Ac katika gari

Ac katika gari

Baiskeli

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2010
Posts
335
Reaction score
61
wadau wa jf kwa wale wanaujua, air condition katika gari ni vipi inakuwa inaongeza ulaji wa mafuta? ni kweli? na inaongeza ulaji kwa kiasi gani maana ya tofauti? na kunanamna inawezakana kutumia ac bila kuongeza ulaji wa wese? naomba kufahamu.
 
Ebanaee ni kweli AC inaongeza ulaji wa mafuta ila hata mimi nimekuwa najiuliza bila kupata jibu, ila kuna siku katika utafiti wangu kujua ni kwanini ukiwasha ac mafuta yanatumika zaidi, nikafungua boneti ikiwa gari inaunguruma bila kuwasha ac ili nione injini inavyozunguka na baadaye nikawasha ac nikaona kuna lidude lingine linazunguka, kwahiyo nika conclude kwamba ukiwasha ac kuna midude miwili inazunguka lakini ukizima ac linazunguka moja tu, hii haikuweza kunisaidia kutoa scientific statement. nadhani wadau watatusaidia hapa
 
Ndugu ac inakula mafuta wala si ya kuhoji na mbaya zaidi gari nyingi ingine zake zimetengenezwa kwa minajili ya kukidhi hali ya hewa ya kwao japan,dubai sasa inapokuja na kukuta ni tofauti nduguu inakuwa double mkewangu alishakomaa na ahilo nikiweka alfukumi mafuta dotdys naenda na kurudi hme nikiwasha ac weeeeeee narudi na redlight nadhan unaijua kama yako green ndio hiyohiyo....ngoja tusubiri wataalamu watusasambulie inakuwaje
 
Kama gari lako lina tachometer (rev counter) wewe iangalie hiyo ndipo utakapopata majibu kwa haraka. Spidi ya engine ndiyo inayotoa mwongozo wa ulaji wa mafuta kwa sababu huashiria ni nishati kiasi inahitajika ichomwe ili kuweza kutoa nishati nyingine. Ukiwa katika mwendo kasi mdogo, matumizi ya kiyoyozi ndani ya gari huongeza ulaji wa mafuta kwa kiwangi kikubwa. The Impact of AC on fuel consumption at higher speeds say in excess of 80km/hr when the engine is already working hard seems to be less pronounced than at lower speeds.

Kwa kujaribu tu, washa gari lako kisha uangalie tachometer inavyosema with and without AC bila hata ya kuanza kutembea. Vitu vingine vinavyochangia ulaji wa mafuta vipo vingi tu kuanzia injectors, silencer ya gari, usafi (si wa macho) wa engine, suspension, vehicle height and mass, tyres etc.
 
hiyo tachometer inakaa wapi kwenye gari, sehemu gani?
 
hiyo tachometer inakaa wapi kwenye gari, sehemu gani?

Kwenye magari ya kisasa ni pembeni na speedometer. Inaonyesha engine speed in revolutions per minute. Kwa gari ya Diesel mara nyingi huwa ni kati ya 1 mpaka 6 x1000 rpms na kwa ya petroli zaidi.
 
Air conditioner inapopoza kuna sehemu zake zinazungushwa - yaani nishati ya kuzizingusha sharti iwepo. Ni budi mafuta zaidi yatumike kukithi hitaji hilo.
 
Back
Top Bottom