Account ya Dogo Jembe imeingiliwa, Je sisi wengine tutapona?

Hakuna kuingiliwa mzee....jamaa kapost mwenyewe sasa anaona moto umewaka anajaribu kuuzima

Ujinga tu, alipost kwa hasira sasa washauri wamewambia kachemka itamharibia , ndo anazuga, mara anapongeza kasi..ni mjinga fulani tu, opportunist.
 
Yule alidhani atakua PM, kupenda sifa kunamuharibia.
 
Ohoooo, asije akawa amesikia amekatwa kwenye baraza ndo mana ameamua kuzua haya
 
Unapita kimya kimya huku umekunja ndita Mr kiparangoto imekula kwako.
 
Mbona hakutoa hilo tamko la kuingiliwa immediately, mpaka watu wamecharuka ndio ajidai aliingiliwa?
 
Dogo Jembe angelikanusha tangu siku ya kwanza zile katuni zilipowekwa tungelimuelewa lakini anapojaribu kuzima moto wakati maji yashachemka ni wazi ametingisha mafiga na maji ya moto yatamuunguza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…