Abdulrazak Gurnah na imani hasi tuliyonayo juu ya uraia pacha

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Wengi wetu ndio kwanza tumefahamu kuwa mshindi wa nishani ya Nobel wa mwaka huu kwa upande wa fasihi ni Mtanzania mwenye asili ya Zanzibar Abdulraza Gurnah. Ndio kwa mara ya kwanza tumeviona vitabu vyake mitandaoni, vilivyompatia nishani yenye heshima na yenye kuambatana na pesa nyingi takriban dola milioni moja.

Utanzania wake umetokana na kuzaliwa visiwani Zanzibar mwaka 1948 na kukulia huko kabla hajasafiri kwenda Uingereza kutafuta maisha. Lipo somo la kujifunza kitaifa wakati suala la nishani yake bado lipo masikioni na vichwani mwetu. Gurnah ni mtanzania kabla hajawa raia wa Uingereza ni sawa na Wole Soyinka ni Mnigeria wa kuzaliwa kabla hajawa Muingereza au raia wa dunia.

Huyu Mzee ni mfano wa namna tunavyoshindwa kuvitambua vipaji vyetu vingi tulivyonavyo. Ni mpaka mtu awe maarufu ndio tunapoanza kufungua macho na kusema alaah kumbe huyo ni mtanzania!, yale yale ya Mwakinyo ni mpaka alipompiga Muingereza nio tukajua kuwa ni mdigo wa Tanga.Ni yale yale ya Yusuf Poulsen ni mpaka alipofunga goli Russia kombe la dunia ndio tukafunguka macho na kujua kuwa ni mdigo wa Tanga, wakati anahangaikia kuichezea Taifa Stars alisumbuliwa akadenguliwa na mwisho akakatishwa tamaa.

Ipo imani hasi juu ya uraia pacha, kwamba hao ni wageni na kibaya zaidi tunawaona kama ni wahujumu wa baadae wa mipango yetu ya kitaifa. Ni ubaguzi kama ule ule tunaofanyiwa na wazungu tunapopanda treni zao za Ulaya. Watendaji tunapokuwa ni sisi hatuzioni dhambi zetu hata kidogo!.

Pengine ndani ya vitabu vya Gurnah kuna maarifa mengi kama yale ya watunzi wa afrika ya mashariki, ndio sasa tunakwenda kuyafahamu wakati tungeweza kuyafahamu mapema zaidi. Ingekuwa ni tiketi ya maarifa yake yaliyothaminiwa huko Ulaya kujumuishwa ndani ya mifumo yetu ya elimu na wanafunzi wa sekondari wangekuwa wameshafaidika siku nyingi tu.

Pia tunalo tatizo la kutazama kila kitu kisiasa, huo urasimu mwingi uliopo ndani ya taasisi zetu ni wa kisiasa zaidi. Tunakwamishana pasipo sababu za msingi, ni mpaka mwanamichezo au msanii fulani anapokuwa 'katoka' kimataifa ndio eti tunasimama kuanza kumpigia makofi.

Angalau Rais Samia na waziri wa mambo ya nje Mama Mulamula wameonyesha utayari wa kulitazama suala la raia pacha katika mtazamo tofauti. Wapo tayari kuiangalia Diaspora ama vile inaundwa na wanadamu wenye miili yenye nyama. Huo ni mwanzo mwema wa kuishi na dunia inayotuzunguka kama unaishi na ndugu wa damu, sio umnyanyapae wakati anakuja ofisi za serikali mpaka akatishwe tamaa halafu maarifa yake yakithaminiwa huko nje ndio kinafiki unaanza michakato ya kuzifanya kazi zake zionekane zimefanywa na Mtanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom