Acheni kulima miwa ya mafuta, limeni chakula!

Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima. Kilimo hiki kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajiriwa au laaa! Jambo la msingi ni kuhakikisha anajitoa kikamilifu katika kuhakikisha anawekeza akili yake katika kilimo hiki.

Kuna aina kuu 2 za miwa katika mbegu za miwa zilizoshamiri sana ambazo ni:

1. Bungala

2. Miwa myekundu.

Unachotakiwa kufanya katika kulima kilimo hiki ni:

Kwanza kabisa tafuta ekari moja ya shamba kisha anza maandalizi lakini zingatia kupuguza matumizi makubwa ya pesa kadri iwezakanavyo yaani kwa shughuli nyinginezo ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe ni vyema ukazifanya ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa mfano kulima, kupiga dawa, kupalia n.k

Tafuta mbegu ya miwa ya Bungala. Miwa hii ni laini sana na ni rahisi kuichana kwa kutumia meno, baada ya kupata miwa hii kata vipande vipande vya pingili tatu tatu. Kumbuka kwamba miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa pale tu inapokuwa imepandwa.

Ili kuzuia isiliwe na mchwa nenda katika maduka ya kilimo na ununue moja wapo ya madawa yafuatayo:-

1. TAP 4% GR: Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji kisha nyunyizia katika mashina ya miwa.

2. Taniprid 25 WG: Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji au pia unaweza kuweka kijiko kimoja cha chai katika kila shina.

3. Imida Gold: Mls 20 kwa lita 20 za maji na unyunyizie shinani.

4. Gammalin 20: Tumia gram 100 kwa lita takribani 20 za maji. Na unyunyizie katika vipande vya miwa au chovya vipande vya miwa katika maji hayo yaliyo na Gammalin 20 na ndipo uende ukavipande shambani kwako.

5. Gladiator FT.

6. Stom


Mambo ya kufanya:

Zingatia kama utatumia aidha Gladiator au Gammalin au Stom, chukua ndoo ya maji ya lita 20 kisha uichanganye na dawa uliyoinunua kisha chukua kipande cha muwa na kukizamisha ndani ya maji hayo na baadae uende kuipanda shambani kwako, hivyo uewezekano wa miwa yako yote kuote utakuwa ni mkubwa sana maana shida kubwa ni mchwa na hapo tayari utakuwa umeidhibiti.


UPANDAJI WA MIWA

Hakikisha unapokuwa unapande miwa yako acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mche na mche pia hakikisha una acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mstari na mstari.

Kumbuka awali tulisema katakata muwa wako kupata vipande vilivyo na vipingili vitatu vitatu, hivyo sasa unapokuwa unapande miwa hii hakikisha hizo pingili zote 3 zimezama ndani ya ardhi na kipande kidogo tu ndio kibakie juu ya uso wa ardhi na mche wako huo unapoutumbukiza kwenye ardhi uwe umelala wastani wa nyuzi 30.

Zile pingili katika muwa wako kumbuka ndipo sehemu hasa miwa inamokuwa inachipuka na kuota. Mantiki ya kuacha nafasi kubwa kati ya mche na mche ni kwa sababu hilo shina lako moja ulilolipanda linaweza likachipua vijimiwa vingine zaidi hata ya ishirini kama ukiliacha shina liendelee kuzaa tu kwa kadri linavyotaka na hatimaye shamba lako litakuwa msitu hata usiopitika.

Lakini kibaya zaidi ni kwamba miwa yako itakosa afya njema na mwisho wa siku miwa yako haitakuwa bora hata bei haitakuwa nzuri pindi utakapoamua au wakati wa kuuza utakapofika. Hivyo unashauriwa kuacha miwa kati ya tano mpaka kumi lakini mfano ukiacha miwa mitano katika shina moja ni dhairi hewa na mwanga vitakuwa vya kutosha shambani lakini hata chakula na virutubisho vingine kwa miwa hiyo vitakuwa lukuki na sio vya kung’ang’aniana hivyo mwisho wa siku utapata miwa mirefu na minene ambayo sokoni itakuwa na mvuto mkubwa kwa wateja.

Mfano chukulia kwamba umelima plot ndogo tu ya upana mita 50 kwa urefu mita 70, kumbukumbu namna ya upandaji miwa kama tulivyozungumza hapo awali umbali wa mita moja moja kwa kila shina. Hivyo kwa plot ya shamba hili utakuwa na miche au mashina uliyopanda kiasi cha 70×50=3500 (mashina elfu tatu na mia tano) sasa chukulia kwa hesabu rahisi kwamba kila shina umeruhusu miwa mitano tu ndio ikuwe pale maana yake kwa mashina 3500 utazidisha mara 5 ambapo itakuwa 3500×5= 17,500 hiyo ndio itakuwa jumla ya miwa itakayovunwa shambani.


Kwa tafiti zilizofanywa zinaonesha kama hautaki shida na unahitaji pesa ya haraka haraka sana huko huko shamba, basi unaweza ukajumlisha miwa yako kwa bei ya chini sana yaani tukadilie vile kwamba tunahitaji pesa ya haraka so tuuze muwa mmoja kwa bei ya jumla ya 300 hivyo jumla ya pesa utakayoipata itakuwa 17,500 × 300 = 5,250,000 (milioni tano laki mbili na nusu). Hiyo ni pesa ya haraka haraka huko huko shambani.

Ila kama ukiweza kusogea zaidi na kuuza kwa faida maana kama umeweza kupigana mpaka kuweza kuikuza ni dhairi kwamba unastahili kupata faida iliyo njema kwako hivyo ni muhimu kuangalia masoko yamekaaje pande zote za miji, ila kama utaweza kuifikisha Dar es Salaam ambako kiuhalisia soko lake ni kubwa sana.
 
Wakuu heshima kwenu,

Naomba kufahamu kuhusu zao hili, kama upatikanaji wa mbegu, muda wa kukomaa tangu kupandwa, heka moja kwa wastani unaweza kupata miwa kiasi gani, na kiasi gani cha pesa kinatosha kwenye mradi huu pamoja na eneo gani zuri la kulima miwa na ziada kama ipo.

Asanteni sana.
 
Mawazo yako mazuri. Wataalamu wa kilimo cha miwa tusaidieni. Ndio namna ya kusaidiana kutoka. Uhakikishe kuna mto karibu ili upate maji ya kumwagilia wakati wa kiangazi kwani TPC, Mtibwa, Kilombero na Kagera sugar wako pembeni mwa mito. Huko Ruvuma na Rukwa kunaweza kuwa potential areas.
 
Mkuu kilimo cha miwa ni biashara nzuri sana. Unahitaji maji mengi na mbolea ya kutosha.

Hekta moja inapasa upate kati ya tani 50-120, pungufu ya hapo itakuwa hasara. Muwa huhitaji siku 270-380 kukomaa kutegemea na hali ya hewa na kabila ya muwa.

Kuhusu mbegu, mbegu bora hupatikana kwenye mashamba makubwa kama Kilombero. Maisha ya shamba la muwa ni hadi miaka mitano kama uahudumia kitaalam, kwa hiyo ni investment ya muda mrefu na inahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia.
 
Mkuu kilimo cha miwa ni biashara nzuri sana. Unahitaji maji mengi na mbolea ya kutosha.

Hekta moja inapasa upate kati ya tani 50-120, pungufu ya hapo itakuwa hasara. Muwa huhitaji siku 270-380 kukomaa kutegemea na hali ya hewa na kabila ya muwa.

Kuhusu mbegu, mbegu bora hupatikana kwenye mashamba makubwa kama Kilombero. Maisha ya shamba la muwa ni hadi miaka mitano kama uahudumia kitaalam, kwa hiyo ni investment ya muda mrefu na inahitaji mtaji mkubwa wa kuanzia.

asante mkuu mchango wako,bt kwa wastani kwa heka inahtajka bei gan kwa wastan?
 
Salam wanajamvi. Naomba ushauri wa kilimo cha miwa. Niko Dar, na ninafikiri kufanya kilimo hicho Bagamoyo au Kigamboni. Maji ya kumwagilia yatakuwepo:
- Mbinu za kilimo bora cha miwa
- Makadirio ya uzalishaji kwa ekari
- Mbegu nzuri ya miwa (laini na inayokomaa kwa muda mfupi) inapatikana wapi?
- Hiyo mbegu nzuri inavunwa baada ya muda gani?

Ni hayo tu kwa sasa. Asanteni sana
 
Mkuu naona uzi wako umelala ngoja niuamshe....me mwenyewe nahitaji kuokota madini kwenye uzi huu nilikuwa na malengo kulima hili zao hivi karibuni.
 
Pia kwakuanzia unaweza kuja Kilombero ukakodi shamba la kupanda la kuanzia kwa majaribio kama upo tayari unaweza nitafuta nikakusaidi kwa 0654889707
 
Kama miwa inachukua miaka mitano hadi kuzeeka, nadhan ni vzr kununua kuliko kukodi shamba
 
Habar waungwana
Mwenye ujuzi wa kilimo cha miwa. Naomba maarifa hasa katika maeneo haya:-
1. Nafasi Kati mstari Kwa mstari
2. Nafasi Kati ya mche na mche.
3. Je zao hili linaweza vumilia maji Kwa muda gani na ujazo wake kiasi gani?
4. Linachukua muda gani mpaka kuvuna.
5. Magonjwa na namna ya kuya dhibiti
6. Mbegu zinapatika wapi? Na je ipi inasoko Kati ya ile yenye rangi nyekundu au njano?
7. Kwa mavuno mazuri shina ( kifungu cha miwa) kiwe na miwa mingapi?

Natanguliza shukran.

Muhimu::

Miwa ninayozungumzia sio ile ya sukari
 
Swali zuri sana,
Maswala kama Haya watu wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) wangekuwa wanaweka kwenye mitandao mtu uki google tu uweze kupata taarifa.

Hata hivyo kuna haja ya SUA kuanzisha CHannel yao humu tuwe tunapata taarifa za kilimo kwa manufaa ya wengi na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom