maandamano wanapata
ingizo jipya kwenye kibubu chao.

upload_2017-5-17_16-17-31.jpeg
 
Hahaha Unahoji Chama kipi Cdm!!
Watetezi wa majizi hao wasaka Tonge watakuwa na vyanzo vya mapato!!
Waulize kwanza hicho kidogo wakipatacho kinamchanuo gani!!
Utaiwa msaliti.
Mbowe na genge lake ndio Tatizo ndani ya cdm
pale hakuna viongozi ni wasaka tonge na wachumia Tumbo
 
Mkuu uko na hoja ya msingi sana ila umekosea sana kusema ccm wanamiliki viwanja, hivyo viwanja ni nguvu kazi ya taifa iliyotumika michango ya watu wote, hivyo ccm walitumia uharamia kuvichukua hivyo viwanja
huyu jamaa naheshimu sana mada zake ila leo kachemka..ccm ilipata vyote ilivyo navyo wakati wa chama kimoja..tena si kwa hiari...hawa wenzetu wa upinzani wanajitahidi kutoa mikononi mwao na ruzuku kidogo wanayopata..
tusifanye siasa ni chuki au majungu..unaweza kuwa ccm na mkeo akawa chadema na ni kawaida.
 
huyu jamaa naheshimu sana mada zake ila leo kachemka..ccm ilipata vyote ilivyo navyo wakati wa chama kimoja..tena si kwa hiari...hawa wenzetu wa upinzani wanajitahidi kutoa mikononi mwao na ruzuku kidogo wanayopata..
tusifanye siasa ni chuki au majungu..unaweza kuwa ccm na mkeo akawa chadema na ni kawaida.
Mkuu,umiliki ni umiliki. Uhalali au uharamu hutamkwa na sheria au mahakama.
 
Back
Top Bottom