Acheni wenye elimu zao walipwe mamilioni

Acheni wenye elimu zao walipwe mamilioni

Wenye wivu mzuri, akiona mwenzie anapata kipato kizuri kwa sababu ya kusoma na yeye anaenda kusoma!!
Wapo watu wengi wamesoma kuliko hata hao wanaolipwa milioni 50...lakini kwa kuwa hawakubahatika kujuana na mkubwa, wataishia kwenye milioni 7 tu. Na hao watu wanayo nafasi kwenye mashirika na taasisi za umma kama hao hao wanaolipwa. Ukitaka kutumia kigezo cha uzalishaji kwamba ndicho kipange nani analipwa kiasi gani unakuwa na akili kama za mkulu wetu wa zamani kidogo...ambaye ndiye huyo aliyekwenda kusomba 'rafiki zake' huko nje ya nchi eti waje wamsaidie 'kuendeleza' Tanzania kwa makubaliano ya malipo makubwa kulingana na standards za huko Ulaya na Marekani.

Si kila sekta inazalisha (directly), na hatuwezi kusema kuwa kwa kuwa huyu anashughulika na shirika au taasisi isiyozalisha basi hana umuhimu. Katika sekta ya umma, kila mtu ana mchango wake. Kama ingekuwa ni hivyo basi tungevunja shule zote maana hazizalishi. Hata hospitali tungebomoa maana ni huduma tu, na madaktari hawana umuhimu kwa mtazamo wenu maana hawazalishi, isipokuwa wafanyakazi wa shirika la nyumba ndio wana umuhimu kuliko walimu na madaktari...halafu tungeona mwisho wake. nahisi kwa mtazamo wenu tungepata maendeleo sana nchi nzima ikiwa TPDC, TRA na NHC...akili hizi zina matege.

Tusidanganyane, mtu kulipwa pesa nyingi US (kwa conversions za bongo) haimaanishi kwamba yeye ni exceptional. Ikumbukwe kwamba hata bartender au mhudumu supermarket US anaweza kuwa na kipato kikubwa kuliko hata profesa wa bongo...ni standard ya maisha ya huko. Walioko huko ughaibuni na wabaki huko huko maana malipo ya huku hayawezi kuwaridhisha kwa haki. na hata huo mchango wao si kwamba ni wa ajabu sana. nina hakika wapo wengi wenye uwezo huo. Ni nia tu na dhamira imekosekana kuiendeleza nchi hii maana kila mmoja anataka atafune tu provided meno anayo.
 
Mkuu naomba kujua hii Open Uni of Dar Iko wapi, kwani nataka nijiunge nacho mwakani! Thanks!
Hapa tujadili concepts mbili kuu. 1.) Open University of Dar es salaam (duniani zipo open universities nyingi) .
 
TZS 15,000,000.00
-free house
-usafiri
-matibabu
-Posho kiasi
Hataki aende UN akaombe kazi huyo hatufai kuwa mtumishi wa Umma tena kwa nchi ambayo watu wanashindia mlo mmoja kwa siku

Mawazo ya kimasikini hayo!
Nani kasema ni UN tu ndio wanaoweza kulipa huo mshahara?!
 
Ujinga nikitu mbaya Sana. Mleta mada Prof Udsm analipwa ngapi? Achen ujinga ujinga tafuten kaz zakufanya sio kuja potosha umma. Kama Prof Udsm apati 40m! Naomba tuache serikal ifanye kaz yake asie taka aende akatafute kaz nje sisi tutasonga mbele nawatarud kupiga magoti kuomba kaz hapa.


Daaaah, umenifikisha nilipokua napatafuta.
Kama great thinker umejibu maswali yangu yote.

Kupanga ni kuchagua.
Kama mtu anaona huko nje kuna mshahara mkubwa basi aende huko.
Huko nje maisha yako juu pia. Huko huwezi kununua shamba ekari moja kwa laki moja kama hapa Tanzania.

Na pia nashauri kuwa kama mtu anaona kuwa yeye ni mahiri sana wa kusimamia kampuni basi aanzishe la kwake mwenyewe sio kusubiri KUTEULIWA kwenye mashirika ya umma.
Mtu anateuliwa bila hata kushindanishwa kwenye shirika la umma halafu anatupangia mshahara kisa kasoma nje ya nchi!!

Hapa ndipo wapinzani wa Magufuli wanapopoteza sifa ya kuwa na mawazo mbadala.
Nchi maskini kama hii huwezi kumlipa mtumishi mmoja mabilioni ya fedha halafu utegemee kujenga nchi ya watu waadilifu. Cha ajabu unamkuta mtu kama huyo hakuna cha ajabu anachofanya zaidi ya kuwanufaisha hao mabwana zake waliomlea huko ulaya kwa kuwasaidia kufanikisha mikataba ya kinyonyaji.

Na mara nyingi hawa wasomi waliosomea sana ulaya ni maajenti wazuri wa kuuza nchi zetu kwa fikra zao za kuona kila aliyetoka ulaya ni bora zaidi na ana elimu zaidi.
Wakati wa Nyerere waliomwangusha na kuua mashirika ya umma ni wale wale waliokua wamesoma huko nje.

Kila sekta ya umma ina umuhimu wake kwenye jamii kwa hiyo inapotokea kiongozi anakubali kuona kiongozi wa sekta moja ni ya muhimu zaidi basi ujue anatengeneza taifa la wezi.
Mfano Mkuu wa Majeshi anayeongoza taasisi kubwa kama jeshi yenye kila aina ya miradi halafu mshahara wake unazidiwa mara kumi na mtu anayeongoza shirika moja tu la nyumba ni ujinga mtupu.
Chini ya Jeshi kuna miradi mingi sana ikiwemo hiyo ya kujenga nyumba bure na kwa biashara.
Sasa itakuaje mkuu wa majeshi naye akataka kulipwa milioni hata mia? Maana huyu naye ni mteule wa Rais.Na kama ni kusoma kwenye medani za kijeshi amebobea katika fani hiyo na nyinginezo.

Kwa mawazo ya mleta mada Magufuli atawakimbiza sana.Wenye nchi wamemwelewa sana.
Nchi itajengwa na wenye moyo. Wenzetu hao wa huko nje walipitia kwenye nyakati za hata kuwatumikisha watu bure na ndio maana wakafikia hapo walipo. Hatutaweza kusonga mbele kama fedha za kuboresha elimu ya mtanzania tutaendelea kuwalimbikizia watu wachache kwa sababu tu wamesomea ulaya.

Ni lazima kwanza tujenge taifa lenye uwezo wa kumuelimisha mtanzania kwanza ili kuvumbua kipaji cha kila mtu. Hata huko ulaya sio kweli kwamba matajiri ni wale waliosoma kwenye vyuo alivyotaja mlete mada.

Kwa maisha ya kitanzania yenye fursa lukuku hata mil. 15 bado ni nyingi. Soko ni lile lile la yule anayelipwa laki 3.Mfanyakazi wa ndani elfu 50 ,mlizi wa nyumba unamlipa laki moja,shamba boy 60. Hapo unamlipa mtu mil. 40 ili iweje?

Kwa hili hongera sana Rais wetu. Timiza ndoto zako kwa taifa letu kwa vitendo.
 
Atakuambia milioni 9 kama Magufuli.

Mtu huwezi kuendesha taasisi yenye kutengeneza mabilioni ya shilingi halafu umlipe milion 15.

Huko ni kuchochea wizi.

Acha unyumbu. NSSF au PPF kazi yao ni kukusanya tu toka kwa wafanyakazi wanyonge na kubuni formula kandamizi kwa Mafao ya kustaafu huku pesa nyingi za wanachama zikitumika ndivyo sivyo, leo uniambie eti MA CEO wao wanastahili kulipwa milioni 40,000,000 kwa lipi ?
 
Kusoma xana sio kwenda oxford hao wanaolipwa mil 40 nina uhakika tungesoma chuo au darasa moja ningewaacha mbali acha uvivu wa kufikiri au hao wanaochukua mil 4o n tanzania one au


Ni kweli kabisa. Hao waliosoma huko ulaya waliporudi Tanzania na kukabidhiwa majukumu jambo la kwanza waliua Elimu yetu ya kujitegemea. Ndio maana wanapotoka ulaya wanawaza kuajiriwa zaidi tena kwa fedha nyingi badala ya kujiajiri na wao kuwa mfano wa kulipa mishahara minono.
Waliua elimu yetu na kujenga shule zao binafsi za gharama kubwa kama biashara zao.

Waliishaurai serikali ipunguze nafasi za kutoa scholarship za kuwasomesha watoto wa maskini wenye akili na badala yake wakatuwekea sheria za kujigharamikia kwenye elimu kwa sababu wao wanalipwa mishahara mikubwa watawasomesha watoto wao ulaya kwenye vyuo vya ghali ili tena baadae waje kututisha na vyeti vya Oxford university na kudai mishahara mikubwa ya mamilioni kama baba zao. Wafanyakazi wa chini wakiandamana kudai nyongeza ya mishahara hao hao wanakuja na kauli ya kusema mshahara mkubwa sio utatuzi wa matatizo kazini na kwenye jamii kwani utaongeza mfumuko wa bei.

Pongezi kwa mh Magufuli kwa kufyeka mishahara ya wafanyakazi wa umma wanaolipwa mamilioni kwa kodi za wanyonge. Pesa zinazookolewa zitumike kuwasomesha watoto wa kitanzania wenye uwezo na waliokosa fursa ili tupate Wasomi wa kweli wa kuijenga nchi yetu.
 
Acha unyumbu. NSSF au PPF kazi yao ni kukusanya tu toka kwa wafanyakazi wanyonge na kubuni formula kandamizi kwa Mafao ya kustaafu huku pesa nyingi za wanachama zikitumika ndivyo sivyo, leo uniambie eti MA CEO wao wanastahili kulipwa milioni 40,000,000 kwa lipi ?

Hujui unaloongea.
 
Atakuambia milioni 9 kama Magufuli.

Mtu huwezi kuendesha taasisi yenye kutengeneza mabilioni ya shilingi halafu umlipe milion 15.

Huko ni kuchochea wizi.


Anazitengeneza kutoka wapi?
Zile ni hela za wafanyakazi wanyonge walizowekeza tena kwa kulazimishwa na sheria.
Kwa nini yeye anataka alipwe Mabilioni wakati ameteuliwa tu?
Mbona hii nchi ina wasomi wengi sana kama hao tatizo ni kwamba hawana wakubwa wanaowafahamu katika ngazi za uteuzi?

Kila serikali inayoingia Madarakani inakuja na kundi la watu wake katika kuendeaha sekta mbali mbali. Kwa hiyo kama serikali inayoingia hauna ukaribu nayo ujue kuwa huwezi kupata nafasi za uteuzi labda upigiwe debe na IMF.

Tunachokataa ni shirika la umma ambalo limeanzishwa na serikali kwa kodi za wananchi kutumika kumtajirisha mtu mmoja.
Ambaye kimsingi tunamwona huko maofisini akiwa anafanyiwa kila kitu na watu wa chini yake tena wa kawaida tu. Akitoka ni kukesha bar na vimada mana hana hata muda wa kusoma zaidi hata kwenye mitandao. Walioko chini ndio wanahaha kusoma zaidi. Tofauti na shirika binafsi ambalo unapokabidhiwa inabidi uwe ndio kama mwenye shirika likiyumba kidogo unakosa kazi.
Ndio maana huwezi kumwona meneja wa shirika binafsi hata kama analipwa milioni 60 ana kitambi cha bia na kitimoto. Anapasua kichwa sana kuendeleza kampuni mana ndipo atakapoliwa kulingana na faida kubwa anayotengeneza.
Tofauti na shirika la umma linapopata hasara bado serikali inatoa ruzuko toka kwenye kodi ya wanyonge na kuimarisha shirika hilo.
 
Kamtafute mwenye CFA (chartered financial analyst) katika hao wanaolipwa 40mil. Ukimpata nna zawad yako
 
Una ushahidi ameipunguza au siasa za kwenye majukwaa zinakuhadaisha??? Kwanza kabisa hajaoridhesha hao mabosi na vitengo vyao wanaolipwa hiyo mishahara, alisema atashusha mpaka 15,000,000 but are you really really sure it wasn't politics??? Kuongea ni jambo moja, kutekeleza ni jambo lingine, ulikuwa unamjua anayelipwa mshahara wa 40,000,000??? Na hata Sasa unaweza kunitajia ni bosi wa kitengo gani analipwa mshahara huo??? Je iwapo kuna mtu yupo kwenye kitengo analipwa 100,000,000 halafu ikapigwa kimya na raisi akakaushia utajua kuhusu hilo????
Nikiwa mwanasiasa naweza kusimama tu nikasema katika nchi yetu kuna watu wanalipwa forty millions per month ila nitaishusha mpaka fifteen millions 'Pwapwapwapwapwa' ni makofi ya wananchi hayo but simply nimetumia common sense kuwakamata
Wake up my brothers and sisters
 
Usome kwa malengo. Kama unasoma tu ili upate digrii unaweza kulia. Kwanza soma kwa lengo la kujiari na pia soma fani ambayo utauzika. Sasa wewe unakwenda chuo kikuu kusoma historia na maigizo, unataka uajiriwe na nani hata kama utatoka na first class?
Acha dharau basi
 
Unakuta watu wamekaa wanafurahia eti haiwezekani mtu apokee mil.40 halafu mwalimu laki tatu , ukimuuliza huyo mtumishi ametumia gharama gani kupata taaluma yake utakuta kalipa ada mil. Moja na laki tano kwa mwaka mwenzako unayemlalamikia kalipa ada mil.

Hamsini kwa mwaka tena kasoma oxford, havard nk. Vyuo vinavyotambulika ulimwenguni , Popote anaajirika ulimwenguni. Ukimpa organization aiendeshe inakuwa efficiently and effectively. Mtu unamkuta kasoma open univers. Kutwa anasoma past paper hiyo competence ataitoa wapi .

Acheni wivu.
Hii awamu
 
Hapa tujadili concepts mbili kuu. 1.) Leadership: je? ni kweli kwamba kama umesoma Harvard, basi wewe unaweza uongozi; kama ukisoma Open University of Dar es salaam (duniani zipo open universities nyingi) au hata University of Dar es Salaam, basi wewe huwezi uongozi. 2.) ni concept ya equity katika payment of benefits ktk organization (chukulia organization ni utumishi wa umma) Je kuna equity kweli kiongozi mmoja wa juu alipwe Tshs 40,000,000/= pm peke yake halafu msaidizi anayemfuata Tshs. 4,000,000/= pm. Hivyo sio suala la wivu, ni suala la kuangalia equity. Vile vile sio suala kwamba kwa vile umesoma katika shule za ghali nje ya nchi basi unafaa kuwa kiongozi. Wengi wa hao wanaolipwa mamilioni "inasemekana" hawana kabisa leadership skills, ingawa ni wazuri sana wa kufanya kazi na media.
Tena kuna wale wanaosoma kwa pesa za serikali huku wakipata stahiki zao zote
 
Unakuta watu wamekaa wanafurahia eti haiwezekani mtu apokee mil.40 halafu mwalimu laki tatu , ukimuuliza huyo mtumishi ametumia gharama gani kupata taaluma yake utakuta kalipa ada mil. Moja na laki tano kwa mwaka mwenzako unayemlalamikia kalipa ada mil.

Hamsini kwa mwaka tena kasoma oxford, havard nk. Vyuo vinavyotambulika ulimwenguni , Popote anaajirika ulimwenguni. Ukimpa organization aiendeshe inakuwa efficiently and effectively. Mtu unamkuta kasoma open univers. Kutwa anasoma past paper hiyo competence ataitoa wapi .

Acheni wivu.
Umeanza vizuri lakini mwishoni umeharibu..inaonyesha kumbe na wewe ni mjinga tu..kwani open university wanasoma bure?Kuchukua masters expenses zake si zinaweza kufika hata mil 10?Wewe ulitaka kila mtu akitaka kusoma lazima akakae chuo ndio kusoma?Eti ukisoma open huwezi kuwa compitent,kwani makazini wanafanya mitihani au wanaaply born skills wakisaidiwa na logic inayotokana na elimu yako? Kwanza lazima ujue wanaoshangilia watu mishahara ishushwe wala sio wasomi wa open university,ni wale ambao hawajaenda shule kabisa..ndo wanataka 'tukose wote',jipange upya uje ulete mada yenye mashiko hapa..
 
Umeanza vizuri lakini mwishoni umeharibu..inaonyesha kumbe na wewe ni mjinga tu..kwani open university wanasoma bure?Kuchukua masters expenses zake si zinaweza kufika hata mil 10?Wewe ulitaka kila mtu akitaka kusoma lazima akakae chuo ndio kusoma?Eti ukisoma open huwezi kuwa compitent,kwani makazini wanafanya mitihani au wanaaply born skills wakisaidiwa na logic inayotokana na elimu yako? Kwanza lazima ujue wanaoshangilia watu mishahara ishushwe wala sio wasomi wa open university,ni wale ambao hawajaenda shule kabisa..ndo wanataka 'tukose wote',jipange upya uje ulete mada yenye mashiko hapa..
Msaada tutani Masters gani ya Open au chuo chochote Tanzania hii inafikia Million 10????
 
Msaada tutani Masters gani ya Open au chuo chochote Tanzania hii inafikia Million 10????
Mi nazungumzia gharama zako zote kwa ujumla utakazokuwa unaingia wakati unasoma..sizungumzii ada hapa.After all sijasema zinafika milioni kumi...nimeandika 'zinaweza kufika',hapo inaweza kuwa milioni 8,9...kutegemea na course na gharama zako binafsi kukamilisha hiyo kozi.Wabongo bwana...wanataka kunilisha maneno hapahapa hata maandishi hayajafutika
 
Elimu yenyewe ndio ile unaipata Kwa stress na tension. Ukiwa chuo malectures wao ndio wanajiona Mungu watu, mtu anakuambia akikushika huchomoi na hapo ni kabachelor, ilija masters ndio issue, uje PhD au level nyingine yoyote shughuli yake usiombe, mtu ukifaulu unashangilia na kurukaruka as if imekuwa ni bahati kupass. Unatoka hapo unaenda kazini unategemea kweli kusiwe na reward of all efforts na cost mtu alizotumia kupata elimu yake? Acha walipwe as long as they deliver what we are expecting of them to deliver with their education
 
Back
Top Bottom