Acha maisha ya zimamoto

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
ACHA MAISHA YA ZIMA MOTO

Watu wanaofanya kwenye idara ya zima moto kazi yao ni moja tu, kusubiri moto utokee na kwenda kuuzima. Kama hakuna moto, hawana kazi kubwa, ila moto unapotokea ndipo hufanya kila juhudi kuuzima.

Sasa kuna watu wengi kati yetu ambao wanaishi maisha ya zima moto.Watu hawa wanaweza kuwa na malengo na mipango mizuri ila wanashindwa kuitekeleza kwa sababu ya mtindo wa maisha waliochagua kuishi ambao ni wa kuzima moto.

Watu hawa huhangaika kuzima kila moto ambao unajitokeza kwenye maisha yao. Watu hawa huishi siku yao kutokana na kitu kilichotokea.

Husumbuka na kila kitu kinachotokea hivyo kushindwa kufanyia kazi malengo waliyojiwekea. Na mara nyingi moto wanaozima hauhusiani kabisa na malengo yao hivyo kujikuta wakizidi kupoteza muda.

Kuna uwezekano mkubwa na wewe ni mmoja wa wanaoishi kwa kuzima moto.
Ngoja nikupe sifa za wanaozima moto uone kama sio mmoja wao.

1. Kama huwezi kutenga muda wa kufanya kuondokana na kelele nyingine zote wewe ni zima moto.

2. Kama huwezi kukaa mbali na simu yako kwa muda ambao unahitaji kufanya kazi wewe ni zimamoto.

3. Kama unajibu haraka kila ujumbe unaoingia kwenye simu yako, au kuperuzi mitandao ya kijamii ukifikiri kuna kitu kinakupita, wewe ni zimamoto.Kama wewe umeingia kwenye kundi la zima moto, nina habari mbili kwako, moja nzuri na moja mbaya.

Naanza na habari mbaya, hutaweza kufikia mafanikio kwenye maisha kwa kuwa zima moto.Na habari nzuri ni kwamba unaweza kubadili tabia hiyo ya zima moto.

Ni wewe kujijengea nidhamu ya kuweza kusimamia mipango yako na kuachana na mambo yasiyokuwa muhimu kwako.

Ni vigumu lakini inawezekana.
 
Kweli kabisa, ila Mkuu uliwahi kufanya kazi zimamoto au umeamua tu kulitumia hilo neno..
 
Hahaa,ngoja nilog off kwanza bila kucoment chochote ili nisiwe zima moto
 
Napenda post kama hizi ...sio za wema kabeba mimba sijui Diamond kafanya vitu gani.... Mtoa mada uko vizuri!
 
Na ukikoment bila kufikiria kwa kina kuwa hicho unachoandika kina maana au hakina....pia ni zima moto doh!!
 
Back
Top Bottom