Acheni ngano na magugu vikue pamoja hadi tunakaribia 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Acheni ngano na magugu vikue pamoja hadi tunakaribia 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 20, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hakuna haraka ya wabunge kujiengua CCM kwa sasa kwa wale wenye mapenzi mema na mageuzi, ila tutumie falsafa ya misaafu kuwa acheni ngano na magugu vikue pamoja hadi wakati wa mavuno utakapowadia tutakapotenganisha ngano kuziweka ghalani (Chadema) na magugu kuyaangamiza. Wametangulizwa akina Malya na wengine kuendelea kuvuna mavuno ya awali na kisha akina Filikunjombe watakapogeukia upinzani 2014 nguvu zote za miguu CCM tengelem hadi kuangukia pua 2015. Lets pray for that, Siasa ni mbinu za kisayansi katika ulimwengu wa leo, sio leo leo tutaharibu mambo.
   
 2. N

  Njele JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakualiana na baadhi wanaosema hawa wabunge wa CCM wenye kupenda mageuzi wasihamie upinzani sasa hivi kwani kwa mtazamo wangu itaingiza taifa kwenye hasara zaidi ya kuandaa chaguzi ndogo ambazo zitaligharimu sana taifa. Bora wabaki huko huko na kupiga vita huku wakiandaa nguvu kwa ajili ya mapinduzi ya kweli kwa uchaguzi mkuu ujao. Ningewashauri wahamu CCM mwaka 2014. Kwa sasa viongozi wengine kama makada wa CCM wasio wabunge ndo waendelee kukapa hadi penalt ambayo itafungwa na wabunge 2014.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Naridhia hoja yako, mapema mno wabunge kujeengua CCM
   
 4. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hii kuridhia ni falsafa ya woga,yaani madudu ya mabilioni na na trilioni ya matumizi ya kisharobaro kwenye serikali yaachwe hadi 2015 ili jamaa waendelee kuiba na kuua watu wa tanzania na uchumi wao.Mkiniuliza mimi nasema walipaswa kuondoka yesterday, ili majimbo yawe wazi kura zipigwe kisayansi tujaribu kunusuru mali ambazo hawa mchwa hawajazifakamia
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hujapata falsafa ya mleta mada. Wapiganaji wazuri kama Filikunjombe wabaki kwanza huko huko hadi 2014 wakati muda wao wa ubunge unaisha ndipo waingie upinzani. Vita wanavyovipiga huko ni vizuri kwani wanayajua madudu mengi kwa vile wako chini ya paa moja.
   
Loading...