Abiy Ahmed: Jeshi la Ethiopia limechukua udhibiti wa Mekele

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema majeshi ya nchi hiyo yamechukua udhibiti wa mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle.

Tigray-Konflikt | Militär Äthiopien

Abiy ametangaza kuwa serikali ya shirikisho sasa imechukua udhibiti kamili wa mji huo ikiwemo uwanja wa ndege, taasisi za umma, ofisi za utawala wa jimbo hilo na maeneo mengine muhimu.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Twitter siku ya Jumamosi, Abiy ametangaza pia kuwa wamemaliza operesheni yao ya kijeshi katika jimbo hilo.
Abiy ameongeza pia kuwa maelfu ya wanajeshi ambao walikamatwa na wapiganaji wa chama tawala katika jimbo hilo ‘Tigray People's Liberation Front'- TPLF, yaani Chama cha Ukombozi wa Watigray pia wameachiliwa huru. Chama cha TPLF kimekuwa madarakani katika jimbo hilo la kaskazini mwa Ethiopia.

Serikali ya Ethiopia ilianzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya TPLF zaidi ya wiki tatu zilizopita kwa lengo la kuwaondoa madarakani.
Mkuu wa majeshi nchini Ethiopia, Jenerali Birhanu Jula Gelalcha

Awali, ripoti katika shirika la habari linalohusishwa na serikali ya jimbo hilo zilisema mji wa Mekelle ulishambuliwa kwa makombora mazito.
Hata hivyo, jopo-kazi lililoundwa na serikali kuu kufuatilia mzozo wa Tigray, limesema hayo ni madai ya uwongo ambayo yanaenezwa na TPLF kwamba serikali serikali kuu imefanya mashambulizi dhidi ya miji na maeneo ya makaazi ya raia.

Kulingana na tarifa ya serikali kuu, vikosi vya serikali vinalenga tu maghala ya silaha za kijeshi ya TPLF na kwamba wanajeshi wa serikali ya shirikisho hawajafanya mashambulizi yoyote dhidi ya miundo mbinu muhimu za raia kama hospital, shule au maeneo ya makaazi.

Taarifa hiyo imeongeza zaidi kuwa wanajeshi wa vikosi vya serikali havijafanya mashambulizi katika maeneo yenye watu wengi.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Mnamo Jumamosi, mkuu wa majeshi wa Ethiopia Jenerali Berhanu Jula alisema baada ya vikosi vyake kuchukua udhibiti kamili wa mji wa Mekelle, sasa wanawasaka wapiganaji wa TPLF wanakojificha.

Hakukuwa na jibu la moja kwa moja kutoka upande wa TPLF.

Machafuko ya jimbo la Tigray yalianza mapema mwezi huu wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2019, alipoviamrisha vikosi vyake kuanza operesheni kwa lengo la kuuondoa uongozi wa jimbo la Tigray.

Chama cha TPLF kimetawala siasa za Ethiopia kwa miaka mingi, lakini tangu Abiy Ahmed alipochukua madaraka mnamo mwaka 2018, amekuwa na msuguano na viongozi wa Tigray.
Pande zote mbili zimeripoti kuhusu mauaji lakini kufuatia kuzimwa kwa intaneti pamoja na huduma za mawasiliano ya simu kukatizwa, imekuwa vigumu kupata tarifa kamili ya vifo kuhusiana na machafuko hayo ya Tigray, ikiwa ni pamoja na mashambulizi kadhaa ya angani na kisa kimoja cha mauaji ya halaiki ambapo mamia ya watu waliuawa.
Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa na zaidi ya Waethiopia 40,000 wamekimbia vita na kuingia Sudan.
 
Hatimaye Vita vimefika tamati, Sasa waweke mazingira mazuri ili waliokkwalio warudi nyumbani.

Vipi kuhusu hatma ya utawala wa hilo jimbo? Ina maana watakuwa chini ya udhibiti wa serikali kuu na hawataruhusiwa kuwa na utawala wa ndani tena?
 
Hongera kwa Serikali ya Ethiopia kwa ushindi huo!
 
Hatimaye Vita vimefika tamati, Sasa waweke mazingira mazuri ili waliokkwalio warudi nyumbani.

Vipi kuhusu hatma ya utawala wa hilo jimbo? Ina maana watakuwa chini ya udhibiti wa serikali kuu na hawataruhusiwa kuwa na utawala wa ndani tena?
walishaunda serikali ya mpito kusimamia kwa muda uchaguzi utaitishwa tena baadae hilo jimbo lilikaidi kusitisha uchaguzi kipindi icha korona likfanya uchaguzi kivyake kwaiyo uchaguzi utarudiwa tena.
 
Hatimaye Vita vimefika tamati, Sasa waweke mazingira mazuri ili waliokkwalio warudi nyumbani.

Vipi kuhusu hatma ya utawala wa hilo jimbo? Ina maana watakuwa chini ya udhibiti wa serikali kuu na hawataruhusiwa kuwa na utawala wa ndani tena?
Huo utawala wa ndani wa Majimbo ndio ulioleta shida, kama alivyokua anataka mbelgiji mmoja hivi huku kwetu
 
Sio kweli acha kupotosha.

Shida ni chama cha TPLF kuasi serikali kuu, majimbo mengine hayakuasi ndio maana hayajawa na mgogoro na serikali kuu.
 
Vipi kuhusu hatma ya utawala wa hilo jimbo? Ina maana watakuwa chini ya udhibiti wa serikali kuu na hawataruhusiwa kuwa na utawala wa ndani tena?
PM Abiy kasema Waco wanasaka sasa na watawadaka tu. Kwa sasa hakuna movements in and out of the Region zipo controlled na Federal forces
 
Back
Top Bottom