Hii ina maana kwamba, ili kufikia mafanikio ya juu katika familia, mwanamume anapaswa kufunga mdomo, kwani majibu mengi anayo mwanamke. Kwa wanaume ambao hawako tayari kuwasikiliza wanawake au kuwaacha wanawake kuwa wazungumzaji wakuu kwenye masuala ya nyumbani na familia, wanapata hasara kubwa. Ni hasara inayotokana na ukweli kwamba, wanaume wengi hawajui kitu kuhusu masuala ya nyumbani na familia kama wanavyojua wanawake.
ahh kwavile nina jinsia mbili BAS NINA FAIDA SANA cz ntabalance kotekote job n home
<br />yaani wewe ni hermaphrodite..............................basi kweli huhitaji mtu maana unajipea mwenyewe na huna zengwe la kuhofu kuibiwa na wezi wabaya..........ila kuweza jikoni, nyumbani na nje ya hapo ...............yategemea vipaji alivyokupa Muumba kuna akina dada wengineo ambao hata kukaanga yai hawawezi hadi waliunguze tu........................mie mwaya naweza hata kutokosa maharagwe.............na kukaanga vitumbua angawaje nina bakora pekee yake.............................................lol
Ni kweli kabisa mkuu, ila mie napenda pamoja kwamba mie ni muongeaji, kuna kauli za mwanaume zinatakiwa hapo, kwamba anakujibu mawazo yako ni mazuri tuyafanyie kazi, au hili baya tusifanye uking'ang'ania anakukumbusha kwamba yeye ni mwamuzi wa mwisho, inapendeza zaidi, pamoja huwa tuna maamuzi ya busara tusing'ang'anie kila usemacho kipite bila kupingwa
Gaga, sipingani na wewe, lakini kama umesoma between line, naamini nimegusia jambo hilo, sema tu ni kwa mkabala tofauti... wakati wewe umesema "Half empty" mimi nimesema "Half full"......kitu ni kile kile.....LOL.......
Nilichosema ni kwamba,....... ngoja ninukuu hapo mahali...............'
"wanawake siku zote ndiyo wenye nguvu kwenye kauli ya mwisho.Ndiyo maana ni rahisi hata kwa wanaume wakorofi kusikika wakisema, nimeamua tufanye alivyotaka, ngoja mambo yaende vibaya, atanijua. Nimemwachia kusudi kama alivyotaka tufanye, lakini ataona mambo yakiharibika. Mara nyingi, mwanamke ndiye anayesikilizwa." Mwisho wa kunukuu.......
Nilichomaanisha ni kwamba hizo kauli za kusifiwa au kupongezwa kwa ushauri makini huwa kunafanywa na wanaume wengi, hasa baada ya kugundua kuwa wake zao wana busara katika kutanzua maswala yahusuyo familia kwa ujumla, na kama atapingana na ushauri wa mkewe mara nyingi hutumia kauli zenye busara na ambazo hazitamkwaza mkewe........ lakini hata pale atokeapo mwanaume mkorofi, mbishi, na mbabaishaji, hukubali lakini akiwa ameupokea ushauri wa mkewe kwa mtazamo hasi...........kwamba, "ngoja nifanye anavyotaka, ili mambo yakiharibika nimshikishe adabu"........ kitu ambacho mara nyingi hakitokei, labda kama atakusudia kisilete majibu mazuri kwa nia ya kutimiza malengo yake, ya kumkomoa mkewe.......... upo hapo?
lol,umenikumbuhsa mbali na kutokosa... Ila hermophrodite jinsia zote hazifanyi kazi kwa wakati mmoja. So pengine anahitaji hermphrodite mwenzie,lol!.
<br />
<br />