Abiria wampa kipigo dereva,wasema tusisubiri serikali hata sisi tunaweza wafundisha adabu

Real kwa wasio panda daladala hawawezi ona haya! Hawa madereva wanatunyanyasa nyakati za jioni na mornie na wanajipangia nauli wanayotaka!
 
Mkuu wangu, madereva na makonda ni binadamu kama ulivyo wewe na mimi, wanakosea na wana udhaifu wao pia. Inawezekana vipi mtu asherehekee abiria kuwapiga ilihali wapo kazini? kwani sheria zinasemaje dereva akitaka kubadili route? APIGWE?

Mkuu ninachopinga ni wananchi kujichukulia sheria mkononi,kisha anatokea mtu anshabikia! Hii haikubaliki hata kidogo ni lazima watu wawe wastaarabu.

Mkuu na huo ni mwanzo tu kuna siku utasikia daladala limechomwa moto....matarfiki hawajigusi kabisa kwa sababu wanapewa elfu kumi kumi na wanapiga kimya wananchi taabikeni mpaka mtie adabu haiwahusu kama sio watanzania kabisa..........huezi jua adha iliyopo mpaka siku uache gari lako huko kimanzi chana uje na daladala utaelewa namaana gani.
 
Real kwa wasio panda daladala hawawezi ona haya! Hawa madereva wanatunyanyasa nyakati za jioni na mornie na wanajipangia nauli wanayotaka!
 
Hiyo nimeipenda.

Kwa jinsi maisha yanavozidi kuwa magumu, kuna cku kabisa ambapo kila mtu anayehujumu wengine ktk nchi hii wakiwemo viongozi wetu watakuna na nguvu ya umma.

Kwani vibaka walianzaje kuchomwa??? Ni kwa mwendo huu huu ambao mamlaka husika zinashindwa chukua hatua stahili na kuacha jamii ikiathirika.

Uvumilivu una mwisho wake na ndo huo unaokuja.
 
Mkuu wangu, madereva na makonda ni binadamu kama ulivyo wewe na mimi, wanakosea na wana udhaifu wao pia. Inawezekana vipi mtu asherehekee abiria kuwapiga ilihali wapo kazini? kwani sheria zinasemaje dereva akitaka kubadili route? APIGWE?

Mkuu ninachopinga ni wananchi kujichukulia sheria mkononi,kisha anatokea mtu anshabikia! Hii haikubaliki hata kidogo ni lazima watu wawe wastaarabu.
:majani7: :majani7:



Abiria ni binadamu pia, nao wanakosea wakati mwingine, na katika mazingira hayo yaliyotokea dereva kakutana na abiria waliochoka baada ya siku ngumu ya kutafuta ugali wa watoto hivyo kuteleza na kumchapa dereva ili kesho akumbuke anadeal na binadamu wenzake, hivyo mshauri dereva afwate sheria na kupeleka basi kituo cha polisi akaelezee jinsi alivyokatisha kufwata route yake na kutandikwa vibao na abiria waliochukizwa na kitendo chake hicho, then sheria ichukue mkondo wake, otherwise asikatishe route na yote hayo hayatamkuta.
 
Kwa hiyo kwa uelewa wako ndugu yangu ni sahihi , abiria kumpiga dereva? wa sheria ipi? Nyie CHADEMA mbona mnapenda vurugu sana? kwa nini hamtaki sheria kuchukua mkondo wake?

Tatizo la madereva wa daladala na tatizohili la kukata route wakati mwingine kuwa wakali kwao like this ukitegemea sheria kuchukua mkondo kwa maana ya Trafik kuwashughulikia,basi usitegemee loloet. Tatizo hili sugu sana kama una usafiri binafsi siku moja jioni ama asbh simama kituo cha daladala utaona gari ya Kinyerezi mathalani kutokea Ubungo,wanatangaza Segerea mwisho! segerea mwisho!
 
Nafuu amekutana na abiria wenye huruma yaani wangekuwa raia wakitaa chetu wangemchoma moto
 
Kuna siku (niliisikia hii story Power Breackfast) hivyohivyo mida ya usiku kama saa 3 hivi daladala la Ubungo Mbezi tena nasikia ilikuwa ile mi'bus mikubwa limesimama Ubungo konda anapigia debe Kimara,siku hiyo nasikia magari ya Mbezi yalikuwa adimu sana,abiria wa Mbezi kibao pale kituoni si wakaamua kupanda hivyoX2 konda kachukua nauli wamefika Kimara dereva kaligeuza kweli wakaanza kurudi Mjini,abiria walimvyomfata dereva akawatishia kuingiza bus mtaroni,hapo basi lipo kwenye mwendo mkali vibaya mno,dereva anakanyaga mafuta huku anachimba mkwara akiguswa amelibwaga,maskini abiria wale ikabidi wawe wapole,dereva anachochea tu,kufika Ubungo walitegemea ange'park ili kama vipi ndo wampige waapi wakiwa wanateremka kwenye mataa ya ubungo si kijani ya kunyoosha na kukunja ikawaka akalala nayo kulia,mpelampela unaambiwa Mandela road sasa hiyo. abiria wote roho mkononi,kufika external akalikunja tena kulia mpelampela kwenye rough road hivyohivyo mpaka Pori gani sijui huko akali'park akateremka mbio,hiyo sasa ilikuwa mida ya saa 5 unaambiwa,ikabidi abiria wam'tight konda,dakika chache likaibuka kundi la vijana na magongo/fimbo(kumbe mitaa ile ndo anayokaa dereva,kwahiyo alienda kuwaita wavuta bangi wenzake wakataka kuwachapa abiria,abiria na wenyewe wakakomaa wakiguswa wanalipiga moto basi ukichukulia miongoni mwao kulikuwa na wavuta fegi wasingekosa viberiti basi unaambiwa mzozo mkubwa ukatokea pale porini,bahati nzuri abiria mmoja alikuwa na namba za Bonge wa Clouds akampigia,bonge ndo akaenda pale na deffender ya polisi wakam'tight Konda akawapeleka kwa dereva wakamchukua wakamlazimisha apeleke abiria Mbezi under escort kisha akarudisha gari polisi na yeye kuhifadhiwa,sijui walimalizaje kesi ile ila abiria wa Mbezi siku ile walifika makwao saa 8 usiku.
My Take:
Kiukweli watumiaji wa usafiri wa daladala huwa wanateseka sana nyakati za asubuhi na jioni,hata kesi inapofikishwaga mbele ya sheria mathalani Polisi huwa inamalizwaga kiaina sana ksbb Jamaa huwa wanawatoa buku 2,2,5,5 dawa ni kuchukua hatua kama ile iliyochukuliwa na abiria wale walioelezewa na mtoa mada,big up kwao sana,matukio ya namna hii yakiwa yanatokea mara kwa mara watatia nidhamu.
 
Mkuu wangu, madereva na makonda ni binadamu kama ulivyo wewe na mimi, wanakosea na wana udhaifu wao pia. Inawezekana vipi mtu asherehekee abiria kuwapiga ilihali wapo kazini? kwani sheria zinasemaje dereva akitaka kubadili route? APIGWE?

Mkuu ninachopinga ni wananchi kujichukulia sheria mkononi,kisha anatokea mtu anshabikia! Hii haikubaliki hata kidogo ni lazima watu wawe wastaarabu.

Mkuu hawa wahudumu wa madaladala wamezidi hii tabia,

Ukiwashitaki kwa Trafiki barabarani ni sawa na kumpelekea Askari chakula cha jioni kwani hakuna kitakachoendelea na hata madereva wanalijua hili.

Tena wanakuonyesha na Askari "Yule nenda kamwambie" Anajua kuwa hatomfanya chochote.

Hii Tabia imezidi kwa Route ya Ubungo - Tegeta, Mwenge - Bunju, Mwenge - Posta, Mwenge - Kariakoo, Posta - Mbezi n.k

Muda wao wa kufanya hivi ni Jioni na Asubuhi.

Hivyo kama Askari wanakula pesa na hawafanyi kazi tunaoumia ni sisi abiria.

CHUKUA SHERIA MKONONI INAPOBIDI, NI JAMBO LA KAWAIDA KWA WASHENZI KAMA HAWA!!!!!!



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom