ACACIA kutoa notisi ya kuishitaki Tanzania na hatma ya majadiliano

Taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa TLS imeeleza kwamba kampuni kubwa ya Uchimbaji Madini, Acacia imetoa notisi ya kuishitaki Tanzania kwa lengo la kudai fidia ya hasara iliyotokana na zuio la Makanikia, kiasi cha takribani Trilioni 5 za kitanzania.

Acacia ni kampuni inayomilikiwa kwa zaidi ya asilimia 65 na kampuni ya Barrick Gold Cooperation na hivyo kuwa mwanahisa mwenye nguvu kubwa zaidi ya kimaamuzi katika uendeshaji wa kampuni.

Pia Barrick ndio wahusika katika majadiliano yanayoendelea, nadhani ni Kutokana na hoja kwamba yeye ndio anabeba dhamana kubwa zaidi ya uendeshaji wa Acacia.

Kwa dhana hiyo ya kimaamuzi ni wazi kabisa hatua yeyote inayochukukiwa na Acacia bila shaka imepata baraka za Barrick, ambapo notisi hii ya kuanza kudai fidia imetolewa katikati ya ukimya mkubwa uliotawala katika majadiliano Kuhusu Makinikia.

Je hii Inaweza kuwa ndio ishara ya kuvunjika kwa majadiliano??.
inawezekana au yaweza kuwa kupitia màzungumzo yanayoendelea tumeishiwa pumzi,sasa wanatumià hiyo fursa kupata mshiko
 
Wachawi na wapiga ramli mwaka huu wana kazi kubwa kweli.

Tatizo la mwanasheria wa Chadema anafikiri nchi haina wanasheria, kasoma yeye peke yake, anadharau mpaka walimu wake,
Wanasheria inao ila why huwa wanashindwa kesi,juzi MASAMAKI amewabwaga,aliyekuwa MKURUGEBZI WA TANESCO amewashinda,hao wanasheroa wanashindaga kes zipi?

May Allah bless Me and You
 
Kwenye hili la ACACIA naona LISU ana maslahi
Kuliko waliosain MIKATABA?
Tusaidie pia tujue nani alikuwa na maslah na MV DSM,ununuzi wa bombadia usiopitia BUNGENI na dreamliner

May Allah bless Me and You
 
Wachawi na wapiga ramli mwaka huu wana kazi kubwa kweli.

Tatizo la mwanasheria wa Chadema anafikiri nchi haina wanasheria, kasoma yeye peke yake, anadharau mpaka walimu wake,

Halafu maadui wa nchi yetu sasa wanataka 'kumpepea' kisiasa eti 'MWANASIASA BORA KABISA WA AFRICA', DUH!
HEBU WAACHENI WALIOIFIA AFRICA WAPUMZIKE KWA AMANI!
 
Kawadharau Ki Vp? Hivi Yule Anaewaita Watanzania Ni Wapumbavu Na Malofa Yeye Halidharau Taifa? Nafikir Ingekuwa Bora Uje Na Hoja Ya Kupinga Kuonesha Jamaa Ni Muongo Kuliko Kuja Na Lawama.

1.Inawezekana ulofa wetu ndio unaona kuwa hajadharau?Kuitwa Lofa sio Tusi.

Wanasheria inao ila why huwa wanashindwa kesi,juzi MASAMAKI amewabwaga,aliyekuwa MKURUGEBZI WA TANESCO amewashinda,hao wanasheroa wanashindaga kes zipi?

May Allah bless Me and You

2.Hili swali alipaswa kuulizwa Lisu, Kumbuka hata JPM aliwauliza kwanini wananshindwa hata kesi za wazi kabisa.

mkuu, sijakusikia vizuri....unasema walimu?

nilipoingia UDSM miaka hiyo, kwenye intake hiyo hiyo nikakutana na ticha wangu wa O level. huyo ticha ali-disco first year. mimi denti wake nilipiga hadi miaka yote na upper second yangu juu!

nikagundua kitu...kumbe maticha wanaweza kuwa vilaza kuliko madenti wao?

embu nawe gundua kitu kati ya Lissu na waalimu wake....

3.Mkuu hapo sikuelewi, unawezaje kupata Upper second kwa kufundishwa na Kilaza?

Kosa lake ni lipi? Kusema anachokijua? Hao wanasheria wa Nchi hii walikuwa wapi wakati tunaweka mikataba ya unyonyaji kwa viongozi wetu wachache kulipwa kingi hizani? Lissu yeye alipigania haya miaka 20 iliyopita, leo analaumiwa kwa lipi?

Tuache unafiki!

4.Lissu ndio mnafiki kama alipigania miaka 20 iliyopita kitu gani kinamfanya apinge sasa? Si aungane na JPM badala kupingapinga na kuleta uchochezi wa kijinga, Tatizo anataka yeye aonekane anajua sana.
 
Wachawi na wapiga ramli mwaka huu wana kazi kubwa kweli.

Tatizo la mwanasheria wa Chadema anafikiri nchi haina wanasheria, kasoma yeye peke yake, anadharau mpaka walimu wake,[/QU
Wapo ila hawapo makini au wanapuuzwa wakishauri, tusingeikingia ktk mikataba mibovu ambayo imetugharimu kama Taifa kwa miaka mingi!
 
Wanasheria inao ila why huwa wanashindwa kesi,juzi MASAMAKI amewabwaga,aliyekuwa MKURUGEBZI WA TANESCO amewashinda,hao wanasheroa wanashindaga kes zipi?

May Allah bless Me and You
Tatizo sheria Tanzania ilisomwa na watu wajinga, watu waliokuwa hawawezi hata saba mara saba ndo wengi walikimbilia kusoma sheria, wachache waliokuwa na uwezo darasani wakaamua kusoma sheria wengi wameajiliwa private sector, kwa hiyo unaweza ona serekali imebaki na wanasheria wanamna gani, failed students, kwao kushindwa ni kawaida wala hawaoni ajabu, walikuwa wanashindwa darasani mpaka kwenye kesi wanaendelea kushindwa.
Halafu ili tatizo la wanasheria kushindwa ndo fashion hata huku private companies wakishtakiwa na mtu binafsi yaani kampuni ni kushindwa tu, mfano mdogo ni AY vs Tigo, huko Geita Gold Mining ndo usiseme kabisa yaani wanashindwa kila siku mpaka kuna wakili alifukuzwa kwa kushindwa kesi nyingi, wanasheria wa Bongo hakuna kitu, zamani UDSM ilikuwa inasifika kutoa best lawyers in East Africa, enzi hizo ya East Africa Community, lakini sasa hivi wanasoma failed students
 
  • Thanks
Reactions: SDG
3.Mkuu hapo sikuelewi, unawezaje kupata Upper second kwa kufundishwa na Kilaza?
mkuu, tulia nikufafanulie....
mwalimu wangu hakuwa ki-laza bali mimi nilikuwa na akili kumzidi.
ndivyo pia ilivyo kwa prof Kabudi (mwl wa Lissu)... huyu si ki-laza isipokuwa tu ana Lissu akili zaidi yake!
 
Serikali wanaidai barrick na IPO kwenye mazungumzo na barrick sasa hivi.
Haipo kwenye mazungumzo na acacia. Acacia wameporwa makinikia, issue ya makinikia IPO kwenye mdahalo kati ya serikali na mwenye mbwa, that is barrick. Usichanganywe akili na nyumbu hata siku moja, ni waongo, wezi, wanafiki.
Kwahiyo azam tv wametoa habari ya uongo? Je ni kwamba hiyo notice haija toka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sheria Tanzania ilisomwa na watu wajinga, watu waliokuwa hawawezi hata saba mara saba ndo wengi walikimbilia kusoma sheria, wachache waliokuwa na uwezo darasani wakaamua kusoma sheria wengi wameajiliwa private sector, kwa hiyo unaweza ona serekali imebaki na wanasheria wanamna gani, failed students, kwao kushindwa ni kawaida wala hawaoni ajabu, walikuwa wanashindwa darasani mpaka kwenye kesi wanaendelea kushindwa.
Halafu ili tatizo la wanasheria kushindwa ndo fashion hata huku private companies wakishtakiwa na mtu binafsi yaani kampuni ni kushindwa tu, mfano mdogo ni AY vs Tigo, huko Geita Gold Mining ndo usiseme kabisa yaani wanashindwa kila siku mpaka kuna wakili alifukuzwa kwa kushindwa kesi nyingi, wanasheria wa Bongo hakuna kitu, zamani UDSM ilikuwa inasifika kutoa best lawyers in East Africa, enzi hizo ya East Africa Community, lakini sasa hivi wanasoma failed students
Mie had napata shaka na wanasheria wa serikali kwakweli

May Allah bless Me and You
 
Back
Top Bottom