Abiria kuibiwa uwanja wa ndege J. K. Nyerere, Tanzania; tunatoa picha gani kwa dunia?

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
512
147
Kwa mudamrefu nimekuwa nikitafakari yanayojiri pale uwanja wa ndege wa Mwl. Julius K. nyerere hususan abiria wanaokuja kuibiwa mizigo yao. Imefikia hatua ya abiria kutobeba au kununua vitu vya thamani na kuweka kwenye masanduku ambayo yanapakiwa kwenye buti la ndege husika. Kama inavyofahamika, abiria anapopakia ndege popote pale duniani anakabidhi masanduku yake kwa wahudumu na abiria huyo atakutana na sanduku lake mwisho wa safari (kama Uwanja wa ndege wa KIA au Dar). Kinachonishangaza ni kuwa masanduku hayo yanapopokelewa na mhusika Dar, anakuta vitu vya thamani vimeshachukuliwa na abiria kubaki akisikitika kwa wizi huu. Na hata kama umefunga kufuli mara nyingi kufuli inavunjwa, japo tunaambiwa inavunjwa wakati wa ukaguzi kwa ajili ya usalama.

Maswali yanayojitokeza hapa ni kuwa je, hakuna security yoyote uwanja wa ndege? Mbona kuna security camera nyingi sana kiasi kwamba huwezi kufanya jambo lolote usionekane? Kama kuna security camera, je uongozi wa uwanja wa ndege unachukua hatua gani kuwadhibiti wafanyakazi kupekua masanduku nakuwaibia abiria? Au viongozi nao ni sehemu ya ufisadi huu na wanafaidika na wizi huu? Serikali yetu inachukua hatua gani kushughulikia tatizo hili? Je abiria akienda kulalamikia uongozi wa uwanja wa ndege atasikilizwa?

Je, hali hii inatoa picha gani ya Tanzania kwa mataifa ya nje? Wadau naomba tuchangie mada hii kwani linatia uchungu sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom