Abiria 17 waliokuwa wanasafiri kwa Basi la Kampuni ya BATCO wanusurika kifo

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Basi la kampuni ya BATCO lililokuwa lilitokea Tarime mkoani Mara kwenda Jijini Mwanza limepata ajali mbaya katika eneo la Pida Kyakabakari mjini Musoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philip Kalagi, ameithibitishia JamiiForums kutokea kwa ajali katika eneo la hilo na kwamba basi la kampuni hiyo limepinduka na kuacha njia na kuwa taarifa za awali zimeonyesha wapo majeruhi 17 ambao wamekwisha ondolewa katika eneo la ajali na kupelekwa Hospitalini.

Amesema majeruhi hao wamepelekwa katika Hospitali za Wilaya ya Bunda na Musoma kwa matibabu, na hivyo taarifa kamili juu ya tukio hilo zitatolewa baadae.
 
Ajiratime acha uongo. Limepinduka kweli, waliokufa papo hapo ni watano. Majeruhi wamepelekwa musoma na bunda. Nimezungumza na aliye eneo la tukio.
 
[h=2]basi la kampuni ya BATCO lililokuwa lilitokea Tarime mkoani Mara kwenda Jijijini Mwanza limepata ajali mbya kwa kutumbukia mtoni na abiria wote katika eneo la Pinda kyakabakari mjini Musoma.[/h] chanzo:ajiratime

Panaitwa Pida mkuu....
Poleni wote wahanga wa ajali hiyo
 
Ajiratime acha uongo. Limepinduka kweli, waliokufa papo hapo ni watano. Majeruhi wamepelekwa musoma na bunda. Nimezungumza na aliye eneo la tukio.

Sasa kaongopa nini, wewe nae bana
RIP marehemu na tunawaombea majeruhi wote Mungu awaponye kwa haraka
 
Kwani nimedanganya nini? soma tena bandiko langu

Mkuu Hujagundua Tu Ni Kwanini Nimeuliza a.k.a Ya Dully Sykes Ni Nini? Anyway Na Mimi Sasa Hivi Nimetoka Kuzungumza Madereva Wa Pande Zote Mbili Na Sasa Namalizia Kuzungumza Na Abiria Waliokaa Siti Za Mwisho.....Nitarudi!!!!!!!!
 
Panaitwa Pida mkuu....
Poleni wote wahanga wa ajali hiyo
Hiyo dawn ya pida ni noma! na hivi wachina walivyoijenga upya hiyo barabara....ni hatareee! Poleni wafiwa na mungu awaponye haraka majeruhi.
 
Uongo ulipost kuwa limeanguka mtoni na abiria wote. Kuanguka katika mto na abiria wote ni msiba mkubwa, jambo ambalo haliko kihivyo.
 
Manyrere sijaelewa umempinga jamaa nini na wewe umeeleza nini,maana jamaa hajasema waliokufa ila katoa taarifa za majeruhi tu.
 
Ajiratime acha uongo. Limepinduka kweli, waliokufa papo hapo ni watano. Majeruhi wamepelekwa musoma na bunda. Nimezungumza na aliye eneo la tukio.

Waliokufa au waliofariki?

Kuna mwandishi mmoja wa habari ameshawahi nieleza kuwa ni mwiko mwandishi wa habari kutumia neno kufa akihusianisha na mwanadamu aliyepoteza uhai...
 
Manyrere sijaelewa umempinga jamaa nini na wewe umeeleza nini,maana jamaa hajasema waliokufa ila katoa taarifa za majeruhi tu.

Mkuu, mleta mada kwenye headline yake alipotosha sana, nadhani Mod amerekebisha. Pili, hakuna mahali panaitwa kyakabakari. Pengine alimaanisha kyabakari. Kasema hiyo sehenu ipo musoma mjini!! Tangu lini kyabakari ikawa musoma mjini? Musoma mjini hakuna ajali. Kama alimaanisha kyabakari, basi ipo wilaya ya butiama. Haya makosa ndiyo maana nimewaka.
 
Back
Top Bottom