Abiria Chunga Mzigo wako na Haki zako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abiria Chunga Mzigo wako na Haki zako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shy, Jun 13, 2010.

 1. Shy

  Shy JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,238
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Nilipanda basi ya Ngorika asubuhi ya saa 12 Kituo cha mabasi ubungo kuelekea Arusha , Lilikuwa ni Ngorika la pili , Kila mtu alitaka kuwahi kupanda gari hilo kwasababu ni kati ya yale yanayowahi zaidi kuondoa kituo cha ubungo kuelekea Arusha na Moshi kila siku .

  Basi lilipoanza kuondoka kutoka nje mtu Abiria mmoja akaingizwa kwenye gari na Mkata tiketi ambaye hakuwa mwajiriwa wa basi lile akapelekwa mpaka nyuma ya gari akapewa sehemu ya kukaa alilipa hela na kupewa tiketi akaambiwa ataletewa chenji yake .

  Mara gari ikawa inaondoka kufika mataa likasimama Yule mkata tiketi akashuka akamwacha abiria wa watu na tiketi yake , simulizi ya mkata tiketi ikaishia hapo hapo basi likawa kimya na tayari kwa safari .

  Kufika Mbezi mkaguzi wa tiketi akaanza kupita kumfikia Yule mzee ,akaambiwa kilichotokea na ndio akaanza kudai chenji yake mkaguzi akamwabia sio yeye aliyempa tiketi hiyo kwahiyo hawezi kumshugulikia mara moja .

  Mimi nilikuwa mbele kidogo ya abiria huyo nikamwambia apige namba ya simu iliyowekwa kwenye tiketi za basi hilo alivyopiga na kusema kisa chake tu wale jamaa wakamwabia hawahusiki awasiliane na walio kwenye basi hilo .

  Baada ya majibu hayo nikamwambia akifika kibaha ashuke na kwenda kulipoti kwa askari wa usalama barabarani na kweli tulipofika pale lakini kwanza akaongea na utingo , dereva pamoja na kondakta na Yule mkaguzi wao wa basi lakini majibu yao yalikuwa yale yale kukataa .

  Wakati majibizano hayo yakiendelea mimi nilishuka kwenye gari na kuanza kuwapiga picha pamoja na kuchukuwa picha za basi hilo haswa namba za gari , wale utingo na konda kuona vile wakaja kunikaba nikaulizwa kwa nini napiga picha na kama ni mwandishi wa habari nionyeshe kitambulisho changu halafu wakaanza kunipeleka kituo cha polisi pale kibaha kwa kupiga picha tukio lile .

  Hatukufika kituo cha polisi mbele kidogo tukakutana na askari mwingine akatusimamisha nikamweleza kilichotokea askari akaamuru nirudi ndani ya gari tuendelee na safari hapo hawakufanikiwa kuchukuwa kamera yangu wala kuniumiza nilijitahidi kuzuia jitihada zote za wao kufanya jaribio hilo .

  Safari ikaendelea kufika mbele kidogo wakataka tena nifute picha au waje kuchukuwa kamera hiyo na kuivunja huku abiria wengi ndani ya basi wakinipigia kelele niache ubishi nifute picha na kuwaonyesha kweli nimefuta picha halafu niende mbele kuwaonyesha konda na dereva kwamba kweli nimefuta .

  Sikufanya hivyo badala yake nilibadilisha memory card ile niliyopiga hizo picha na kuweka nyingine ambayo ilikuwa tupu na kumpa jirani yangu kwenye basi ashike , tulipifika chalinze wakasimamisha gari na mmoja akashuka kwenda kutoa cha polisi chalinze kutoa taarifa kwa kile nilichofanya .

  Mwingine akawa ndani ya gari akatishia kuniadhibu nakumbuka alirusha ngumi kama 3 hivi lakini nilimkwepa na kuendelea na msimamo wangu sitoi kamera kwao wala picha sifuti waende polisi kama walivyoahidi .

  Tulibishana kwa dakika kama 15 ndani ya basi mpaka polisi alivyokuja kunichukuwa ndani ya basi na kamera yangu kufika kule nikapekuliwa nikavuliwa viatu na mkanda wa suruani kisha nikapewa amri ya kukaa chini huku wakisikiliza maelezo ya Yule jamaa wa basi .

  Walivyomaliza kusikiliza maelezo yao nikaulizwa kwanini nilifanya vile nikawaambia tu nimeamua kuchukuwa picha zile kutokana na tukio lilitokea na nina haki zote za kupiga picha au kuchukuwa picha za tukio lolote kama raia kamili wa watanzania .

  Nikaendelea kuwaambia Tunatakiwa kuweka kumbukumbu ya vitu vinavyoendelea njiani kwa ajili yao polisi kama chochote kitatokea kama hivyo na mambo mengine mengine mengi ya kiusalama ile ilikuwa ni kumbukumbu tu nikaomba waniambie kama kuweka kumbukumbu ni kosa .

  Baada ya mazungumzo ya muda kidogo nikaombwa niwape kamera askari waangalie kamera yangu kama kweli picha zilikwepo nikawapa walipoangalia hawakukuta picha yoyote wala chochote , nikatoa vitu vyote nilivyokuwa navyo mfukoni hawakukuta chochote .

  Nikaambiwa niende kwenye gari na siku nyingine likitokea tukio kama hilo niwasiliane nao moja kwa moja nisianzie malumbano kwenye vyombo vya usafiri nikarudi kwenye gari kuendelea na safari .

  Kuanzia hapo basi letu likawa linakaguliwa kwa kuingiliwa na polisi wa usalama barabarani kila linapofika kituoni na kuuliza maswali abiria kama kuna tatizo lolote limetokea .

  Lilikuwa fundisho Sikuhiyo nilivyorudi kwenye gari kila mtu alinishukuru kwa uamuzi niliouchukuwa na likawa funzo kwa dereva na konda wa basi lile kwasababu njiani kote walikuwa na heshima .

  Ni vizuri abiria wajifunze kutetea haki zao na za wengine endapo wataona zinachezewa kwa makusudi , kama ukizarau siku itamkuta mtoto wako au hata ndugu yako akakosa mambo ya muhimu kwenye maisha yake na kazi zake zingine
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,509
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Unaona askari wetu walivyo wapungufu wa kuelewa,,,,sasa hapo mwenye kosa ninani...nilifikiri wangemkalisha chini konda na dereva wa gari ili waulizwe namna wanavokatisha ticket zao pengine wanaajiri matapeli etc...na wewe ulikuwa unamtetea innocent abiria, walitakiwa wakushukuru kwa hilo kwasababu kuna watu wanaingizwa mjini sana na hao wakatishaji ticket ambao wameruhusiwa na wenye basi kabisa...cha ajabu, ni abiria walioko kwenye basi, badala ya kushirikiana abiria kwa abiria, wanasaidia konda..ajabu kweli...
   
 3. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ....Those are Tanzanians for You@! Woga mwiiingii na kutojua kutetea haki zao..!
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,010
  Likes Received: 2,790
  Trophy Points: 280
  sasa hao polisi walikuwa wanakupa msukosuko wa nini?...mi huwa nashindwa kuelewa hii dhana ya ulinzi shirikishi ni ipi...polisi wanahitaji elimu ya ziada...na hayo mabasi ya namna hiyo huwa yana matatizo sana na ukiangalia ndio yanayoongoza kwa ajali...dereva bangi tupu utingo ndo usiseme....siku nyingine bwana Shy panda Dar experess au Kilimanjaro, hutakutana na hayo yote
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,509
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahaha, preta umenifurahisha..unavutia kamba kwako ehee, umechoka na haya mabasi ambayo wameassemble bodi zake kenya..unataka yale yale ya kina mangi wenzetu....(nakutania lakini usichukie)...
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,010
  Likes Received: 2,790
  Trophy Points: 280
  usijali...mimi napenda nipande gari lenye ishara ya waaminio....kuna yale magari yanaitwa saibaba, kwa nyuma juu kulia huwa kuna kitambaa cheusi kidogo kinapepea...hilo hata unipandishe na bunduki bora unilipue...at least nikiona maandishi kama 'bwana ndie mchungaji wangu' au 'ni kwa neema tu' huwa napata faraja moyoni na hata safari inakuwa ya amani
   
 7. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Pole Mkuu Shy... Lakini hii ndio Tanzania yetu... Askari hawajui wajibu wao... kazi kunyanyasa raia wema tu kwa vi-sh. 1000 wanazoachiwa na makonda
   
 8. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana mkuu Shy kwa misukosuko ulokumbana nayo, eg. kupelekwa kituo cha polisi, kuvuliwa viatu,mkanda etc. pia hongera sana kwa ujasiri na msimamo wako. Lakini hawa askari wetu dah!!! balaa tupu.
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,816
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  "Kila goti litapigwa mbele za Bwana"
   
 10. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2010
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Sasa tupandishie hizo picha basi tuwaone hao makonda wakorofi si umesema ulibadilisha memory card? Tuwekee hapa tuwaone hao mafirauni wanaomwibia mzee wa watu maskini utakuta hiyo pesa aliifanyia kibarua miezi mitatu lol!!
   
 11. Muthaisu

  Muthaisu Member

  #11
  Jun 14, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Poleni lakini polisi wa kiafrika ni wa mama mmoja! hapa NZ policy are very helpful infact kuna kitu inaitwa citizen arrest wanaogopa sana!
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,175
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Sasa umeshawadai wenye basi kwa confinement na unlawful arrest. Maana hakuna kosa la jinai ulilofanya na bado ukawa arrested. Kuna mshiko mzuri tu usichelewe ndugu yangu. Changamkia tenda hiyo
   
Loading...