Acha Uzembe

Acha Uzembe

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,270
Reaction score
29,938
Mfumo wa maisha ya familia nyingi siku hizi unawalazimu wahusika kutafuta wafanyakazi wa ndani (mahausigeli) kwa ajili ya kuwasaidia kazi. Ni uamuzi mzuri kwa sababu hurahisisha kazi ya kutunza familia na wengi huwa msaada mkubwa, achilia mbali wale wachache wenye tabia zisizofaa.

Hata hivyo, kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, vilio vya wanawake waliopo kwenye ndoa kulalamika kuibiwa waume zao na wasichana wa kazi vinazidi kuongezeka. Katika kila wanawake kumi wanaoishi na wasichana wa kazi, saba waliwahi kutendwa kwa waume zao kusaliti ndoa na mahausigeli au kujaribu kuwashawishi wavunje nao amri ya sita. Wanawake wengi ambao wapo katika uhusiano rasmi watakuwa mashahidi wa hili.

Yaani unaenda kumchukua dada wa kukusaidia kazi za nyumbani kijijini, unamleta mjini, unamhudumia kwa kila kitu, anaanza kuoga na kupendeza na mwisho unajikuta ukisaidiwa hata yale ambayo hukuomba kusaidiwa au ambayo hayastahili kuwa na msaidizi.

Wanawake wengine wanajeruhiwa zaidi baada ya waume zao kuishia kuwapa mahausigeli ujauzito au kuzaa nao! Dada wa kazi anageuka na kuwa mke mwenzio. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili na ningependa tuzijadili kwa pamoja.

1. KUJISAHAU
Wanawake wengi wana kawaida ya kujisahau wanapopata wasichana wa kuwasaidia kazi. Kama kipindi cha nyuma kabla hajapata hausigeli mwanamke alikuwa akimfulia mumewe, kumuandalia chakula kizuri na kutunza vizuri familia, akishapata dada wa kazi, hujisahau na kuacha kutimiza wajibu wake kama mke.

Matokeo yake, unakuta dada wa kazi ndiyo anashughulikia mambo yote muhimu yanayomhusu mume kuanzia anapoamka asubuhi mpaka usiku. Ndiyo! Mumeo akiamka asubuhi, dada wa kazi ndiyo anaenda kutandika kitanda, anamuandalia maji ya kuoga, anamuandalia kifungua kinywa na kumnyooshea nguo za kuvaa siku hiyo.
Mchana au jioni akirudi, yeye ndiyo anampokea, anamuandalia maji ya kuoga kisha anamuandalia chakula cha usiku. Yeye ndiye anayefua nguo zote za mumeo, hata zile ambazo hastahili kuzifua. Unategemea katika mazingira kama haya nini kitatokea kama siyo mumeo kuanza kumpenda hausigeli?

2. UKARIBU ULIOPITILIZA
Suala lingine ambalo linawaponza wanawake wengi waliopo kwenye ndoa, ni kuruhusu waume zao wawe na ukaribu wa kupitiliza na mahausigeli. Kutokana na ubize wa kazi au mtindo wa maisha, unakuta mwanamke anakuwa bize na mambo yake mengine na kusahau wajibu wake wa msingi wa kuwa karibu na mumewe.

Kwa mfano, usiku mama anawahi kwenda kulala kwa kisingizio cha uchovu na kumuacha mumewe na hausigeli wanatazama runinga pamoja sebuleni. Au unakuta asubuhi, mama wa familia anawahi kuondoka kabla ya mumewe na kuacha mwanya wa wawili hawa kuwa karibu na kuzoeana.

Jioni pia, baba anawahi kurudi nyumbani lakini akifika, mkewe anakuwa bado hajarudi au hata kama amerudi, yuko bize na mambo mengine kabisa. Hakuna mtu anayependa kukaa na upweke kwa hiyo kwa sababu umeshindwa kutimiza majukumu yako, taratibu atahamishia ukaribu kwa dada wa kazi, watazoeana na kuanza kuvukiana mipaka.

Unategemea mwisho utakuwa ni nini?
 
Kuna wanawake ambao kazi zao ni za kusafiri, ile umerudi tu nyumbani ukienda ofisini unaaandika ripoti ya safari, ikifika kwenye kikao wameipenda unapangiwa safari nyingine. Safari hizi ndio zinaleta uzima wa nyumba, kuna wazazi wa kuwahudumia, ada ya watoto, sasa baba anajikuta muda mwingi anabaki na watoto na dada wa kazi. Vishawishi hapo ni vikubwa.
 
Mfumo wa maisha ya familia nyingi siku hizi unawalazimu wahusika kutafuta wafanyakazi wa ndani (mahausigeli) kwa ajili ya kuwasaidia kazi. Ni uamuzi mzuri kwa sababu hurahisisha kazi ya kutunza familia na wengi huwa msaada mkubwa, achilia mbali wale wachache wenye tabia zisizofaa.

Hata hivyo, kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, vilio vya wanawake waliopo kwenye ndoa kulalamika kuibiwa waume zao na wasichana wa kazi vinazidi kuongezeka. Katika kila wanawake kumi wanaoishi na wasichana wa kazi, saba waliwahi kutendwa kwa waume zao kusaliti ndoa na mahausigeli au kujaribu kuwashawishi wavunje nao amri ya sita. Wanawake wengi ambao wapo katika uhusiano rasmi watakuwa mashahidi wa hili.

Yaani unaenda kumchukua dada wa kukusaidia kazi za nyumbani kijijini, unamleta mjini, unamhudumia kwa kila kitu, anaanza kuoga na kupendeza na mwisho unajikuta ukisaidiwa hata yale ambayo hukuomba kusaidiwa au ambayo hayastahili kuwa na msaidizi.

Wanawake wengine wanajeruhiwa zaidi baada ya waume zao kuishia kuwapa mahausigeli ujauzito au kuzaa nao! Dada wa kazi anageuka na kuwa mke mwenzio. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili na ningependa tuzijadili kwa pamoja.

1. KUJISAHAU
Wanawake wengi wana kawaida ya kujisahau wanapopata wasichana wa kuwasaidia kazi. Kama kipindi cha nyuma kabla hajapata hausigeli mwanamke alikuwa akimfulia mumewe, kumuandalia chakula kizuri na kutunza vizuri familia, akishapata dada wa kazi, hujisahau na kuacha kutimiza wajibu wake kama mke.

Matokeo yake, unakuta dada wa kazi ndiyo anashughulikia mambo yote muhimu yanayomhusu mume kuanzia anapoamka asubuhi mpaka usiku. Ndiyo! Mumeo akiamka asubuhi, dada wa kazi ndiyo anaenda kutandika kitanda, anamuandalia maji ya kuoga, anamuandalia kifungua kinywa na kumnyooshea nguo za kuvaa siku hiyo.
Mchana au jioni akirudi, yeye ndiyo anampokea, anamuandalia maji ya kuoga kisha anamuandalia chakula cha usiku. Yeye ndiye anayefua nguo zote za mumeo, hata zile ambazo hastahili kuzifua. Unategemea katika mazingira kama haya nini kitatokea kama siyo mumeo kuanza kumpenda hausigeli?

2. UKARIBU ULIOPITILIZA
Suala lingine ambalo linawaponza wanawake wengi waliopo kwenye ndoa, ni kuruhusu waume zao wawe na ukaribu wa kupitiliza na mahausigeli. Kutokana na ubize wa kazi au mtindo wa maisha, unakuta mwanamke anakuwa bize na mambo yake mengine na kusahau wajibu wake wa msingi wa kuwa karibu na mumewe.

Kwa mfano, usiku mama anawahi kwenda kulala kwa kisingizio cha uchovu na kumuacha mumewe na hausigeli wanatazama runinga pamoja sebuleni. Au unakuta asubuhi, mama wa familia anawahi kuondoka kabla ya mumewe na kuacha mwanya wa wawili hawa kuwa karibu na kuzoeana.

Jioni pia, baba anawahi kurudi nyumbani lakini akifika, mkewe anakuwa bado hajarudi au hata kama amerudi, yuko bize na mambo mengine kabisa. Hakuna mtu anayependa kukaa na upweke kwa hiyo kwa sababu umeshindwa kutimiza majukumu yako, taratibu atahamishia ukaribu kwa dada wa kazi, watazoeana na kuanza kuvukiana mipaka.

Unategemea mwisho utakuwa ni nini?
hebu jaribu kusoma vitabu vitakatifu ili ujue majukumu ya dada wa kazi,utastaajabu kuwa ukisemacho hapo kipo tangu kale,sawa na umalaya tu,vipo tangu enzi mkuu!
 
hebu jaribu kusoma vitabu vitakatifu ili ujue majukumu ya dada wa kazi,utastaajabu kuwa ukisemacho hapo kipo tangu kale,sawa na umalaya tu,vipo tangu enzi mkuu![/

Napenda sana kama utakuja hapa unionyeshe baadhi ya maneno matakatifu yakieleza majukum ya Dada wa kaz
 
Hata hivyo, Abrahamu na Sara hawakupata mtoto, naye Sara aliyekuwa na umri wa miaka 75 akawa hana tumaini lolote la kupata mimba. Hivyo, akamwambia Abrahamu: “Yehova amenifunga nisizae watoto. Tafadhali, lala na mjakazi wangu. Labda ninaweza kupata watoto kutokana naye.” Ndipo Abrahamu akamchukua Hagari kuwa mke wa pili, akalala naye, naye akapata mimba. Mara tu Hagari alipojua ana mimba, akaanza kumdharau bimkubwa wake. Sara alimlalamikia Abrahamu kwa uchungu na kumfedhehesha Hagari, na hivyo akamfanya akimbie.—Mwanzo 16:1-6.
 
Hata ukimlamba atatoka tu mwanaume ni mwanaume ila kiukweli mwanaume wa ukweli hajishushi hata siku moja kulala na mdada wa kazi fanya utafiti familia zinazokumbana na hivyo vibwanga utAkuta mume mlevi,hajakuoa kwa makubaliano ni force marriage either ulikuwa na mimba au hela au alitamani tu ila hajapenda na pia anamatatizo fulani i mean hajakamilika anakaupungufu fulanii maana kama kweli yupo fresh hawezi huu ndio ukweli pia nahii haridhiki tamaa makusudii hivyo vyote vimechangia
 
Hao walikuwa na shida ya mtoto.....!!!!!!
Na Mungu hajahalalisha
 
Kifupi wanawake wengi wanajisahau sana kwenye majukumu ya familia zao kwa kigezo cha kazi zina wazidi na hili ni kosa wafanye marekebisho koz mwanaume nae huwa ana penda kuwa busy ila akiwa na mkewe apikiwe apetiwe petiwe kidogo eeh kama hivyo yaani
 
Back
Top Bottom