rmashauri
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 3,011
- 454
Habari wakuu!
1.Nini tofaauti ya current account na Saving account?
2.Je hyo USD account napewa ATM card? Kama ndio ATM kuna $ pia?
3.Nikiwa na $ account kwenye bank naweza nikarusha hela(TT) kununua gari japan? Je cost zake zipo vp? Maana bank nyingine kutuma TT ni 60$
4.Nini faida ya kua na $ acc vs TZS acc?
Mkuu majibu ya maswali yako hivi:
1. Current akaunti ni akaunti ya kibiashara (hufunguliwa na makampuni makubwa na madogo) wakati savings ni akaunti ya mtu binafsi ya kutunza pesa zake. Masharti ya transactions ya pesa yanatofautiana na hapa ni maelezo marefu
2.Kwa uzoefu wangu mdogo, mabenki yetu hayatoi ATM kwa Forex accounts wanakupa kadi tu za kawaida ambapo ni lazima uende kaunta pale unapotaka kuchukua au kuweka pesa
3. Jibu ni ndiyo waweza kurusha USD kutoka akaunti yako moja kwa moja kwenda Japan kununua gari. Gharama zinatofautina kutoka benki moja kwenda benki nyingine, the cheapest ni Bank of India wanaotoza USD 12, CRDB na NMB ni USD 50
4. Faida ya kuwa na USD account Vs Ths account ni kuwa, thamani ya pesa yako inazidi kuongezeka dhidi ya shilingi inayoporomoka kila wakati