Abdurahman Kaniki angefaa kuwa IGP lakini alinaniliwa baadae akatupwa huko akawa balozi na sasa ni mstaafu na kaacha machapisho kadhaa yenye tija

Abdurahman Kaniki angefaa kuwa IGP lakini alinaniliwa baadae akatupwa huko akawa balozi na sasa ni mstaafu na kaacha machapisho kadhaa yenye tija

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,630
Reaction score
25,586
Huyu kamanda aliwahi kuingizwa kwenye kinyang'anyiro cha wale waliotajwa kuwa angeteuliwa kuwa IGP kwenye utawala wa hayati John Magufuli. Hiyo ni kwasababu huko nyuma tayari alikuwa Naibu wa Ernest Mangu aliyekuwa IGP tangu Mwaka 2013.

Baadaye baada ya kufanyiwa figisu aliendelea na cheo cha Unaibu IGP akipitwa na Kamanda Sirro ambaye aliteuliwa kuwa IGP na hayati Magufuli cheo ambacho kiufundi kilimfanya akae ofisini akisoma magazeti kutwa kucha.

Lakini baada ya hapo zengwe likaendelea cheo cha Unaibu IGP kikafutwa na kwa namna fulani Mwaka 2017 akapewa Ubalozi na akateuliwa na hayati Magufuli akaenda kuiwakilisha Tanzania huko Zambia.

Lakini katika kuangalia makamanda wasomi ndani ya Jeshi la Polisi nimeona huyu kamanda Kaniki anafaa hata kupewa kazi ya mkataba ili asaidie kulirekebisha Jeshi la Polisi kiutendaji na kimtazamo.

Ni msomi mzuri tu wa masuala ya usalama nchini na chapisho la kupata Shahada yake ya Uzamili katika Chuo cha Mafuzo ya Usalama cha "Transnational Crime and National Security: Issues and Options for Tanzania".

Kamanda mstaafu Kaniki ana Shahada ya Kwanza ya Sheria na Shahada ya Uzamili zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ingine ya Uzamili inahusu usalama na Stadi za Kistratejia na pia ana Shahada ya Udaktari wa Falsafa (Phd) kutoka Chuo cha Ulinzi Tanzania.

Mtu kama huyu ni wa kumtumia uzuri kutengeneza Jeshi letu la Polisi kwa kutumia ujuzi wake wa miaka mingi ndani Jeshi hilo na utaalam alionao kutoka darasani.

Kunaweza kufanywa ni kumpatia ajira ya mkataba wa miaka mitatu mitatu huku akiwepo aliye chini yake akijifunza kazi ambaye atachukua nafasi pindi afande mkuu atapomaliza mikataba yake rasmi.

Kwa hali ya sasa kiusalama wa raia na mali zao nchini na matishio ya watu kutekwa na kupotezwa sidhani kama IGP aliepo afaa kuendelea na kazi hiyo.
 
Kwani unadhani hao wengine wanaoboronga hawana elimu?
Na hilo swala la kusema ukampe mkataba tena mtu aliyestaafu ni ushauri wa kipumbavu kwenye Watanzania milioni 65 kuna watu wengi mno wenye CV nzito kumzidi yeye wanahitaji kazi.
Kama hakuleta impact yoyote kwa vyeo vyote alivyowahi kushika kabla ya kustaafu hata akipewa tena nafasi hakuna cha maana atakachofanya.
Umesoma nilichoandika au umekurupuka tu kuandika upumbavu?
 
Unataka kuniambia..…hakuna mtu mwingine ndani ya hilo jeshi mwenye CV kubwa kumzidi....?
Mkuu, labda wawepo sasa hivi ila kama tukiona hizo CVs pengine tutapata mtazamo mwingine.

Ila huyu kafungua njia na hata kama amestaafu, bado ni hazina ya kufundisha vijana.
 
Kwani tatizo la jeshi la polisi Tanzania ni maafisa wake kutokuwa na elimu au kuongozwa kwa maelekezo kutoka juu??
Tatizo ni kutotumia elimu yao na kusimamia misingi ya kazi bila kujali kiongozi ataka nini.

Ikitokea kiongozi akawa awafukuza kila IGP anaemteua kwa kusimamia hayo mawili( elimu na misingi ya kazi) kutatokea suluhisho.
 
Huelewi tatizo liko wapi.
 
Kama Taifa tukiwa na hiyo nia ya kulirekebisha Jeshi sawa.
Ila kama hakuna hiyo nia na utashi, hata uwe na wasomi wangapi ni kazi bure.

Nadhani pia huko jeshini wasomi wapo, sema ndio hivyo.
Kwa mfano polisi wakituhumiwa kishiriki kufanya "cover-ups" na serikali tiyari wameua imani kwa wananchi na wajitengenezea mazingira ya kufikishwa mahakamani endapo hali ya kisiasa ikibadilika.

Mfano mwingine ni kwamba haiwezekani suala la kipolisi linyamaziwe kwa polisi hao (Murilo na Misime) kushindwa kupata cha kuzungumza, lakini mtu asie polisi kama Msigwa ambae ni msemaji wa serikali ajitokeze kwenye runinga na azungumzie masuala ambayo ni ya kipolisi.
 
Huelewi tatizo liko wapi.
Naelewa uzuri sana tatizo lilipo ila nazungumzia zaidi ikitokea huko juu kunotoa maagizo kunapobadilika, watu kama hawa ndo wa kuwafikiria lengo likiwa ni kujenga upya au "rebuilding".
 
Huyu kamanda aliwahi kuingizwa kwenye kinyang'anyiro cha wale walotajwa kuwa angeteuliwa kuwa IGP kwenye utawala wa hayati Magufuli. Hiyo ni kwasababu huko nyuma tiyari alikuwa naibu wa Ernest Mangu aliekuwa IGP tangia mwaka 2013.

Baadae baada ya kufanyiwa figisu aliendelea na cheo cha unaibu IGP akipitwa na kamanda Sirro ambae aliteuliwa kuwa IGP na hayati Magufuli cheo ambacho kiufundi kilimfanya akae ofisini akisoma magazeti kutwa kucha.

Lakini baada ya hapo zengwe likaendelea cheo cha unaibu IGP kikafutwa na kwa namna fulani mwaka 2017 akapewa ubalozi na akateuliwa na hayati Magufuli akaenda kuiwakilisha Tanzania huko Zambia.

Lakini katika kuangalia makamanda wasomi ndani ya jeshi la polisi nimeona huyu kamanda Kaniki afaa hata kupewa kazi ya mkataba ili asaidie kulirekebisha jeshi la polisi kiutendaji na kimtazamo.

Ni msomi mzuri tu wa masuala ya usalama nchini na chapisho la kupata shahada yake ya uzamili katika chuo cha mafuzo ya usalama laitwa "Transnational Crime and National Security: Issues and Options for Tanzania".

Kamanda mstaafu Kaniki ana shahada ya kwanza ya sheria na shahada ya uzamili zote kutoka Chuo kikuu cha Dar-es-salaam, Shahada ingine ya uzamili inohusu usalama na stadi za kistratejia na pia ana shahada ya udaktari wa falsafa (Phd) kutoka chuo cha ulinzi Tanzania.

Mtu kama huyu ni wa kumtumia uzuri kutengeneza jeshi letu pa polisi kwa kutumia ujuzi wake wa miaka mingi ndani jehsi hilo na utaalam alo nao kutoka darasani.

Kinoweza kufanywa ni kumpatia ajira ya mkataba wa miaka mitatu mitatu huku akiwepo alie chini yake akijifunza kazi ambae atachukua nafasi pindi afande mkuu atapomaliza mikataba yake rasmi.

Kwa hali ya sasa kiusalama wa raia na mali zao nchini na matishio ya watu kutekwa na kupotezwa sidhani kama IGP aliepo afaa kuendelea na kazi hiyo.
Utoto unakusumbua
 
Kuna CV na uzoefu
Weye sasa ndo wafungua "pandora box" yaani waleta khasa maana ya mada.

Kwa wale watu ambao humaliza shahada ya kwanza na kuanza kazi mahala fulani kutegemea na aina ya kazi, ukitaka kwenda kusoma masters ni katika kuingia kiundani katika eneo lako hilo la kazi iwe rasilimali watu, biashara, uchumi na mengine.

Mmoja wetu hapo juu kasema tupo watu milioni 65 hivyo hatuwezi kukosa watu wanoweza kuwa IGP, jambo ambalo silipingi, lakini watu hao wana uzoefu wa kazi zao na shahada zao za uzamili zalingana na kazi zao?
 
Soma comment zote za wadau humu utaelewa kati ya mimi na wewe ni nani ameandika upumbavu.
Labda utuambie kwamba huyo mtu unayempigia debe una mahusiano naye ila vinginevyo hoja zako hazina mashiko.
Waona sasa upumbavu wako ulipoegemea?

Wote waloandika hapa wapo "objective".

Alieikopesha akili yako kufikiri kwamba mie nampigia debe ndugu Kaniki hapa ni nani?

Huu upumbavu ndo tusoutaka huu.
 
Huyu kamanda aliwahi kuingizwa kwenye kinyang'anyiro cha wale waliotajwa kuwa angeteuliwa kuwa IGP kwenye utawala wa hayati John Magufuli. Hiyo ni kwasababu huko nyuma tayari alikuwa Naibu wa Ernest Mangu aliyekuwa IGP tangu Mwaka 2013.

Baadaye baada ya kufanyiwa figisu aliendelea na cheo cha Unaibu IGP akipitwa na Kamanda Sirro ambaye aliteuliwa kuwa IGP na hayati Magufuli cheo ambacho kiufundi kilimfanya akae ofisini akisoma magazeti kutwa kucha.

Lakini baada ya hapo zengwe likaendelea cheo cha Unaibu IGP kikafutwa na kwa namna fulani Mwaka 2017 akapewa Ubalozi na akateuliwa na hayati Magufuli akaenda kuiwakilisha Tanzania huko Zambia.

Lakini katika kuangalia makamanda wasomi ndani ya Jeshi la Polisi nimeona huyu kamanda Kaniki anafaa hata kupewa kazi ya mkataba ili asaidie kulirekebisha Jeshi la Polisi kiutendaji na kimtazamo.

Ni msomi mzuri tu wa masuala ya usalama nchini na chapisho la kupata Shahada yake ya Uzamili katika Chuo cha Mafuzo ya Usalama cha "Transnational Crime and National Security: Issues and Options for Tanzania".

Kamanda mstaafu Kaniki ana Shahada ya Kwanza ya Sheria na Shahada ya Uzamili zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ingine ya Uzamili inahusu usalama na Stadi za Kistratejia na pia ana Shahada ya Udaktari wa Falsafa (Phd) kutoka Chuo cha Ulinzi Tanzania.

Mtu kama huyu ni wa kumtumia uzuri kutengeneza Jeshi letu la Polisi kwa kutumia ujuzi wake wa miaka mingi ndani Jeshi hilo na utaalam alionao kutoka darasani.

Kunaweza kufanywa ni kumpatia ajira ya mkataba wa miaka mitatu mitatu huku akiwepo aliye chini yake akijifunza kazi ambaye atachukua nafasi pindi afande mkuu atapomaliza mikataba yake rasmi.

Kwa hali ya sasa kiusalama wa raia na mali zao nchini na matishio ya watu kutekwa na kupotezwa sidhani kama IGP aliepo afaa kuendelea na kazi hiyo.
Hiyo nafasi atapew yule mama alotupwa ubalozini nje kule
 
Weye sasa ndo wafungua "pandora box" yaani waleta khasa maana ya mada.

Kwa wale watu ambao humaliza shahada ya kwanza na kuanza kazi mahala fulani kutegemea na aina ya kazi, ukitaka kwenda kusoma masters ni katika kuingia kiundani katika eneo lako hilo la kazi iwe rasilimali watu, biashara, uchumi na mengine.

Mmoja wetu hapo juu kasema tupo watu milioni 65 hivyo hatuwezi kukosa watu wanoweza kuwa IGP, jambo ambalo silipingi, lakini watu hao wana uzoefu wa kazi zao na shahada zao za uzamili zalingana na kazi zao?
Sawasawa, umeeleweka vyema
 
Back
Top Bottom