ACACIA Mining PLC: We do not agree with President Magufuli Committee's findings...

Haya hao wataalam wamesema kuna wizi ila wazungu wanadai taarifa zao ziko wazi basi sawa tusubiri nani ataumbuka mwishoni maana mambo ya sheria ni facts na vielelezo so ni muda tu ndio utakaoamua ila uzuri lisu amewashauri mapemaaaaa mje mshindwe wenyewe tu maana kila tukishauri mnasema tunapinga

Weka kumbukumbu zako vizuri acha porojo za kitoto, hao Acacia wametoa taarifa yao ya kwanza mchanga ulipozuiliwa wakasema mchanga hauna thamani yoyote.

Leo wanasema unatamani lakini siyo kiasi hicho kinachosemwa.

Kwa nini wawe na semi zaidi ya mbili, wanadanganya.

Yaani wewe unajiita zitto junior , kumbe poyoyo tu Kama zitto senior!?
 
Ripoti ya wataalamu ndiyo ushahidi. Ni wajibu wa mtuhumiwa kukanusha kwa ushahidi pingamizi!

WanaJf na ACACIA wameshupalia ripoti hii ya kitaalamu, wasubiri ripoti ya Tume ya Wanasheria na Wachumi kwanza, kwa kuwa walioguswa ni watumishi tu wa umma.

Kiherehere cha nini kama siyo kukiri udanganyifu!

Hata kama mkataba unawaruhusu kusafirisha mchanga siamini kama ni 'open cheque'!!!
nyinyi watu mnahitaji elimu sana,kamati inapendekeza walipe the accruing amount kwa madini ambayo eti walikuwa hawalipii kodi na mrabaha,wao watakataa kulipa kwa sababu watakwambia walikuwa hawachambi hayo...wewe utatakiwa utoe ushahidi kuwa walikuwa wanayachimba...hapo kunahitaji phd kweli kuelewa?
 
Haya hao wataalam wamesema kuna wizi ila wazungu wanadai taarifa zao ziko wazi basi sawa tusubiri nani ataumbuka mwishoni maana mambo ya sheria ni facts na vielelezo so ni muda tu ndio utakaoamua ila uzuri lisu amewashauri mapemaaaaa mje mshindwe wenyewe tu maana kila tukishauri mnasema tunapinga
Sasa wew ulitegemea wakubali? Wakati ceo yupo kikaangoni na board sasa hivi. Lissu nani nchi hii. Kama lissu mshauri mzuri basi chadema ingekuwa imeshida uchaguzi nchi hii. Hapana aisee abaki tu kuwa mshauri wa CDM na sio taasis kubwa kama serikali
 
Twendeni taratibu, container bado zipo na hata hao Acacia kama hawariziki wanatakiwa wawalete wataalam wengine kuchunguza, Hakuna cha SGS wala ACE wote hao wapiga dili bandarini, Sampuli inayochukuliwa wanaipeleka maabara KENYA but ripoti inayotoka kule inatunzwa tu kwenye makabrasha na kutumwa ulaya.

Hata kama kuna kilichoongezeka hawakitoi wanakiwasilisha kama kilivyo kwa waliowapa kazi (ACACIA)
Ndio. Kama hawaridhiki basi walete mwingine achunguze. Tafiti inapingwa na tafiti. Sasa wanapingana na ripoti bila hata kuiona na kuisoma.
 
Maamuzi yakifanyika bila tume ya uchunguzi au ushirikisaji wadau wengine, inaitwa kukurupuka.

Tume imeundwa, tena ya wataalamu, ripoti yao siyo sahihi!

nyabhingi: tueleze njia sahihi ichukuliwe kuhakika uchimbaji madini nchini!
sitaongea maneno mengi mkuu,unaikumbuka kamati teule ya mwakyembe iliyochunguza sakata la richmond?unajua tulishindwa ile kesi kwa kufuata ujinga wa mapendekezo ya mwakyembe?
 
Watanzania bwana kuna jambo moja hua mnasahau, nimemsikia mwenye nchi yake anapiga hesabu toka 1998 tumeibiwa kiasi gani cha fedha kwa kusafirisha mchanga nje, wakati huo huo mtanzania anashindwa kujiuliza kwani toka 1998 ni akinanani walikua wanaongoza hii nchi??? Walikua wanatunga sheria za hii nchi, akinanani walipaswa kuisimamia hii nchi isifike huko ilikofika??? Kama sio hawa hawa wamekuja na sura nyigine mwili uleule????

Yaaani nchi muiingize kwenye matatizo wenyewe tena makubwaaaaa, ya rushwa umasikni ufisadi wakutosha afu leo mnajitia inawauma sanaaaaaaaa, eti mmeumia mmeibiwa sana sasa imetosha, unafki wahali ya juuu!!

ivi uyu 1998 si alikua kwenye serikali kama waziri, nayeye alifanya nini????? Alishauri nini?? Kama alivyo mtumbua mhongo kwa maswali hayo kwamba alikua anafanya nini na yeye alifanya nini?? Eti kathubutu, kathubutu nini mfano!???kutuonesha chama chake kilivyo na watu weziiiiii?? Kilivyo shindwa kusimamia mali za nchi??? Afu mnapiga kelele mnaambiwa kabisa lichama na serikali yake ndio limefanya haya toka 1998 mnakenua!!! Haya Tunalipwa sasa?!!! Au nimwendo wa time na kamati kutoa ripoti kisha kutumbua na kutengua then miaka 5 kwishney nothing new??

Na Nyie vyombo vya usalama mlioambiwa mchumguze na kukamata walio husika kwenye hili msiishie hapo tu mchunguze wooote walio kua serikalini toka uhuru kwa kutuletea haya matatizo na myakamate kabisaaaaa yoote majizi yalioifikisha nchi hii hapa afu leo wanajifanya eti ni akina malaika wamekuja kutuokoa!!! Eti inawauma, inawauma nini??? Inawauma kushiriki udalali wakutuibia chini ya mwavuli wa lichama menu au???

Ujinga hii nchi bado upo mkubwa sanaaaaa!! Yaaani mvuruge wenyewe afu saiz mnajitia kutafuta mchawi!!!???
Hicho ndo watanzania wengi tunashindwa kuking'amua kama tatizo ni ACACIA au sheria zetu za madini,kama wanatuibia tatizo lipo kwenye sheria kupitia kwa waliopewa dhamana ya kuzitunga na kusimamia,katika hili kama watanzania haturidhiki na mapato yanayotokana na madini kuna haja ya kulekebisha sheria zetu.
Haiingii akili mfano katika metallic mineral royalt ni 4% tu?? kuna haja ya kufanya mapitio ya sheria na sio kukurupuka tu.
 
Huko sawa kabisa na mii nakubaliana na hilo. Wawajibishwe kwa kudanganya kama itathibitika pasipo na shaka. Ila kumbuka huwezi kutumia data za haya makontena 200 na ushee kama base ya claims zako, lazima uwe na twakimu za makontena yote tangu shughuli hiyo ianze, unazipata wapi? lazima uende maabara zilikopimwa na kule zinakofanyiwa extraction na mwisho utatumia twakimu walizokupatia. usifikiri hayo matrilioni yote ni yako kama hizo takwimu ni kweli. Utlipwa asilimia mliyokubaliana kwenye mkataba na hapo ndo kuna tatizo kubwa kweli kweli. Mikataba ni mibovu na kinyonyaji na inaweza kukutia hasira kweli kweli. Mahakama inatoa hukumu kwa evidences na mikataba na sio bla bla nyingine. wenzetu wanajua sisi wazembe so evidences za kutosha wanazo na sisi labda ni hizi za jana tu ndo sahihi, zilizobaki tutamuia evidence zao tu, upende usipende


Nakubaliana nawe.

Na hapa sasa ndipo wanasheria wanasema wako na weredi wasimame tushinde hii kesi ya kuibiwa na wazungu koko na wazungu pori
 
Kuna tume inayohusisha wanasheria nayo itatoa ripoti yake na mapendekezo.
Rais hajatoa conclusion na ndio maana amesema wanasubiri mapendekezo ya tume zingine kwanza.
Sasa kama wanasheria wamejumuishwa kushauri unamashaka gani na wansheria wetu.
Hii ni vita ya uchumi angeweza rais kuangalia na kukaa kimya kama waliomtangulia na tukaendelea kualalamika tuuuu
Umenena vyema mkuu. Tusubiri matokeo ya hiyo tume nyingine. Ila hii vita Kali, Ndo maana unaona vilio vingi maana mkono wa Acacia umetembea ili watu wawe na vipaza sauti, hawaishi kuwasemea.
 
Vibaraka wa wezi kumbe wamejaa humu sikujua hili! hawa jamaa wa madini kumbe wezi tu, wanatuibia sana na ndiyo maana madini hayana faida yeyote kwetu.
 
sitaongea maneno mengi mkuu,unaikumbuka kamati teule ya mwakyembe iliyochunguza sakata la richmond?unajua tulishindwa ile kesi kwa kufuata ujinga wa mapendekezo ya mwakyembe?
Umetaja tu Tume ya Mwakyembe bila kurejea kilichotokea na mapungufu yake, ili ueleweke.

Niliomba uweke uzalendo mbele kwa kutoa ushauri wa jinsi ya kumaliza suala hili la kusafirusha mchanga. Badala yake unaendelea kulaumu.

Hakika anayeona mapungufu huwa na jinsi mbadala
 
Yaan watanzania humu ni wajinga sana, eti tulipe fidia? hivi mnawaamini hawa makaburu? utafiti hupingwa kwa utafiti na si maneno, huyu anatoa hiyo statement ili kuwapooza wanahisa ambao hisa zao zimeshuka kwa kiwango cha kutisha huko London, sasa mlitaka asemeje? acheni upumbavu wa kijinga wa kuanza kumlaumu Rais, kuweni na akili za kufikiri hata kidogo, makontena yapo bandarini sasa tatizo ni nini?

Kwa hiyo wataalamu wetu hamuwaamini? mnadhani wametoa taarifa hii mbinguni? acheni ufara ninyi....
 
We pasikali, ivi mlikua wapi sikuzote?? Nani chanzo cha haya yote, nani alipewa mamlaka ya kulinda na kusimamia hii nchi namalizake zote toka 1998!!! Kama alivyo tumbuliwa muhongo na kuagizwa vyombo vya ulizi viwachunguze wahusika wote bila unafki i need to see the folowing people in jail!!!

1. B . mkapa
2. J.K.Kikwete
3. All minesters since 1998!!! Wote walikula njama ya kushiriki kuliibia hili taifa wataifishwe mali zao zoote kulipa hasra walio tupa!!! Then acacia ifate!! Mengine unafki tu!!! Tuone nani atabaki!!!
Mkuu Yoga, tuko akina sisi kazi yetu ni kusema tuu na hapo ndio mwisho wa uwezo wetu.
Ukipata muda pitia hapa
angalia nimesema nini? . Haya niliyoyasema humu yatakuja gundulika na kamati ya raisi wa 2025!.
Gesi asili: Is it "day light robbery?!" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Paskali
 
Nakubaliana nawe.

Na hapa sasa ndipo wanasheria wanasema wako na weredi wasimame tushinde hii kesi ya kuibiwa na wazungu koko na wazungu pori
Na palipo nitia shaka kwenye ripoti ya jana ni zile minerals zilizokuwa kwa kiasi kidogo sana kama kilo chache tu kwa kontena la tani 20. Hayo wenzetu wanayaita with no commercial values kwa sababu gharama ya kuyapata ni kubwa kuliko pesa utazoyauzia. But jana pia kamati wameyahesabu wakitumia market value bila ya kujali extraction cost.
 
Back
Top Bottom