Abdul Nondo afunguka kuhusu bodi ya mikopo

Abdul Nondo afunguka kuhusu bodi ya mikopo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917



Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa kigezo cha bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa kuzingatia tu wanafunzi waliosoma shule za serikali na kuwabagua wale waliosoma shule za private si sawa kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwakosesha haki watu kusoma.

Abdul Nondo amesema hayo siku moja baada ya kauli ya Rais Magufuli kusema kuwa bodi ya mikopo haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi ambao awali walionekana kusoma katika shule za binafsi na kudai kuwa watu hao wanauwezo hata wa kusomesha na wazazi wao ndiyo maana waliweza kusomeshwa katika shule binafsi walipokuwa wakisoma.

"Mara ya kwanza kabisa, niliwahi sikia kauli ya namna hiyo kwa Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi akisema kama umesoma private school hupati mkopo. Kauli hii tuliipinga vikali, kipindi hicho na tukasema sio fair sababu gharama za chuo ni kubwa (Ada, hela ya kula ,copy, usafiri,hela ya malazi, hela ya mafunzo kwa vitendo field). Ni tofauti kabisa na fedha ya ada shule ya private laki 8, au mil 1 ambayo pia watu husoma kwa ada hiyo private. Kuwanyima mkopo ni kuwakatishia ndoto zao kabisa"

Nondo aliendelea kusema kuwa sababu nyingine ni kuwa uwezo wa mzazi unaweza kubadilika badilika inawezekana kipindi cha nyuma alikuwa na uwezo wa kulipia gharama lakini kipindi mtoto anaingia chuo labda mzazi amepatwa na magonjwa ya kudumu, uchumi umeyumba kiasi cha kushindwa kumudu gharama hizo jambo ambalo linapelekea wanafunzi wengine kukosa haki ya kusoma elimu ya juu.

"Mfano kipindi mtoto akiwa anasoma 'private' mzazi alikuwa na uwezo wa kulipa, kipindi mtoto anaingia chuo baba au mzazi amepata magonjwa, ameparalyze, amefilisika, kumnyima mkopo mtoto huyu ni kumkatishia malengo yake. Pia tulihoji juu ya kama mtoto amesoma kwa kudhaminiwa inakuwaje, kuna wanaodhaminiwa kusoma private schools na mashirika binafsi, watu binafsi, na husomeshwa shule tuu sio chuo, baadaye hutelekezwa chuo wajitegemee. Hii bodi ya mikopo walisema wataweka kipengele kuambatanisha vielelezo vya udhamini ila huwa ni geresha tuu huwa hawatoi hata uambatanishe ndio maana sio sahihi kutoa mkopo kwa kigezo cha u private schools, au u government schools siyo haki"

"Tulihoji pia wapo waliosoma kwa kurUdia mitihani kutafuta 'credits' mara nyingi hawa huwekwa katika kundi la private schools, wapo QT (qualified Tests), wapo diploma wote hawa huwa termed as private schools. Kuwanyima mkopo kwa vigezo hivi ni kupoteza ndoto zao. Kigezo cha kutoa au kutotoa mkopo kwa kuangalia ulisoma private au government sio kigezo sahihi. Kime katisha ndoto za wanafunzi wengi saana sababu hakitoi majibu halisi ya uwezo wa mwanafunzi kustahimili gharama"

Mbali na hilo Abdul Nondo amesema bodi ya mikopo sasa imekuwa ikikusanya marejesho ya mikopo kuliko kipindi chote kama ambavyo wao wenyewe wamekuwa wakisema hilo hivyo amewaomba kigezo hicho cha kuangalia mwanafunzi alisoma shule gani na kumpa mkopo huku wengine wakikosa mkopo kutokana na shule walizowahi kusoma siyo haki na kuwa kitendo hicho ni kukatisha ndoto za watu kusoma elimu ya juu.

"Hakuna kipindi bodi ya mikopo wanakusanya makusanyo na marejesho Kama kipindi hiki, tuwasii bodi ya mikopo hiki kigezo hakifai. Kama bodi ya mikopo wataamua kukitumia kama kigezo cha kukosa mkopo, basi tunawaomba waandike katika muongozo wao wa 2018/2019 .Wakiongeze kuwa "Kama ulisoma shule ya binafsi hupati mkopo" ili wazazi wajipange mapema na wajue kuwa mtoto akisoma private school hapati mkopo kutoka bodi ya mikopo. Itasaidia ikifafanuliwa hivyo"
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Tatzo lenu lumumba mmekuwa misukule ambyo haifikirishi ubongo hata kidonga.

Dogo yupo clear kabisa kuwa uwezo wa mzazi unaweza badilika muda wwte.

Mimi nilsoma shule za serkal had form 6. Mzaz wangu alikuwa na kipato cha chin sana. Ila baadye altusua mapene nakuweza nisomesha chuo na wadogo zangu walionifata walisoma private.

So mzazi kusomesha mtoto serkal au private sio kipimo cha finance ya mzazi. Kuna wengine hata wazazi wao walifariki kabla hawajafika chuo na walkuwa wakiwasmesha private.
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Huenda ulisomeshwa na mjomba lakini leo mjomba, katumbulia just a small case!
 
Nondo yupo nondo kweli kweli,

Endelea kupaaza sauti na kutetea wanyonge Kijana mwenzangu.

"Maisha yangu yana ubora,mwenzangu unaubora gani..? Hata nikiwa bora nani atakaye kuwa bora nami"

Taifa letu litakombolewa na kizazi chetu vijana!
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3

Mbona mnajitoa ufahamu hiyo milioni 2.5 na zaidi kumbuka unalipa mtoto yuko shule ,maradhi ,chakula,sujui usafiri vyote vimo kwenye Ada,tofauti na Chuo wee unalipa hio 1.9 au 3m.mambo mengine Chuo hakihusiki nacho utajijua utalala wapi,utakula wapi utafikaje Chuo kumbuka gharama ya stationery ni kubwa Sana kununua handout nk
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Mkuu usijitoe ufahamu, hiyo 1.5 ya chuo ni ada (school tuition fee) pekee bado madudu mengine kibao pesa kama hiyo au zaidi.

mkosoe Nondo ktk siasa zake zingine ila sio kwa hili la mikopo. dogo yupo sahihi kabisa.
hali ya kiuchumi hubadilika. Kuna kupunguzwa kazini, kampuni yako au uliyo ajiliwa kufilisika, kuugua n.k. vinaweza kupelekea mzazi kushindwa kuendelea kumlipia mtoto elimu ya juu kam private.
 
Ila tuongee ukweli kama umeweza kulipa zaidi ya 2.5 kwa miaka 7 ongeza 4 ongeza 2 halafu leo 1.5 ya chuo itakushindaje miaka 3
Sorry, kabla hatujaingia ktk mjadala kama huu, tujiulize je serikali inapotoa pesa kama hii ya mkopo chanzo cha serikali ni nini?, jibu ni kodi. Kama ni kodi je mtoto wa private school mzazi wake halipi kodi?.
 
Back
Top Bottom