Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
KUPANGA NI KUCHAGUA, KUTOCHAGUA NI KUJIUMBUA!
Na. M. M. Mwanakijiji
kwa mara nyingine tena naomba niwe mleta habari mbaya kwa Watanzania. Hili wazo la kukimbilia kulima miwa ili mpate mafuta litaifikisha nchi pabaya. Kuna maeneo mengi ambayo watu walikuwa wanalima chakula sasa wanakimbilia kulima miti ya mafuta na miwa.
Yota haya yanatokea kwa sababu ya imani ya utajiri wa haraka haraka kwani kama hatuwezi kuchimba mafuta kwanini basi tusiyazalishe kwenye mimea? Ingawa mafuta yatokanayo na mimea (biofuel) ndio mojawapo ya bidhaa adimu zaidi duniani sasa hivi, hali halisi ni kuwa kwa nchi kama ya kwetu, utajiri wa kweli hauko kwenye miwa na miti ya mbono.
Ndugu zangu, tutakuwa tumeingia mtego mbaya kabisa kama tunaamini japo on principle kuwa miwa na mimbono ndiyo itakayowatoa wakulima wetu kwenye kilimo cha kimasikini na cha kuhemea. Hivi hawa wataweza kushindana na wakulima wa nchi za magharibi ambao wameacha kulima nafaka kwa ajili ya chakula na badala yake wanaanza kulima nafaka kwa ajili ya mafuta?
Mazao ya wakulima wetu waliotoka jasho kwa wingi yatakuwa kweli na bei sawa kwenye soko la dunia ukilinganisha na mazao ya mafuta toka nchi za magharibi ambako gharama ya uzalishaji wake itakuwa chini sana kwa heka moja ukilinganisha na kwetu. Je tutakapopewa bei ya chini huko mbeleni tutalalamika kweli wakati hawa hawa viongozi wanaotutia mioyo kulima mimbono watakapokuja na kusema "ndivyo hali ilivyo kwenye soko la dunia"?
Kinachonishangaza zaidi ni jinsi gani wanasiasa wetu na wataalamu wetu wameacha kuchangamia jambo ambalo kwa hakika tuna faida ya kiushandani na kutuingiza katika kitu ambacho ni wazi kitatugeuka. Leo hii tunasikia jinsi wawekezaji kutoka Brazili na nchi nyingine wote wakikimbilia Bonde la Rufiji ili waanze kulima miwa ya mafuta kwa kutupa tumaini kuwa tutaweza kushindana na mafuta yatakayozalishwa huko kwao Brazili ambako kilimo cha miwa ni cha kisasa kweli.
Lakini zaidi kinachonisumbua nikiwa mchambuzi wa masuala haya ya kiuchumi na kijamii ni wasiwasi wangu kuwa tutakapokuwa tunachangamkia tenda ya miwa na mimbono tutaanza kuacha kulima mazao ya chakula. Hebu fikirini kwa dakika moja endapo makampuni ya magharibi yakianza kuingia Nyanda za Juu kusini na maeneo yale ya bonde la Usangu, Mbalizi, n.k yakageuzwa badala ya kulima mahindi ya chakula na kuanza kulima mahindi ya mafuta?
Sizungumzii kitu cha ndoto; Wakati kimbunga kimepiga nchi ya Mynamar (Burma) hivi karibuni mojawapo ya matatizo makubwa ya chakula yametokana na uamuzi wa utawala wa kijeshi wa visiwa hivyo kuanzisha kampeni ya kutumia Ekari 200 za mraba kupanda miti hiyo ya mimbono (jatropha) ili kuzalisha mafuta ya dizeli ambayo kwa hakika ni mafuta mazuri na ya kiwango cha juu tu. Hata hivyo ili kufanikiwa hivyo ilibidi wabadilishe baadhi ya maeneo yaliyokuwa yanatumika kulima chakula na kuyafanya yalime mimbono na hilo limekuwa gharama kubwa kwa Myanmar.
Kimbunga cha Nargis kilipopiga kimeharibu maeneo mengi ya viunga vya mpunga na nafaka nyingine na hivyo kusababisha upungufu mkubwa wa chakula. Tusije tukaingia katika mtego huo.
Wenzetu China na India ambao wamekuwa wakipanda zao hili la mimbono wamekuwa wakipanda kwenye maeneo ambayo nafaka hazistawi kwani mimbono ni miti inayostahimili ukame. Binafsi ningeona kampeni hii ya mimbono ingekuwa kwenye mikoa ya kati kama Dodoma na Shinyanga na Tabora na hata baadhi ya mikoa ambayo rotuba yake ni ya mashaka. Lakini tusipoangalia tunapoanza kugawa maeneo yenye rutuba kama bonde la Rufiji kwa kulima miwa badala ya nafaka kwa hakika tunajitengenezea njaa yetu wenyewe.
Binafsi naamini kuwa kama Watanzania wanataka kweli kunufaika na kilichomo chao na kupata utajiri kutoka hicho, basi hakuna njia nyingine isipokuwa kilimo cha chakula. Leo hii wakati dunia ina hangaika na upungufu mkubwa wa chakula Tanzania nchi iliyozungukwa na maziwa makubwa matatu, mito mingi ya misimu yote tunashindwa kuingia katika kampeni ya haraka ya kulima nafaka ili mwakani tuanze kuilisha Afrika!
Watawala wetu wamebweteka mawazo yao kwenye madini, na utalii na sasa kwenye haya mafuta lakini wameshindwa kuja na vitendo vya kweli vya kukibadilisha kilimo cha chakula nchini na kukifanya kuwa ni kilimo cha faida. Watawala wetu bado hawajaona umuhimu wa kweli wa kuhamasisha mbinu, na taratibu za kisasa za kilimo na matokeo yake wameendelea kuimba wimbo ule ule wa enzi na enzi wa "mapinduzi ya kilimo".
Saa na wakati kamaa huu ndio wakati muafaka kabisa kwa taifa letu kuongoza katika mapinduzi ya kilimo cha chakula. Cha kwanza ambacho tungeweza kufanya ni kutoa unafuu wa kodi na motisha kwa wawekezaji wa kilimo cha mazao ya chakula kuja nchini. Kubwa kabisa ni kufuta kodi yoyote (ambayo bado ipo) ya zana za kilimo, kurahisisha upatikanaji wa ardhi yenye rutuba, na zaidi ya yote kuhakikisha kuwa tuna sera itakayowafanya wananchi wa maeneo mbalimbali kuwa sehemu ya uwezekaji mkubwa wa chakula aidha kwa kuingia ubia (pale wanapoouza maeneo ya mashamba yao) na pia kama wafanyakazi (badala ya kujilimia wenyewe tu).
Pia bado naamini tungerudia mambo yale tuliyokuwa tunayafanya zamani kwa ufanisi mkubwa ambapo shule za Sekondari na Vyuo vilikuwa vinashiriki kikamilifu katika kilimo cha chakula na kujitegemea. Leo hii nashtushwa na habari kuwa Waziri Mkuu ameenda Dodoma kushiriki katika harambee ya kuchangia chakula katika shule. Hili sijui limetoka wapi kama siyo uvivu wa utendaji na uzembe wa kisiasa.
Nilikosoma mimi na bila ya shaka wale wenzangu waliosoma Bweni watakumbuka kwenda shamba kulima mahindi , alizeti, ufuta na vile vibustani vya mboga mboga. Ninakumbuka nilipokuwa shule vyakula pekee ambavyo tulikuwa tunaagzia nje ni nyama, sukari, chumvi na mchele. Maharage tulikuwa tunalima sisi wenyewe, mahindi tulikuwa tunalima na alizeti tulikuwa tunalima wenyewe na kukamua mafuta yake sisi wenyewe. Zaidi ya yote bustani zetu zilikuwa zina mboga za kila aina kama mchicha, kabichi, vitunguu na nyanya (nakumbuka zile nyanya zilivyokuwa zinapotea mara zikianza kuonesha dalili ya kuwiva).
Leo hii tumefika mahali tunafanya harambe ya kuchangia chakula!! Haya bwana nyie limeni mafuta tu, hiyo siku ikifika tutaona kama watoto na watoto wa watoto wetu na wenyewe watakaa chini kulishwa matufa ya mimbono na badala ya kutafuta miwa wajikuta wanafyonza mafuta kutoka kwenye miwa!!
Haihitaji uanasayansi kuona kuwa tunakoelekea siko, tubadili njia na tuje na sera ambayo iko balanced ili tusije tukajikuta tunatilia mkazo mafuta halafu tukishapata hizo hela za mafuta, hatuna chakula cha kununua! Kupanga kwa kweli ni kuchagua, na kuchagua ni kupangua, na ukipangua utakuwa unachagua!