Abiria wampa kipigo dereva,wasema tusisubiri serikali hata sisi tunaweza wafundisha adabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abiria wampa kipigo dereva,wasema tusisubiri serikali hata sisi tunaweza wafundisha adabu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mirindimo, Jun 11, 2012.

 1. mirindimo

  mirindimo JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 60
  Midaa ya saa mbili usiku gari yenye usajiri T 633 BSS inayofanya route za mbezi kawe lakini wakati huo ikitokea magomeni ambapo konda wake alidai wamekwenda kujaza mafuta,lakini ndani ya gari kuna abiria akasema katoka nahiyo gari kinondoni....!

  Hapo ndipo abiria walichefuka kwani konda huyo alisema yeye anaishia ubungo tu na anaenda kawe kulaza gari na abiria walipanda gari hiyo wakijua inaenda mbezi...alipofika ubungo aliingia sheri na kuwataka abiria wote washuke bila mafanikio,aligeuza gari nakuelekea darajani ambapo konda alianza kupiga debe la kawe ndipo abiria wakafunga mlango na kuchomoa funguo huku wakimpa dereva vibao vya maana na wakiwa na hasira kali,wakasema tumechoka kuonewa kila siku na hatutaki askari kwani hamuwaogopi kwa sababu mnawapa hongo kila siku sasa unatupeleka mbezi ama tunakushughulikia sisi wenyewe!

  Dereva alitaka kushuka akavutwa kurudi ndani na mlango wake na dirisha vikafungwa huku akikamatwa shati na mkaka alieshiba.....baada ya ugomvi huo aligeuza na kupeleka abiria mbezi..!

  Wana jamvi wenzangu tatizo hili ni sugu na hasa wakati wa jioni madereva wanajiamulia kufanya chochote na nauli yoyote tena wakati mwingine anaweza asipakie abiria akawapita mmesimama, abiria tusiokua na magari binafsi tunateseka sana, hata wakati wa asubuhi pia hulazimika kuzunguka na gari na kulipa nauli mara mbili zaidi ya kawaida.....watanzania tusione hii kitu ni ya kawaida hapana we don't deserve this, let's join our power and say its over, together we can make this city a better place for everyone! Nashindwa kuelezea kile nnachosikia moyoni mwangu lakini wanaopata hizi taabu ni watabaka la kawaida na chini ,maisha ni magumu.

  Basi tunaomba tuboreshewe huduma zingine jamani angalau zitufariji au kwa sababu magari ni ya kwenu mnaojiita vigogo ? Ipo siku yatakwisha na siku hiyo naingoja kwa hamu sana! Ningekua na Rifle ningemshoot yule konda na dereva.....! Kwanza wale ni deiwaka manake hata uniform hawakua nazo na luga wanazoongea za kihuni tu....acha niishie hapa....!
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa ni kwa nini uunge mkono wananchi kuchukua sheria mkononi?
   
 3. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Uhuru HALISI wa watu utaletwa na watu wenyewe.
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kwa kuwa siku hizi hupandi daladala ndio maana unasema hivyo,ulipokua mwembechai hukusema hivyo
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Mwendo huu ni mzuri sana,kama serikaki ya CCM imeshindwa nguvu ya umma inaweza
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu, madereva na makonda ni binadamu kama ulivyo wewe na mimi, wanakosea na wana udhaifu wao pia. Inawezekana vipi mtu asherehekee abiria kuwapiga ilihali wapo kazini? kwani sheria zinasemaje dereva akitaka kubadili route? APIGWE?

  Mkuu ninachopinga ni wananchi kujichukulia sheria mkononi,kisha anatokea mtu anshabikia! Hii haikubaliki hata kidogo ni lazima watu wawe wastaarabu.
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  uislam unasema jambo baya likataze kwa mkono,ikishindikana kwa mdomo,hatimaye lichukie moyoni!watanzania tumekua tunarukia hatua ya pili badala ya kwanza
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  aliekata route amechukua sheria mguuni????
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  na kuchukia kwa moyo ni UDHAIFU WA IMAN,,,,,
   
 10. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hameni huko karibuni huku mikoani nako kuna maisha wananchi wenzangu
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  kwa sababu serikali ya ccm mliyoichagua nyie cuf na ccm imeshindwa
   
 12. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nd. Tume tunaopanda daladala ni binadamu kama madereva. Kawaida ya binadamu mwenye akili timamu ni kutafuta ufumbuzi muafaka wa matatizo yake, ikiwemo kubadilisha mbinu kama inalazimu. Haiwezekani unyanyaswe na dereva tangu chekechea, chuo hadi kazini. Miaka yote hiyo Trafiki na sheria vipo lakini hali inazidi kuwa mbaya tu
   
 13. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Comrade umenifurahisha sana kwa kumpatia mkuu jibu hili Murua kabisa hakika limemtosheleza kabisa
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  Hapa ndio muone umuhimu wa mabasi ya UDA.
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu ntake radhi, mimi siisupport CCM hata kidogo.
   
 16. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kwa uelewa wako ndugu yangu ni sahihi , abiria kumpiga dereva? wa sheria ipi? Nyie CHADEMA mbona mnapenda vurugu sana? kwa nini hamtaki sheria kuchukua mkondo wake?
   
 17. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kuna thread moja humu JF, Huyu jamaa aliunga mkono Al shabab kuwaua mawaziri wale wa kenya. Sasa hii moral authority ya kujifanya muungwana hapa ameipata wapi?
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama waliojariwa kuchukuwa hatua hawafanyi hivyo basi somebody is will, and today they didi exactly that!
   
 19. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  mmmmmhh haya
   
 20. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu FJM, nakuheshimu sana. Tafadhari futa post yako. Haiwezekani uunge mkono uvunjaji wa sheria kiasi kile!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...