Acha Kumwibia Mwajiri Wako

Waajiri wenyewe wa Kiswahili nao ni wezi,wanakwepa Kodi na kulipa mishahara Mbuzi Wafanyakazi.
Mimi nikiajiriwa na Mzungu,siibi ila Maboss wa Kiswahili hawa,hapana!
 
Vyovyote utakavoona ww kikubwa maisha yaende! Mbona wengi tu wamepiga bingo serikalini, makanisani, misikitini na kwenye NGOs na maisha yanaenda vzr we tia ulokole ufe maskini golden chance haichezewi
Maisha ya kupiga bingo mali isiyo yako hayataiacha salama familia yako siku ukifa.

Rizika na unacho pata kihalali ipo siku utatoboa.

Usiwaige hao wezi waliolaaniwa.
 
Waajiri wenyewe wa Kiswahili nao ni wezi,wanakwepa Kodi na kulipa mishahara Mbuzi Wafanyakazi.
Mimi nikiajiriwa na Mzungu,siibi ila Maboss wa Kiswahili hawa,hapana!
Ujumbe unasema "acha Kumwibia Mwajiri Wako"

Haijalishi ni mzungu ama mmatumbi, acha wizi.
 
Mimi ni mfanyakazi wa kawaida tu si tajiri ila pia si maskini. Hela ya kula tu ninayo Niko hapa Mwanza.

Ili kujiongezea kipato nilifungua bizness kubwa kiasi mtaji kama 8m nikaajiri vijana sita wa kiume wakawa wakifanya bizness pesa inaingia wanalisha familia zao na posho nawapa wakaanza kuiba hadi kufikia kutangaza na kujisifia eti mi ni mjinga wanaiba sana na watanifilisi stori zikanifikia nikafunga ile bizness acha vijana na familia wapauke wengine wakatimka kusikojulikana!

Nikafungua bizness ingine kubwa kiasi mtaji kama 3m nikaajiri single mothers 4 waliolekezwa na wazee wa mtaa kunifuata kuomba msaada , mama mmoja alikuwa akilala njaa na wanawe hadi kulazwa kwa vidonda vya tumbo nikamhurumia sana. Baada ya miezi miwili business ikawaka wadada wote wakajisahau wakaanza kushindana kuiba na kusuka minywele ya laki na mawigi ya laki mbili!! Nikawa nawashangaa pesa kidogo tu ushamba umewajaa!malipustick na wanja hadi masikioni na Wala sikuwa nikichukua pesa nilitaka faida ikuze mtaji na hawakuweza kutunza pesa zote zikaishia vikoba na mavazi Tena kwa mashindano na sifa! Miezi 8 tu business ya pili iliyokuwa imestawi nayo ikafa hata sijui wadada walikoishia.

Bizness zikanishinda nikaamua kujikita tu na kazi yangu ya Utumishi wa wadanganyika!

Watu maskini wengi bongo ni wajinga sana hata ukiwakwamua lazima waibe wakukomoe baada ya muda bizness zinakufa wanarudi kwenye msoto waliouzoea!!

Dawa ya wizi ni kufunga bizness na kubadili namba ya cm Ili mizinga na vichomi visikuandame kwa wale wajinga walioua bizness!

Kwasasa nina hakika wizi wa mbongo ni wa Asili ya mababu zetu ambao wameturithisha nasi tunaiba kushinda waalimu zetu mababu!

Hakuna dawa ya wizi wetu wabongo!
 
Ujumbe huu uwafikie watumishi na Viongozi wote kisiasa, waache mara moja kutuibia wananchi, sie ndo Waajiri wao Eti!!
 
"Dawa ya wizi ni kufunga bizness na kubadili namba ya cm Ili mizinga na vichomi visikuandame kwa wale wajinga walioua bizness!"

Sifungi biashara yangu kwa sababu ya mtumishi mwizi .Namtimua ,naajiri mwingine biashara inaendelea .Ni mwaka wa saba sasa naajiri na kutiamua,na biashara Bado IPO na inakua
 
Wanatubana sanaa na kwenye mishahara wanacheleweshea

Mshahara wenyewe tulikubaliana 550k amelia lia mpaka 250k
Mtu kama huyo kwann usimuibie

Ofisi kufungua saa 11 hasubuhi kufunga saa 4 usiku na siku kukiwa na meeting au event anatukalisha mpaka saa 8 usiku

Tutawaibia mpaka yesu anaporudi ni haki hatuibi tunachukua haki zetu tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…