Abtali Mwerevu, Mtu mwema, Makini na Mwaminifu Kupitiliza

Abtali Mwerevu, Mtu mwema, Makini na Mwaminifu Kupitiliza

Abtali Mwerevu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
773
Reaction score
668
Nimekuwa nikiitumia JamiiForums tangu inaanza. Kwanza niliitumia kawaida bila kujiunga, mpaka nilipoamua kujiunga rasmi mwaka 2013. Kila ninapoingia mtandaoni mtandao wangu wa kwanza ni JamiiForums. Mara zote nilipoingia, nilikuta habari za watu wengine mpaka hii leo nilipoingia na kukuta tuhuma juu yangu. Habari imeletwa na member aitwaye "Manfried ", anadai ninatangaza ajira za utapeli, na nimetapeli watu katika mtandao wa WhatsApp. Manfried anaenda mbali zaidi kwa kuomba nipewe 'life ban'.

Habari hizi ni uongo mkubwa! Hakuna mtu aliyetapeliwa, ndiyo sababu 'Manfried' hatoi ushahidi wowote wala haelezi kwa kina alivyotapeliwa.

Huu ni uongo, lakini kwa nini nisingiziwe? Zipo sababu mbili:

Sababu ya kwanza haijulikani. Anajua mleta mada mwenyewe!

Sababu ya pili ni nadharia tu:

Nitafafanua sababu ya pili:

Katika matangazo niliyoweka, niliweka vigezo vya miaka, nilisema, anatakiwa kijana aliyehitimu 2024 na 2025, pengine wasio na sifa hizi walikasirika kwa kuona wamewekwa pembeni. Hili lina ushahidi, malalamiko mengi katika tangazo yalikuwa katika kigezo cha miaka, nilieleza sababu ya kufanya hivyo. Hata hivyo, wakongwe walinishambulia sana. Wakongwe wana hasira na waliona wametengwa!

Huko WhatsApp nilipokuwa napokea sifa za waombaji, kuna waombaji niliwaeleza hawana sifa zinazotakiwa. Pengine walikasirika na kuamua kuzusha jambo.

Wapo waliofika pengine hawakufurahishwa na utaratibu. Utaratibu wa 'probation', kwamba ufanye kazi miezi mitatu chini ya uangalizi, utapewa nauli na chakula, baada ya miezi mitatu ya uangalizi, malipo kamili yataanza.

Niwaombe vijana mlionitumia jumbe zenu wakati wowote niliotangaza kazi, nikawapokea katika centre yangu Kinondoni Mtaa wa Kambangwa mkabala na serikali ya Mtaa pembezoni mwa Hotel De Mag, mje kunitetea... yule mtu mcheshi mliyekutana naye, akawafanyia interview akitabasamu, ile sura isiyo na hatia, anaitwa tapeli! Pazeni sauti zetu, hata mkiwa wawili inatosha!

Katika tangazo nililoweka, nilipata vijana wawili, wakike na wakiume wapo wanaendelea vyema na kazi. Nilihitaji vijana wanne, wamebaki wawili, hata hivyo sina nguvu za kutangaza tena!

Kwa mazingira hayo, hakuna utapeli, kuna watu waliomba mwaka jana, juzi na wanafanyakazi mpaka leo. Tutafute jina jingine.

Endapo Manfried ataachwa tu hivihivi bila kuchukuliwa hatua, itanipa mashaka juu ya usalama wa kuwa humu JF, kwamba mtu akuzushie jambo, halafu aachwe tu... siamini kama JF itamuacha hivihivi.

Hakika ni ajabu ya mwaka, 'member' asiyefikisha hata mwaka mmoja wa kuwa jukwaani, kamzushia mkongwe jukwaani mwenye zaidi ya miaka 12. Hata hivyo, aminini... IMETOKEA.
 
"Utaratibu wa 'probation', kwamba ufanye kazi miezi mitatu chini ya uangalizi, utapewa nauli na chakula, baada ya miezi mitatu ya uangalizi, malipo kamili yataanza."

Acha longolongo. Lipa watu. Kama hauko tayari kuajiri fanya kazi peke yako au na wanafamilia yako kwanza BADALA YA KUTUMIKISHA WATU KIJINGA KISA HAWANA AJIRA.
 
Hayo nimasharti yake ,ni vema amesema mapema kuliko kudanganya, mi nikutakie kila raheli kwenye biashara yako
 
"Utaratibu wa 'probation', kwamba ufanye kazi miezi mitatu chini ya uangalizi, utapewa nauli na chakula, baada ya miezi mitatu ya uangalizi, malipo kamili yataanza."

Acha longolongo. Lipa watu. Kama hauko tayari kuajiri fanya kazi peke yako au na wanafamilia yako kwanza BADALA YA KUTUMIKISHA WATU KIJINGA KISA HAWANA AJIRA.
Hv maana ya uko chini ya uangalizi, s wanaona perfomance yako ili hali unapewa huduma zote kama mfanyakazi ikiwemo mshahara, baada ya probation ndo wataangalia wanakupa mkataba ama la, dah.
 
Matapeli mara nyingi Wana maneno mengiiiiii! Nadhan nimeeleweka😄
Screenshot_20240915-175409_1.jpg
 
Back
Top Bottom