ACACIA kutoa notisi ya kuishitaki Tanzania na hatma ya majadiliano

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
Taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa TLS imeeleza kwamba kampuni kubwa ya Uchimbaji Madini, Acacia imetoa notisi ya kuishitaki Tanzania kwa lengo la kudai fidia ya hasara iliyotokana na zuio la Makanikia, kiasi cha takribani Trilioni 5 za kitanzania.

Acacia ni kampuni inayomilikiwa kwa zaidi ya asilimia 65 na kampuni ya Barrick Gold Cooperation na hivyo kuwa mwanahisa mwenye nguvu kubwa zaidi ya kimaamuzi katika uendeshaji wa kampuni.

Pia Barrick ndio wahusika katika majadiliano yanayoendelea, nadhani ni Kutokana na hoja kwamba yeye ndio anabeba dhamana kubwa zaidi ya uendeshaji wa Acacia.

Kwa dhana hiyo ya kimaamuzi ni wazi kabisa hatua yeyote inayochukukiwa na Acacia bila shaka imepata baraka za Barrick, ambapo notisi hii ya kuanza kudai fidia imetolewa katikati ya ukimya mkubwa uliotawala katika majadiliano Kuhusu Makinikia.

Je hii Inaweza kuwa ndio ishara ya kuvunjika kwa majadiliano??.
 
Wachawi na wapiga ramli mwaka huu wana kazi kubwa kweli.

Tatizo la mwanasheria Wa Chadema anafikiri nchi haina wanasheria, kasoma yeye peke yake, anadharau mpaka walimu wake, Nyambafu kabisa.
Yule fisadi mliyetuambia Mara mmekuta mamilioni ndani kwake, Mara ana nyumba 200. Anaitwa Masamaki wa TRA ilikuwaje DPP akaifuta kesi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maslahi ya upande mwingine/upande wa wazungu.
Hujajibu kwa vipi.

Mtu anaweza kuwakilisha maslahi ya upande wa Tanzania, akaisema serikali inavyoharibu, halafu mtu asiyejua kunyambulisha hoja, kwa kuwa hajui kunyambulisha hoja, akaona mambo kwa juu juu na kuhitimisha tu kwamba, kwa kuwa huu mtanange ukokati ya serikali na Acacia, na huyu Tundu Lissu anaisema vibaya serikali, basi huyu lazima atakuwa anawakilisha maslahi ya Acacia.

That is a non sequitur fallacy.

Ni kama umesema kwamba "Kwa kuwa wanaume hawana uwezowa kubeba mimba, na Doris hana uwezo wa kubeba mimba, basi Doris ni mwanamme".

It doesn't follow.

Umejihakikishiaje kwamba Tundu Lissu anawakilisha maslahi ya Acacia na si kwamba anawakilisha maslahi ya Tanzania kwa kuikosoa serikali ambayo haiwakilishi maslahi ya Tanzania vizuri?

Tundu Lissu alionya kuhusu hii mikataba ya serikali tangu enzi za Mkapa, akisema itatugharimu, kitu ambacho kimekubalika na serikali leo.

Kwa nini unasema anawakilisha maslahi ya Acacia?
 
Back
Top Bottom