Abdul Nondo anaweza kuja na maelezo yatakayowaacha watu midomo wazi

wewe usitafte watu
Hizi sifa za kijinga za kujiteka ili upate kiki za kisiasa ndio mbinu mpya ya kusaka dola hapo ufipa?? wewe usitake watu waagize vilainishi huku unastahili poda chunga domo lako tafadhal
 
Huyu dogo hakutekwa , Bali ilitengenezwa scene ambayo imebuma , kila kitu kitawekwa wazi soon
 
Yaani kuna watu mnaamini atarudi?Mnajua nia ya watu hao waliofanya hivyo?Mbona kuna wengine k.v. Ben,Azory hadi leo hawajarudi?Mashehe walirudi lakini unajua nguvu iliyo nyuma yao?Je kuna nguvu gani nyuma ya huyu kijana hadi muamini ataachiwa arudi?
Tayari ameshaachiwa mkuu!!
 
Mkuu umenikumbusha sakata la kutekwa Ulimboka baada ya mgomo wa madaktari nchini na kuahidi kusema kila kitu lakini baada ya kupata nafuu hakusema lolote lile. Na huyu alitekwa wakati wa Kikwete na Serikali yake haikutia neno.


JK naye hakuwa mtu mzuri. Utawala wake ndio uliasisi haya yanayoendelea leo hii.
 
Wasiojulikana lakini wana bunduki na kila kitu na wanaingia maeneo ya ulinzi muda wote - hili ni neno tu linatumika watu wanazugwa.
 
nakubaliana na mtoa mada, yaan huwez kupata ukweli kwa mtu aliye tekwa. angalia Roma kwenya press alisema kitu tofaut na matarajia ya wengi. chakushangaza kwenye wimbo akaimba kitu tofauti. bila kuwa msanii tusingepata picha kwamba waliomteka ni askari, na aliye mteka kateka mpaka uchaguz wake. na kumshukuru mtekaji aliyetabiri kupatikana kabla ya jumapili. yaan yote haya kwenye press hakuongea hata moja
 
JK naye hakuwa mtu mzuri. Utawala wake ndio uliasisi haya yanayoendelea leo hii.

Mkuu kwa hili nakuunga mkono kwa asilimia 100. Huwa nashangaa watu wakija hapa jukwaani na kuanza kumsifia JK. JK pia hakuwa mzuri, bali aliamua kunyamaza kwakuwa alikuwa naye kachoka na hiyo kazi. Lakini unyama huu unaoendelea sasa kwa kasi, muasisi wake ni JK. Awamu hii imeweza kutekeleza hilo kimachomacho maana mkuu wake hawezi siasa za ushindani na haendi ulaya/US hivyo hana hofu ya kuhojiwa huko nje. Kilichomfanya JK akawa anatekeleza haya mambo kwa siri ni kwakuwa alikuwa anapenda sana kwenda nchi za nje hivyo alijua angekutana na maswali magumu.
 
Wote waliotekwa na kuachiwa hawajawahi kurudi wakiwa kama walivyokwenda. Siyo ajabu akafanywa kama Slaa ama Ulimobka, Au Roma. Hawezi kuwa the same person.

Watch and see!
Huyu katoka hana hata mchubuko.Usisahau inadaiwa ni kada fulani ndio kawa wa kwanza kumpa msaada.
 
Huyu dogo hakutekwa , Bali ilitengenezwa scene ambayo imebuma , kila kitu kitawekwa wazi soon
Hawa watu Mungu kawanyima maarifa ndio maana kila siku wanavurunda katika mipango yao.Hili huwa nalisema mara kwa mara.
 
Wasiwe tu wamemfanya dogo vibaya kisha wakamchukia video kwa vitisho aseme vile wanataka wao,, na iwe n kumnyamazisha moja kwa moja
Nasikia huu mchezo upo...hata roma kuna waswas huu kwani udume wote kama rapper hana tena.
Unafanywa then unaambiwa ukinyanyua domo tuna ieneza mitandaoni.
Utabana kimya tu
 
Huyu kijana anaweza kuja na maelezo tofauti kabisa na jinsi watu wanavyotarajia maana nae ni mtanzania kama walivyo kina Dr.Slaa,Katambi na wengineo unless ameumizwa.

Msisahau hata wale mashehe baada ya kuachiwa walikuja na maelezo ya kushangaza sana kuwa waliowateka eti hawakuwa na nia mbaya.

Tusisahau pia kuna hoja ya Bashe ambayo inatakiwa kungia Bungeni kuhusiana na matukio haya hivyo tukio hili huenda liko kimkakati kizaidi.

Ukweli kuhusu matukio haya kwa sasa kamwe hatuwezi kuupata kutoka kwa wanaotekwa na pia kamwe hatuwezi kuupata kutoka kwa watu wanaotuhumiwa kutenda mambo haya. Kumbukeni hata ya Roma Mkatoliki

Pia unaweza kutekwa na kisha kwa usalama wako ukaambiwa utoe maelezo yatakayowafurahisha au kuwasafisha waliokuteka.

Katika kuhada umma wako wanaoweza kununuliwa alafu hao hao tukasikia wamatekwa na kisha baadae kupatukana lakini wakiwa na maelezo ya kushangaza kabisa.

Mimi mwenzenu sina imani mpaka pale tutakapokuja kubadili watu waliokalia ofisi muhimu za nchi hii.

Hawa watu wana kiburi kwasababu wao ndio kila kitu na wao ndio wameshika sehemu zote muhimu na ndio maana wanaweza kufanya hivi kila sik bila ya hofu yeyote.
Mkuu una akili mno ! Nimemsikiliza RPC wa Iringa , nimegundua kuna mchezo wa kishamba sana anaotaka kuucheza , halafu nimemcheka kwa dharau sana !
 
Back
Top Bottom