Achana na kitu pesa

Achana na kitu pesa

MILCAH28

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
1,140
Reaction score
328
JAMAA alikuwa kagombana na mkewe, hatimae akamwambia mkewe kwa ukali, "Unajua nimechoka sasa haya kusanya nguo zako na......" Kabla hajamalizia sentensi simu ya mkewe ikalia, kumbe alikuwa ni baba mkwe. Basi mzee akaanza kuongea na binti yake baada ya salamu, na katika kile kimya Jamaa kasikia mkwewe akisema, " Aise binti nimebahatika nimeuza ile nyumba yangu ya Moshi sasa nimeona niwatumie milioni 20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio, haya mwambie ntampigia kesho, kama ana mradi mwingine nimpe fedha kidogo". Baada ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa akamuuliza 'Ehe ulikuwa unasema umenichoka nikusanye nguo na ni kiwe nini?' Jamaa kwa upole akajibu, " Nilikuwa nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue"
 

Attachments

  • 1406756267375.jpg
    1406756267375.jpg
    100.1 KB · Views: 897
Hahahahahahah chezea pesa wewe, hapo nahisi jamaa alipiga deki na kupika kabisa!!!! Ila jamani mapenzi sio pesa. :A S wink:
 
pesa pesa ina weza ikanunua hata baridi kwenye jangwa (joto kali)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom