Acha kusumbua watu wakuchangie kwenye harusi yako

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
274
Reaction score
486
Harusi ni sherehe inayofanyika baada ya agano la ndoa.

Unapowaza kufanya harusi usifikirie kuhusu pesa zilizopo kwenye mifuko ya watu.

Angalia mfuko wako mwenyewe kama unaweza kumudu gharama za sherehe ya harusi au ufunge tu ndoa bila sherehe.

Hakikisha huna deni kwa mtu yeyote baada ya harusi. Fanya jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako, sio kwa kusubiri michango ya watu wengine.

Harusi ni yako, usiwabebeshe watu wengine majukumu yasiyostahili. Usianze kutoa lawama na kuona wale wasiokuchangia kama wana roho mbaya wakati harusi umeipanga mwenyewe.

Harusi sio msiba labda useme umetokea bila kutarajia. Harusi ni jambo la kupanga na ni jambo la maanndalizi ya muda mrefu. Hivyo unayo nafasi ya kujipanga mwenyewe.

Unaweza kufanya harusi ya kiwango unachotaka bila kuomba michango ya watu.

Unaweza kufanya harusi ya gharama kubwa au unaweza kufanya harusi ya gharama ndogo. Inategemea na wewe mwenyewe ulivyojipanga.

Mfano: ili kufanikisha harusi yako unaweza kuweka target halisi kama vile TZS 5M, 10M, 15M au zaidi kulingana na aina ya harusi unayotaka.

Anza kuweka akiba mapema hata kama ni kidogo kidogo kama vile TZS 100,000–300,000 kwa mwezi.

Punguza matumizi yasiyo ya lazima kwa muda (hii inauma kidogo lakini ina matokeo makubwa). Ili kile unachojibana kije kifanikishe gharama za harusi.

Jitahidi kutengeneza vyanzo vingi vidogo vya mapato ikiwezekana (side hustle, biashara ndogo, kazi za ziada). nk

Usisite kuambia familia au rafiki zako wa karibu mapema kwamba natarajia kufunga ndoa mwenzi fulani pia nimepanga kufanya kasherehe kidogo.

NB: Hapa ni unawapa tu taarifa ila sio kuomba michango yao. Kisha wasikilize, wengi watakupongeza na kama wataguswa baadhi watakuchangia hata bila wewe kusema wakuchangie.

Kama ni sherehe ya ukumbini au nyumbani, tengeneza kazi za kuwaarika kuhudhuria tu sio za kuchangia.

Hakika wengi hawatokuja bure. Kuna wengine watakuchangia kabla na wengine watakuja na zawadi zao mikononi walau wakufute jasho.

Ukiwapa kadi za kuchangia amini kabisa wale watakaoshindwa kutoa michango hawatoweza kufika kwani watajiona kama hawahusiki na harusi hiyo.

Kumbe kama ungewaarika tu wangeweza kuja na chochote au wanaweza kusema ndugu yangu nimeshindwa kufika lakini kidogo changu hicho kitasaidia.

Mwisho wa siku, harusi ni siku moja tu, lakini amani na uhuru wa kifedha unadumu miaka mingi.

Wewe mwenyewe uko wapi katika hili?
Unaamini katika kuchangiwa au katika kujipanga mwenyewe?

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.

Content By George Francis
criadordefrases-meme-1770189990905.webp
 
Hakuna anayelazimishwa kuchangia harusi. wanaochangiana waacheni waendelee kuchangiana, wewe usichange na usiombe mchango. ila kama umechangiwa lazima uchangie hilo ni deni.... Mtu anachangiwa halafu ikifika yeye kuombwa mchango makelele kila mahali...
 
Watu tunachangia watu walewe bar sembuse jambo la heri la harusi!!

Anae changia achangie asiye taka apige kimya , tusipangiane maisha
 
Content By George FrancisView attachment 3539471
Naunga hoja mkono
 
Wengne tulipokuja mjini ndo tukaona watu wanachangiwa sijui send off mara arusi

kule ukuryani kwetu unajitegemea kuanzia mahari hadi gharama ya harusi
hata zawadi zitokanazo na sherehe huwa ni ziada, tunachojali ni kuwa watu wale washibe
Tusipowachangia wanatuchukia
 
Hakuna anayelazimishwa kuchangia harusi. wanaochangiana waacheni waendelee kuchangiana, wewe usichange na usiombe mchango. ila kama umechangiwa lazima uchangie hilo ni deni.... Mtu anachangiwa halafu ikifika yeye kuombwa mchango makelele kila mahali...
Wengine wanalazimisha, watu hatuwasiliani, hatupigiani simu wala hawana mpango na sisi ila siku wakitaka kuoa ndio tunawaona na kadi zao za michango. Tusipochangia wananuna
 
hao achana nao... shikana na wale waliokuwa nawe wakati wa mahitaji. kununa kwao ni heri yako maana kibubu chako hakitapungua
 
Back
Top Bottom