ACACIA: Hatujafikia makubaliano yoyote ya kuilipa Tanzania

Kweli kutojua kingereza ni kazi na aibu...mleta mada kakurupuka bila kusoma na kuelewa hiyo taarifa ya Acacia...
Wao wameandika kuna negotiation imefanyika but Agreement ya nini kilipwe bado,,,AGREEMENT in makubaliano kwa kiswahili na NEGOTIATION ni majadiliano,,,so baada ya mazungumzo ya Leo bado hawajakubaliana kiasi cha kulipa na huo ndo ukweli maana bado uchunguzi wa pili unatakiwa ufanyike wakiwa na lengo moja pande zote mbili then ndo agreement or makubaliano ya kiasu gani kilipwe itoke,,,ndo maana Rais kasema itaundwa timu ya majadiliano or negotiation then waje na agreement,,,
Mleta mada kama kingereza ni kigumu basi hata wengi wanaokusaport hampishani ujinga
 
Acacia wao wabishi, ila hawana usemi juu ya Barrick wanaomiliki 63.9% ya Acacia.

Leo wamesema watatuma watu N.America.

Na serikali itajadiliana nao na si Acacia, wakae kimya hata waliyoandika ni kama yamekaa kidharau huku Barrick kwa website yao wameandika vizuri tu.

Lakini sina mnajua mgeni anatumia lugha gani, lazima pia kuwe na kiwango cha kuridhisha kujua tafsiri ya mazungumzo, vinginevyo kila mmoja atatoka na lake, wewe unaambiwa tuko tayari kulipa chochote mlichopoteza kulingana na mikataba yetu wewe unatoka ukirukaruka kuwa tunalipwa bila kujua umahiri tutakaotumia kujusty figures zetu!
Ni kweli kwenye vikao ndipo mbichi na mbinu zitajulikana, magufuli kabuni mladi wake kaja kwa style yake maana wenzake walivuna pesa nyingi huko Alianza mkapa akavuna madini mengi kisha jk akarekebisha sheria na yy akala chake na huyu kaja na mbinu zake ili na yy avune chake kwanza, watanzania ni baadae ingawa wanamuunga mkono wakiamini atawapa mgao.
 
Sentensi inasema "no agreements have been reached" ila wewe umeandika hakuna makubaliano ya kuwalipa yaliyofikiwa.Hapa kuna dhamira ya kuelekeza mitazamo kule unapotaka wewe.Kwanini usingesema hakuna makubaliano ya kukutanisha timu zijadili yaliyofikiwa!!
 
Hiyo barua imeandikwa na nani na rais kafanya mazungumzo na nani? Hata kusoma mmeshindwa?
Kama hujui uhusiano uliopo kati ya Barick na Acacia basi hufai kushiriki forum hii.

Kwahiyo Magufuli alipofanya mazungumzo na Barick aliyayafanya kwa ajili ana mgogoro na BARICK au ACACIA?
 
Kwenye PR au communications kuna kitu kinapata art of negotiations or persuasion. Kuna watu wazuri sana kwenye hii kitu na wengine ni wadhaifu. Makampuni mengi ya wazungu wanaofanya kazi globally huwa wana vitengo au watu wa kazi hiyo. Kwa kifupi ni walaghai na wanaweza fanya chochote kutimiza nia yao. Leo hii mdosi aliyekuja amebadili upepo kwa namna fulani. Wamepata Udhindi fulani. Share zao zimeanza kuimarika sokoni. J3 tulisema lazima watulipe leo j5 tumeishia kusema tutafanya nao mazungumzo ya kulipwa. Hapo sasa ndo wataalam wao wa negotiations na persuasion wanapoingia. Of course tutalipwa lakini chenga flani tutaliwa. Tusubiri tuonne
 
Hili swala ni confusing mara wamekubali kilipa mara wamekanusha??
Walikuja kumpooza mkuu bila kuahidi kulipa chochote isipokuwa kitakachukubalika baada ya majadiliano! Kama raisi alisema kitu kama hicho ni kwa sababu zakisiasa au yai lilikataa!
 
Kweli kutojua kingereza ni kazi na aibu...mleta mada kakurupuka bila kusoma na kuelewa hiyo taarifa ya Acacia...
Wao wameandika kuna negotiation imefanyika but Agreement ya nini kilipwe bado,,,AGREEMENT in makubaliano kwa kiswahili na NEGOTIATION ni majadiliano,,,so baada ya mazungumzo ya Leo bado hawajakubaliana kiasi cha kulipa na huo ndo ukweli maana bado uchunguzi wa pili unatakiwa ufanyike wakiwa na lengo moja pande zote mbili then ndo agreement or makubaliano ya kiasu gani kilipwe itoke,,,ndo maana Rais kasema itaundwa timu ya majadiliano or negotiation then waje na agreement,,,
Mleta mada kama kingereza ni kigumu basi hata wengi wanaokusaport hampishani ujinga
Makubaliano ya kulipa nini?
 
Sentensi inasema "no agreements have been reached" ila wewe umeandika hakuna makubaliano ya kuwalipa yaliyofikiwa.Hapa kuna dhamira ya kuelekeza mitazamo kule unapotaka wewe.Kwanini usingesema hakuna makubaliano ya kukutanisha timu zijadili yaliyofikiwa!!
" no agreements have been reached" kwa kiswahili " hakuna makubaliano yaliyofikiwa.
 
Back
Top Bottom