comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 8,839
- 6,573
Kampuni ya Indiana ilipewa lesesi ya kutafuta madini na kuanzisha mgodi. Ikafanya hivyo kwa gharama zake tena gharama kubwa.
Tanzania kama taifa tukatumia Resource nationalism bullying tukawafutia leseni bila kuwalipa fidia wala kurudisha gharama zao. Kwa maana nyingine tukapata mgodi bila kuingia gharama zozote za kutafuta mgodi.
Tunaishi kwenye dunia ya utawala bora tumepelekwa mbele ya sheria ili kila mwenye stahiki yake apewe.
Sheria imeelekeza turudishe gharama alizotumia Indiana kuyatafuta madini na mgodi. Sisi wenye eneo tumebaki na mgodi.
Katika mantiki hiyo hakuna upande uliopata hasara Indiana wamepata hela zao sisi tumepata mgodi. Ikiwa tuna uwezo wa kuchimba tuchimbe; kama hatuna tutamkodishia mtu mwenyeuwezo achimbe tutagawana fidia.
Kinachoshangaza ni kuona watu wanadhani tumepigwa ni wajinga wakielewa wataacha kwa sababu watakuwa wameelewa kwamba ni wajinga.
Pia soma
- Tanzania kuilipa Indiana Resources Ltd Bilioni 237 baada ya kuvunja mkataba mwaka 2018. Yatanguliza Bilioni 92