Abiria wa Mwenge Posta

Abiria wa Mwenge Posta

supermario

Member
Joined
Dec 2, 2011
Posts
48
Reaction score
15
Ukifika kituoni Mwenge hususani wakati wa asubuhi yanapokuja mabasi ya kwenda Posta unaona jinsi watu wanavyo kimbilia ili kupata nafasi za kukaa. Cha kushangaza zaidi ni wale abiria wanaokuwa wa kwanza kugombania siti alafu anashuka Bamaga, Sayansi, Makumbusho, Victoria na wengine hata ITV.

Kwa nini wasipande mabasi yaendayo kariakoo, temeke, mbagala maana yote hupitia katika vituo hivyo na huwa hayana usumbufu kutokana na kuwa mengi.

Yani fujo zote za kuwahi siti na kukaa mwisho alafu unashuka bamaga? sababu ni nini ati?
 
Jukwaa la Siasa !??!!??? Jamvi la Politic.. ??!!? Mbona tumevamiwa..!

Angalia vizuri...Hapa tuko jukwaa la habari mchanganyiko au general forums..!
Halafu unasema 'mbona mmevamiwa?'kwani una haki miliki na JF?? Tusipende kujiona bora kuliko wengine, JF ni jukwaa huru alimradi tu huvunji sheria na kanuni zake
 
Binafsi nawapenda kwa mazoezi wanayofanya ya kugombea daladala, lazima wakimbie tu huko na huko
 
huku Ntwara han-na hiyo japo kuna ruti ya Mwenge-Posta kama huko Dar.
 
Mimi wanaonifurahisha ni wale wa mbagala manake wao wanapita madirishani haijalishi ni mwanamke au mwanaume wote wamoja
 
Wezi hao!!

Mtanzania mwenye utajiri wa hajabu davis mosha by le mutuz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom